Muda mwingine jitahidi ushirikishe ubongo wako vyema kabla ya kuja kuandika huu ujinga ulioandika hapa, inawezakana vipi triolini 20 kuibiwa ilihali tumeona wakati wa uhai wake miradi mingi mikubwa ya kimkatakati ikiendelea kujengwa na kukamilika.
Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni, na imani hata kama ulaji ulikuwepo ila si kama tulivyoanishwa na ripoti ya CAG, hata kipindi cha Hayati Mkapa, hata mstaafu JK ufisadi ulikuwa mkubwa mno hata kwa huyu mama siku akitoka madarakani mtajua ni jinsi gani alivyofuja fedha za umma, “Embu tujaribu kuwa na akiba ya maneno”.
Kuna mkakati ambao unaendeshwa chinichini na kikundi fulani kumchafua Hayati Magufuli ila na uhakika hawataofanikiwa kamwe maana watu hao hao ndio wanapita katika madaraja yaliyojengwa na huyo wanaemuita mwizi.
Hii dhambi haitowaacha salama kama ambavyo libya inateseka kwa sasa baada ya kumuua Ghadafi, huyu huyu mnaemnanga na kumsingizia kila aina ya uovu akiwa kalala mavumbini ipo siku mtamkumbuka.