Prof. Assad: Niliondolewa kazini kinyume na taratibu kwasababu nilikuwa sifuati maelekezo ya Mtu

Prof. Assad: Niliondolewa kazini kinyume na taratibu kwasababu nilikuwa sifuati maelekezo ya Mtu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Niliondolewa Ofisini kinyume na taratibu kwa sababu nilikuwa nasimamia na kufanya kazi kwa kufuata taratibu na miongozo ya kazi na sio maelekezo ya mtu,kuna mahali viongozi wetu wanashindwa kusimamia wanachokiamini kwa hofu ya kuporwa V8, wanahofu kukosa riziki.

Hili suala la kuniita CAG aliyemaliza muda wake binafsi linaniudhi, katiba ibara ya 144 inatamka wazi muda wa kumaliza na sababu za kukoma kuwa CAG, mimi nilipotolewa ofisini sikuwa nimemaliza muda wangu. Nadhani hatukuwa wazuri katika kusimamia katiba.

Mussa si jina langu, jina alilonipa baba yangu ni Jaffar. Wakati nasoma kulitokea matatizo fulani, ikabidi nitoke sehemu moja kwenda nyingine ili kumaliza masomo na hili jina la Mussa nikalipata huko ila watu wanaonifahamu wananijua kama Jaffar- Profesa Mussa Assad, CAG wa zamani.

Analazimisha kuonekana ni mtu msomi anaejielewa ana misimamo.

Bahati mbaya alikutana na Chuma.

Nilichokuwa nampendea yule baba JPM ukijifanya wewe ni wa muhimu sana kwenye hii nchi yeye anakuonesha namna ulivyo takataka tu na nchi inaweza kwenda mbele bila wewe hahahah.

Profesa uliondolewa na kidume sasa unalialia nini!!?
 
😄😄 Hatimae nchi inaenda bila yeye aliyejiita jiwe, aliyekua anajisemesha eti akiwa hayupo nchi hii itaendaje as if aliiumba yeye nchi hii 😁😁😁😁
 
Back
Top Bottom