LOOOoooh!Wenye akili hatutakusikiliza! Ulikuwa sehemu ya mfumo kandamizi, hukusema lolote ukitetea kwenda "chooni". Leo usitudanganye, ni kwa vile uko nje ya mfumo, lakini huna dhati ya moyo kutetea haki!
Kama ulikubali kushirikiana na wauaji wa wakati ule, leo nyamaza! Nyamaza kabisa, wahutubie hao "ngedere" wasiojua kuwa ukiunguza msitu ukachekelea unaungua, ikifika jioni usilalamike wapi pa kulala!
HUU UKWELI, NA NI UKWELI MTUPU, ALIOUSEMA JANA ALIBIDI AUSEME AKIWA NDANI YA MFUMO AU ATOKE.KUONESHA KUWA HAKUBALIANI NA UKANDAMIZAJI DEMOKRASIA
KAMA AKINA MBOWE, LISU, LEMA , HECHE NA WENGINE WENGI AMBAO SIJAWATAJA WALIVYOKITETEA WANACHOKIAMINI MPAKA WENGINE KUFA
Sijui kwa nini mara nyingine huwa sikuelewi vizuri mkuu 'Retired'.
Kama hapa, nashindwa kuelewa hasa kwako ni nini na huyo Tibaijuka.
Kwani lengo kuu ni lipi hasa... Kama Tibaijuka pamoja na historia yake mbaya ya huko nyuma sasa anasaidia kufikia lengo lile lile kuu sasa hivi, shida iko wapi hadi bango linyanyuliwe juu yake!
Kadai hisa iwapo lengo litafikiwa, ili na yeye awe sehemu ya hao watakaochukua kampuni?
Leo hii ukiniambia nikaombe msaada kwa shetani ili haya mazimwi yanayo tuandama yatokomezwe, nitamsikiliza huyo shetani bila ya ahadi yoyote ya kumpa ushirikiano baada ya kazi kufanyika. Hali imefikia hatua hiyo mbaya.
Kwani kati ya Tibaijuka na hilo genge la Samia wewe unaona ni nani hatari zaidi kwa waTanzania?
Kwa hiyo nazidi kukushangaa sana kwa mada yako hii.