Prof. Anna Tibaijuka, ulikaa kimya wakati unahudumu katika Serikali kandamizi ya hiki unachokikemea sasa kulinda maslahi yako, na sasa kaa kimya!

LOOOoooh!

Sijui kwa nini mara nyingine huwa sikuelewi vizuri mkuu 'Retired'.
Kama hapa, nashindwa kuelewa hasa kwako ni nini na huyo Tibaijuka.

Kwani lengo kuu ni lipi hasa... Kama Tibaijuka pamoja na historia yake mbaya ya huko nyuma sasa anasaidia kufikia lengo lile lile kuu sasa hivi, shida iko wapi hadi bango linyanyuliwe juu yake!

Kadai hisa iwapo lengo litafikiwa, ili na yeye awe sehemu ya hao watakaochukua kampuni?

Leo hii ukiniambia nikaombe msaada kwa shetani ili haya mazimwi yanayo tuandama yatokomezwe, nitamsikiliza huyo shetani bila ya ahadi yoyote ya kumpa ushirikiano baada ya kazi kufanyika. Hali imefikia hatua hiyo mbaya.

Kwani kati ya Tibaijuka na hilo genge la Samia wewe unaona ni nani hatari zaidi kwa waTanzania?

Kwa hiyo nazidi kukushangaa sana kwa mada yako hii.
 
Bwashee umewaona Dr Nchimbi na Tundu Lisu kwenye kongamano? 🤣🤣
 
Bi mkubwa ana tofauti na yule maria sarungi,kipindi cha jk alikua mmoja wa wanufaika alikula kimya,alipoingia jpm akagusa ugali wake acha acharuke!wanakuwaga sio wastahimilivu hao
 
Unawezaje kuikosoa serikali ambayo unatumikia? Ukiwa nje ya ulingo ndipo unaweza kujiachia kwa lolote. Profesa yuko sawa kabisa.
 
Ni kweli anaongea ukweli lakin hana sifa tena ya kuongea kwa kuwa alishapoteza hiyo sifa. Mfano ukipata kifungo gerezani na kuhukumiwa tayari huna sifa tena ya kugombea urais ingawa unaweza kuwa unaongea vizuri.The same to your prof.
 
Kama kaungama na kutubu muache na yeye apaze sauti kutetea haki za raia.
 
Ni kweli anaongea ukweli lakin hana sifa tena ya kuongea kwa kuwa alishapoteza hiyo sifa. Mfano ukipata kifungo gerezani na kuhukumiwa tayari huna sifa tena ya kugombea urais ingawa unaweza kuwa unaongea vizuri.The same to your prof.

Hajawahi hukumiwa kwa hiyo issue. Au wewe ulimhukumu? But ukienda gerezani kwa wizi ukatoka akawa mtu mwingine anaiba una nafasi nzuri ya kumwonya huyo ubaya wa gereza. Ana haki kikatiba ana anaitumia. Aaachwe aseme. Mbowe ameshawahi gerezani so haruhusiwi kuonya watu kuhusu ugaidi?
 
sijamkataza kusema na sina nguvu wala mamlaka hayo. My point is , huyu msimuamini! Mtu akibaka mtoto , kesho utamwamini kumuachia mtoto kuwa eti katubu? Uwe na mashaka naye. Do you want to say Samia akimuita atakataa wito kuwa wewe ni dhalimu siwezi hudumia serikali dhalimu? Mbowe et al walikataa kutumikia serikali dhalimu, and faced and still are facing the consequences!
 
Unawezaje kuikosoa serikali ambayo unatumikia? Ukiwa nje ya ulingo ndipo unaweza kujiachia kwa lolote. Profesa yuko sawa kabisa.
Mnafiki, unaachana na uteuzi wao maana unaamini katika haki! Watu waadilifu huwa wanajiuzulu kutumikia wdhalilmu, yeye hakufanya hivyo.... akapata vihela vya mboga!
 
Kwanini akae kimya?
 
Bado akiamua atakaa kimya tu. Lakini kama amegeuka na kuacha uovu akageukia Wema basi Tumshukuru kwa hilo aungane nasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…