Hizi shule za gharama zinawafilisi wazazi, au zinawachelewesha kupata maendeleo; kuna mtu namfahamu, kipato chake laki 5, kasomesha mtoto chekechea mpaka la saba, ada shilingi milioni 2.5 kwa mwaka; kijana akafaulu na kupangiwa shule ya serikali.
Akampeleke tena private, kwa ada ya milioni 3 kwa mwaka; sasa yuko kidato cha tatu; mzazi wake ana ha ha; ata kununua nguo mpya avae imekuwa shida.
Mwisho wa siku, huyu kijana atakuja akutane na kijana aliyesoma kayumba pale chuo kikuu; sasa hapo sijui ni nani ataonekana mjanja?