Prof. Baregu na Prof. Safari mpo wapi katika kuanguka huku kwa CHADEMA?

Shida ya chadema wanaamini kwenye chama chao hakuna tatizo, hawajui kwamba kuamini hakuna tatizo ndio tatizo lenyewe.
 
Itikadi haifi wala haianguki iko ndani ya mioyo ya watu ,mnajidanganya Sana.
Kweli kabisa itikadi haifi ndani ya watu makini. Wengi tulidhani CDM kina itikadi na watu makini. Ilishangaza sana mwaka 2015 itikadi kupigwa teke na kufutwa mpaka kwenye website ya CDM kisa ili apokelewe mgombea urais. Wale wasiokubaliana wakaitwa wasaliti
Yaani si wasaliti wa itikadi bali wasaliti wa wale wasiokuwa na itikadi. Sishangai watu makini kama Prof Safari au Prof Berega au hata Mabere Marandu kujitenga baada ya kugundua hakuna iitikadi ndani ya watu wale.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maprofesa wawili mulioko ndani ya CHADEMA munafahamika vizuri sana kwa ubobezi wenu. Prof. Baregu ni mzuri sana katika sayansi ya siasa, umewafundisha wengi na wamefanikiwa. Prof. Safari yuko vizuri katika sheria. Ni kesi nyingi umeonesha umwamba wake. Wanasheria wengi ni matokeo ya juhudi zako na uwezo wako. Wote munastahili sifa.

Watu hawa wawili nimekuwa nikiwatumainia sana muisaidie CHADEMA. Sifahamu kwanini kipindi hiki mumekuwa kimya kiasi kwamba msaada wenu hauoneakani. Yawezekana msada wenu hauhitajiki. Muelekeo wa CHADEMA kwa sasa ni aibu kwenu ambao mulistahili kuonesha muelekeo unaofaa.

Binafsi nahisi labda mulifanya makosa kuona malengo ya CHADEMA yalikuwa ni yapi. CHADEMA hawako ktk siasa, wako ktk biashara na bahati mbayamaprofesa wawili, kwa pamoja. Biashara ya udanganyifu hamuiwezi.
Walishaondoka hawapo tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema inaanguka au hayo ndio matamanio ya ccm? Mmepiga propaganda wenyewe, mmewanunua baadhi ya viongozi wa cdm kwenye ile nia ya Magufuli kuhakikisha anaiua chadema, sasa naona mnajaribu kuchukua mrejesho kama chadema imekufa. Sisi washabiki wa cdm tuko imara na hatuyumbi kwa hizo hujuma za wazi. Hizo mbinu mnazotumia sasa hivi ccm mlifanikiwa enzi za kizazi kilichopita cha NCCR ya Mrema, CUF ya Lipumba nk, ila kwa mbinu hizo za kichovu, sio rahisi kuwapata watu wa kizazi hiki.

Kizazi hiki Ni next level, Kiko digital tayari huku ccm ikiwa bado analogia, ndio maana mbeleko halisi ya ccm ni vyombo vya dola na kundi la watu wasiojulikana. Ili mjue kizazi hiki sio cha kuongozwa na ccm tena, acheni tume huru ya uchaguzi, kisha tuingie kwenye uchaguzi kila mtu awe na nguvu yake ya kisiasa kisha mje mlete mrejesho hapa jukwaani.
Mkuu unaishi utopia. Unaishi kwenye fikra na hisia na siyo uhalisia. Hivi ulitaka CDM ifeje ili ujue imekufa. Ndani ya kipindi cha miaka 2 Chama kimekimbiwa na zaidi ya wabunge 15 Madiwani ndo usiseme. Kimepoteza ngome zake kuu zote za arusha na moshi. Hiyo Tume ya Uchaguzi hata mbowe awe Mwenyekiti hamtoboi. Kwasababu huko nje chama kimepoteza mvuto mmebakia mashabiki wa kwenye mitandao.

Lakini nikubaliane nawwe kwakuwa umejipambanua kama mshabiki wa CDM. Unapokua mshabiki wa jambo fulani mara chache sana kuona udhaifu wa kitu unachoshabikia na imani yako inakua ni kubwa sana katika jambo hilo.

