Tatizo biti inatengenezwa na mtu mmoja.Nilikuwa naangalia Sauti Sol daah wale jamaa,yule mpiga gita wao anaplay part kubwa sana ya kupata biti unique wanapoingia studio,plus na wao wana uwezo wa kupiga vyombo vya muziki,product inayotoka hapo lazima iwe unique.
Bongo producer mmoja anafanya kazi kibao,kila kitu anafanya yeye lazima biti zitajirudia,kichwa kinachoka mwisho wa siku ubunifu unakuwa hamna.
Lakini kama biti ingekuwa inatengenezwa na watu wengi lazima biti zetu zingekuwa na upekee.
Ila tusiwalaumu maproducer tatizo wasanii wa bongo fleva hawapi thamani maproducer wanawazulumu kila siku,tena kama hawa wenye majina wanapenda dezo utawasikia "bila mimi wewe wasingekujua.....",wakati msanii mwenyewe hajui kupiga hata manyanga,vocal yenyewe ya kawaida.