Hizo ni hisia zako, na huenda zimetokana na uzoefu wako binafsi, ila sio lazima iwe hivyo, kuna wanawake wengi wenye mtoto wameolewa bila shida, wanafurahia ndoa zao na pia kuna wadada kibao hawajaolewa na wala hakuna dalili ya kuolewa, pamoja na kwamba hawana watoto. Hiyo ni dhana potofu, tatizo sio kuwa na mtoto, tatizo ni kuwa na sifa za kuolewa, waoaji wanaangalia sifa bora za mke na haijalishi kama ana mtoto ama hana. Kama wewe mdada unahisi huolewi kwasababu una mtoto, huo si mtazamo sahihi, jiangalie upya, yawezekana huolewi kwasababu huna sifa za kuolewa na wala si kwasababu una mtoto. Kuna wadada wenye nafasi kubwa sana ya kuolewa pamoja na kwamba wana watoto, kwasababu ya ubora wao wa kuwa mke.