Ninajua siasa kwa kiwango cha kuridhisha, chama kupoteza mvuto ni pale siasa zinapokuwa zinafanyika. Kama siasa hazifanyiki unatumia kipimo gani kujua kuwa chama kimepoteza mvuto? Chini ya Magufuli hakuna siasa za ushindani wala ushawishi, bali kuna siasa za shuruti. Kinachofanyika hivi sasa ni wananchi kushurutishwa kuikubali ccm, na wasipoikubali inatumika shuruti kuwapa wananchi viongozi wasio na ridhaa nao. Mifano ipo dhahiri toka chaguzi za marudio, mpaka hivi majuzi uchaguzi wa serikali za mitaa.

Naona umetaja wabunge na madiwani kuhama kama ishara ya chama kufa. Hii mbinu imetokea nchi za ulaya mashariki kuwa unamuhujumu mpinzani wako, kisha unawachukua watu wake kwa rushwa, vitisho na njia nyingine chafu, halafu unafanya propaganda kuwa mshindani wako ni dhaifu, wakati huo huo ukiendelea kumnyima uwanja sahihi wa kufanya siasa. Haya yote yanatokea tunayaona na tunayatambua vyema. Ni kweli mnaweza kuwapata wajinga kadhaa wakapotea na huu mwenendo na hiyo propaganda mfu, lakini tunaoijua hali hiyo haitupi shida kwani ni jambo la muda tu ukweli uko wazi. Na sisi kwa kulijua hilo tumehakikisha wananchi wengi hawajitokezi kupiga kura ili kuwaonyesha wazi kuwa hamko madarakani kwa ridhaa yao, bali kwa jeuri ya vyombo vya dola. Nikusaidie boss, kizazi hiki sio cha enzi za Nyerere, kizazi hiki ni digitali kinapata taarifa direct na kina ufahamu mkubwa, na wala hakisubiri taarifa za viongozi waliopitwa na wakati kwakuwa wanamadaraka. Kwa maneno marahisi ccm sio chama cha kizazi hiki bali ni cha kizazi kilichopita, ndio maana kinatumia shuruti, ukatili na uhayawani wa wazi kukaa madarakani.
 
Again ninakuambia unaishi kwa fikra zako na hisia na siyo uhalisia. Unapozungumzia siasa kutofanyika sijui unakua na maana gani? Nijuavyo mimi, siasa zinafanyika kama kawaida. Wabunge wapo bungeni wanafanya siasa pamoja na kwenye majimbo yao. Mbowe kila siku anaongea na vyombo vya habari, anafanya siasa. Lissu kabla hajapata lililompata alikua anaongea kutwa kucha kwenye mitandao na vyombo vya habari, anafanya siasa. Kina Zitto wote wanafanya siasa. Sasa wewe sijui ulitaka siasa zipi?

Tunapozungumzia chama kukosa mvuto, ni namna kinavyokimbiwa na viongozi na wanachama wake na siyo namna gani kinafanya siasa. Unapotaka kufanya Siasa ni lazima upate different forums and opportunities za kuwafikia wananchi ili kupenyeza ajenda zako. Sasa huwezi kutegemea tu siasa za majukwaani tu eti useme ile ndo namna pekee ya kufanya siasa na kuwafikia wananchi. Wenzetu nchi zilizoendelea, baada ya uchaguzi huwasikii wakifanya tena siasa za majukwaani. Siasa zote zinahamia Bungeni. kwasabbu wanaamini kila mwanasiasa anakua amepata fursa na sehemu ya kufanya siasa.

Sasa wewe endelea kujidanganya chama chako kimeminywa kufanya siasa wakati huko ndani kuna madudu yanayofanyika nje ya siasa kinachopelekea kukosa mvuto kwa wananchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maprofesa wawili mulioko ndani ya CHADEMA munafahamika vizuri sana kwa ubobezi wenu. Prof. Baregu ni mzuri sana katika sayansi ya siasa, umewafundisha wengi na wamefanikiwa. Prof. Safari yuko vizuri katika sheria. Ni kesi nyingi umeonesha umwamba wake. Wanasheria wengi ni matokeo ya juhudi zako na uwezo wako. Wote munastahili sifa.

Watu hawa wawili nimekuwa nikiwatumainia sana muisaidie CHADEMA. Sifahamu kwanini kipindi hiki mumekuwa kimya kiasi kwamba msaada wenu hauoneakani. Yawezekana msada wenu hauhitajiki. Muelekeo wa CHADEMA kwa sasa ni aibu kwenu ambao mulistahili kuonesha muelekeo unaofaa.

