Prof. Assad: Niliondolewa kazini kinyume na taratibu kwasababu nilikuwa sifuati maelekezo ya Mtu

This man is a genious aise, halafu ana maisha simple sana kuna kipindi nilipishana nae pale millenium tower akisubiri usafiri wa Uber.
Kwa hiyo mkuu mliongea akakuambia anasubiri uber??
 
Kabla hajaondoka alidai atakuja gombea umalaika mkuu, labda yuko huko.
Mkuu yaani huo Moto wa Jehanamu utamwachia? Tayari ni member wa Lucifer hawezi kuwa Malaika hata kwa ndumba.
 
Mpaka Leo zile 1.5 trillion alizohoji CAG Assad hazijawahi kutolewa majibu yenye mashiko. Chattel Chattel priorities.
 
Profesa uchwara aliyejifanya mhimili wakati mihimili iko 3 tu.

Ajaribu kugombea urais basi labda timu gaidi watamsajili 2025.
Siku zote ukweli una uma. Hajadai urais bali ametoa hoja yake ya kuondolewa nafasi ya kazi ajili ya kufata taratibu za kazi na sio maagizo ya mtu. Jibu kwa hoja.
 
acha kujichekesha kwangu,wewe ni nani mpaka uwapangie watu wakati gani aongee nini. BTW Assad hii sio mara ya kwanza kuongea hiki,au ulitaka akiongea aje akupe ripoti?
Sasa na wewe uache kuni bebisha kwangu....wewe ni nani mpaka unipangie cha kuandika? Umezungusha mikono mpaka akili nayo imezunguka... Lowassa fisadi au si fisadi?
 
Jibu hoja alio toa ni kweli au sio kweli na toa ushahidi toka katiba na sheria za nchi. Labda kama unakubali na wewe yakufike.
 
Ripoti tu ya soko la k/koo waziri mkuu alitoa wiki hadi leo imekata miezi kimya.
Mpaka Leo zile 1.5 trillion alizohoji CAG Assad hazijawahi kutolewa majibu yenye mashiko. Chattel Chattel priorities.
 
Auditing ni muhimu sana kwa makampuni yanaongozwa na company act na procedures zinaeleweka za kumu engage auditor users wake ni Shareholders and other interested users ila kwa nchi kitu pekee kinachomuongoza CAG ni Katiba tuu ambayo inaelezea kuanzia engagement yake mpaka mengine, na users wake ni General public.

Mwanataaluma huyu anachoongea sio cha kubeza japo yaliopita si ndwele tugange yajayo.
 
Hasira za Tril 1.5 alizopiga hayati na zile million 400( za umma) za matibabu ya Ndguyai nchini India ndizo zilizotengeneza fitna na hila kumtoa Prof Assad ofisini kabla miaka yake miwili ya kustaafu haijafika.
 
Hasira za Tril 1.5 alizopiga hayati na zile million 400( za umma) za matibabu ya Ndguyai nchini India ndizo zilizotengeneza fitna na hila kumtoa Prof Assad ofisini kabla miaka yake miwili ya kustaafu haijafika.
Some katiba kuhusu muhula wa CAG; ni miaka mitano, ambayo Assad alimaliza. Baada ya hapo, Rais anaweza kumteua tena kwa muhula mwinginemmoja wa miaka mitano tena, lakini JPM hakumteua. Asilalamike bali asome Katiba ajue inasemaje.
 
Kidume hakipo ila watu kawaachia maumivu makali hawataa wapate recovery...ni kulialia mpaka wanakufa nao [emoji1][emoji1][emoji1]
Magufuli pia walimuua kwa kujifanya anajua sana, ndio maana kifo chake kilikuwa na utata mwingi

Na yeye ndio alikuwa akijiona bila yeye nchi haitaenda,
 
Hasira za Tril 1.5 alizopiga hayati na zile million 400( za umma) za matibabu ya Ndguyai nchini India ndizo zilizotengeneza fitna na hila kumtoa Prof Assad ofisini kabla miaka yake miwili ya kustaafu haijafika.
Jmn kuiba trilun 1.5 CYO mchezo aibe wapeleke wapi labd ndio kajengea madaraja jmn duh na kufince Kaz zingine
 
Kidume chako kiko wapi kwa sasa?

Chuma hakina ujanja mbele ya kutu.
 
Mwenzio kaacha legacy chuo kikuu UDSM na pia as one of the best CAG... vp wewe una legacy yeyote zaidi ya UCHAWA?
Best CAG alikuwa Utuoh; alimaliza kipindi chake akiwa anaheshimika sana. Assad hakuwa na legacy yoyote ya kuacha pale UDSM, aliondoka akiwa associate professor mwenye journal papers 14 tu, nusu yake zikiwa ni local kwenye journals za NBAA na IFM.

Yeye hakusomea kuwa CAG, hiyo ni position ya uteule tu. Baada ya kuondolewa nafasi ya CAG alitakiwa arudi UDSM. Condoleeza Rice alipomaliza kuwa Secretary of State marekani alirudi Stanford kuendelea kuwa profesa wa public policy. Steven Chu (Nobel laureate) alipoacha nafasi ya Secretary of energy, alirudi Stanford kuendelea kama profesa wa Physics.

Kwa nini jamaa huyu analalamikia nafasi za kuteuliwa kila siku na kusahau ukweli huo kwake yeye kama "msomi"? Nadhani alijua ameula miaka kumi tena, akatupilia mbali lecture zake zote. Baada ya kutimuliwa akawa hawezi kufundisha tena kwa vile alishatupa lil desa la kufundishia.

Miaka ya 2006-2007 kulikuwa na member mmoja hapa anaitwa Nungwi alikuwa akimshambulia sana huyu bwana kuwa hana lolote kichwani; inawezekana kweli Nungwi alikuwa akimfahamu jamaa huyu vizuri sana kuliko sisi wengine wakati huo.
 
Huyu mzee mpuuzi tu, mbona hakuyasema haya kipindi cha Mwendazake? Sasahivi ni kama anatafuta huruma ya SSH ili ampe cheo... Zama zake zilikwisha akubali matokeo sio kulia lia kila siku kama mtoto wa kambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…