Binafsi nahisi labda mulifanya makosa kuona malengo ya CHADEMA yalikuwa ni yapi. CHADEMA hawako ktk siasa, wako ktk biashara na bahati mbayamaprofesa wawili, kwa pamoja. Biashara ya udanganyifu hamuiwezi.

Uliowataja hapa 95% ya Family Friends wao ni Watu wa CCM tofauti na walipo, Wao hivyo ukisema Wao ni CHADEMA 100% sikuamini kabisa.
 
Again ninakuambia unaishi kwa fikra zako na hisia na siyo uhalisia. Unapozungumzia siasa kutofanyika sijui unakua na maana gani? Nijuavyo mimi, siasa zinafanyika kama kawaida. Wabunge wapo bungeni wanafanya siasa pamoja na kwenye majimbo yao. Mbowe kila siku anaongea na vyombo vya habari, anafanya siasa. Lissu kabla hajapata lililompata alikua anaongea kutwa kucha kwenye mitandao na vyombo vya habari, anafanya siasa. Kina Zitto wote wanafanya siasa. Sasa wewe sijui ulitaka siasa zipi?

Tunapozungumzia chama kukosa mvuto, ni namna kinavyokimbiwa na viongozi na wanachama wake na siyo namna gani kinafanya siasa. Unapotaka kufanya Siasa ni lazima upate different forums and opportunities za kuwafikia wananchi ili kupenyeza ajenda zako. Sasa huwezi kutegemea tu siasa za majukwaani tu eti useme ile ndo namna pekee ya kufanya siasa na kuwafikia wananchi. Wenzetu nchi zilizoendelea, baada ya uchaguzi huwasikii wakifanya tena siasa za majukwaani. Siasa zote zinahamia Bungeni. kwasabbu wanaamini kila mwanasiasa anakua amepata fursa na sehemu ya kufanya siasa.

Sasa wewe endelea kujidanganya chama chako kimeminywa kufanya siasa wakati huko ndani kuna madudu yanayofanyika nje ya siasa kinachopelekea kukosa mvuto kwa wananchi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hilo bungeni unalionea wapi, huenda ww ni mbunge hivyo hizo siasa unaziona. Je bunge unalosema ndio hili hili linalomtukuza rais na kupitisha kila takwa la rais kwa shuruti?

Huyo Mbowe anaoongea na vyombo vya habari vya uchochoroni na kila mara anafanyiwa mizengwe, au unadhani hatuoni? Lissu hali kadhalika alikuwa anaongelea uchochoroni, na kama ni huku mitandaoni mbona tunaona wapinzani wakiwa active kuliko sehemu nyingine? Hizo nchi za wenzetu una kipi cha kujilinganisha nao? Wao chaguzi zao ni huru, je nchi zao pia rais ndio anachagua tume ya uchaguzi? Je kiongozi wa chama kilicho madarakani ndio anapanga vyama vingine vifanye vipi siasa, huku akikipa chama chake upendeleo wa wazi? Huku kwetu mazingira yetu siasa za majukwaani ni moja ya kuwafikia wananchi, kwani huko Marekani unamuona Trump akigawa hela kwenye mikutano, na kila ziara yake kujazwa na bendera na mavazi ya chama chake? Usitolee mifano isiyokubeba.

Narudia tena, kwenye chaguzi zetu tunaona wazi zikinajisiwa, je katika mazingira watu wanatoka na mabox ya kura kwenda kujaza kura za ccm, tena kwa uratibu wa jeshi la polisi utasemaje cdm inakosa mvuto kwa wananchi? Unadhani hizi siasa alizokuja nazi rais wa sasa wa kushurutisha wananchi kuikubali ccm bila ridhaa yao ndio itakipa ccm mvuto, na kuipotezea mvuto cdm?
 
Hizo fikra kwamba wanaohama CDM ni waganga njaa ndio tatizo lenyewe ndugu tindo

Sasa kama unahama chama kisha unaomba kufagia ofisi ya ccm kama sio mganga njaa ni nini? Hao wanawake wanaosema wamenyanyaswa kingono,nani anyanyase hayo maajuza aache mabinti wadogo? Hayo mazee hata yakikunywea bia yako unapata hasira. Mapango waliyonayo hata ukiingiza mkono unapita ndio yanajidai yamenyanyaswa kingono, kwanza kwa sura gani walizo nazo?
 
Hilo bungeni unalionea wapi, huenda ww ni mbunge hivyo hizo siasa unaziona. Je bunge unalosema ndio hili hili linalomtukuza rais na kupitisha kila takwa la rais kwa shuruti?

Huyo Mbowe anaoongea na vyombo vya habari vya uchochoroni na kila mara anafanyiwa mizengwe, au unadhani hatuoni? Lissu hali kadhalika alikuwa anaongelea uchochoroni, na kama ni huku mitandaoni mbona tunaona wapinzani wakiwa active kuliko sehemu nyingine? Hizo nchi za wenzetu una kipi cha kujilinganisha nao? Wao chaguzi zao ni huru, je nchi zao pia rais ndio anachagua tume ya uchaguzi? Je kiongozi wa chama kilicho madarakani ndio anapanga vyama vingine vifanye vipi siasa, huku akikipa chama chake upendeleo wa wazi? Huku kwetu mazingira yetu siasa za majukwaani ni moja ya kuwafikia wananchi, kwani huko Marekani unamuona Trump akigawa hela kwenye mikutano, na kila ziara yake kujazwa na bendera na mavazi ya chama chake? Usitolee mifano isiyokubeba.

Narudia tena, kwenye chaguzi zetu tunaona wazi zikinajisiwa, je katika mazingira watu wanatoka na mabox ya kura kwenda kujaza kura za ccm, tena kwa uratibu wa jeshi la polisi utasemaje cdm inakosa mvuto kwa wananchi? Unadhani hizi siasa alizokuja nazi rais wa sasa wa kushurutisha wananchi kuikubali ccm bila ridhaa yao ndio itakipa ccm mvuto, na kuipotezea mvuto cdm?
We jamaa acha kujitoa akili kutokana na ushabiki wa vyama. Hivi kwa wingi wa wabunge wa CCM ulitegemea Bunge lisipitishe matakwa ya CCM na Serikali yake ije ipitishe matakwa ya Chadema? Kila chama lazima kisimamie ilani na maslahi yake, Sasa hapo shuruti inatoka wapi? Hata CDM ingekua na wabunge wengi ingelinda maslahi yake.

Unasema mbowe na Lissu wanaongelea vichochoroni. Hivi kichochoro kwako wewe ni kipi? Ulitaka wakaongelee wapi ambapo sipo kichochoroni? Cha kujiuliza hata kama wanaongelea huko kichochoroni ujumbe wao unafika kwa Jamii au haufiki? Au umeshawahi kuzuiliwa usifike?

Hii hoja ya mabox ya kura kuibiwa ni hoja muflisi na imepitwa na wakati. Toka upinzani unaanzishwa hii ndo ilikua hoja yao kwenye kila chaguzi wanaposhindwa. Wewe subiria wakati utakupa somo zuri sana kuhusu huu upinzani uchwara unaopigania kwenye mitandao. Kina mbowe wanapiga hela wewe unakesha humu kuwapaka mafuta.

Alamsiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Prof. Safari ni msaka tonge tu, niliwashangaa sana CHADEMA kuwakumbatia hawa wasaka tonge na watumishi wa CCM waliotoka CUF miaka ya nyuma. Huko CUF waliondoka baada ya kushtukiwa.
 
Chadema haifi. Msimu huu wa uchaguzi tunatazamia kuona watu wengi wakihama na hasa wale walikuwa viongozi na wakiangalia hali wanaona hawatapita kwenye mchujo ndani ya Chama. Tunatazamia kuwaona kina Lijualikali wengi. Hasa wakati ule wa kikao cha mwisho cha mchujo wengi watatangaza kuhama. Tumejiandaa kisaikolojia. Chadema ni taasisi imara na hakifi. Safari hii ushindi utakuwa mkubwa sana kuliko uchaguzi uliopita. Kama tu uchaguzi ungekuwa huru chini ya tume huru ya uchaguzi, Chadema kina nafasi na uwezo wa kushinda ngazi ya uraisi na wabunge zaidi ya nusu. Hamahama hiyo ni kawaida na hatutishiki wala hatudanganyiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kujiandaa kisaikolojia ni muhimu sana,ni kweli chama hakitakufa ila kitakuwa kama TLP
 
Mtasubiri sana kwa Chadema kufa. Chadema imo mioyoni mwa Watanzania na huwezi kuua kitu kinachopendwa sana na mamilioni ya watu.
 
Bila korona hali ya siasa ingeshakuwa tete sana. Taarifa kuwa korona inapungua tayari mzozozo unaanza! Siasa bwana!

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom