Prof. Baregu na Prof. Safari mpo wapi katika kuanguka huku kwa CHADEMA?

Prof. Baregu na Prof. Safari mpo wapi katika kuanguka huku kwa CHADEMA?

Mkuu unaishi utopia. Unaishi kwenye fikra na hisia na siyo uhalisia. Hivi ulitaka CDM ifeje ili ujue imekufa. Ndani ya kipindi cha miaka 2 Chama kimekimbiwa na zaidi ya wabunge 15 Madiwani ndo usiseme. Kimepoteza ngome zake kuu zote za arusha na moshi. Hiyo Tume ya Uchaguzi hata mbowe awe Mwenyekiti hamtoboi. Kwasababu huko nje chama kimepoteza mvuto mmebakia mashabiki wa kwenye mitandao.

Lakini nikubaliane nawwe kwakuwa umejipambanua kama mshabiki wa CDM. Unapokua mshabiki wa jambo fulani mara chache sana kuona udhaifu wa kitu unachoshabikia na imani yako inakua ni kubwa sana katika jambo hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanini hamtaki tume huru kama unahisi chadema imepoteza mvuto? Hamtaki chama kifanye siasa, siasa mnafanya nyie lakini bado mnaogopa kuweka tume huru

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Again ninakuambia unaishi kwa fikra zako na hisia na siyo uhalisia. Unapozungumzia siasa kutofanyika sijui unakua na maana gani? Nijuavyo mimi, siasa zinafanyika kama kawaida. Wabunge wapo bungeni wanafanya siasa pamoja na kwenye majimbo yao. Mbowe kila siku anaongea na vyombo vya habari, anafanya siasa. Lissu kabla hajapata lililompata alikua anaongea kutwa kucha kwenye mitandao na vyombo vya habari, anafanya siasa. Kina Zitto wote wanafanya siasa. Sasa wewe sijui ulitaka siasa zipi?

Tunapozungumzia chama kukosa mvuto, ni namna kinavyokimbiwa na viongozi na wanachama wake na siyo namna gani kinafanya siasa. Unapotaka kufanya Siasa ni lazima upate different forums and opportunities za kuwafikia wananchi ili kupenyeza ajenda zako. Sasa huwezi kutegemea tu siasa za majukwaani tu eti useme ile ndo namna pekee ya kufanya siasa na kuwafikia wananchi. Wenzetu nchi zilizoendelea, baada ya uchaguzi huwasikii wakifanya tena siasa za majukwaani. Siasa zote zinahamia Bungeni. kwasabbu wanaamini kila mwanasiasa anakua amepata fursa na sehemu ya kufanya siasa.

Sasa wewe endelea kujidanganya chama chako kimeminywa kufanya siasa wakati huko ndani kuna madudu yanayofanyika nje ya siasa kinachopelekea kukosa mvuto kwa wananchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
"wenzetu nchi zilizoendelea" je hii ni nchi iliyoendelea? Pili jiwe aliposema siasa mpaka 2020 Ulielewa nini? Unaweza kuwa na kichwa lakini kikabaki cha kufugia nywele tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We jamaa acha kujitoa akili kutokana na ushabiki wa vyama. Hivi kwa wingi wa wabunge wa CCM ulitegemea Bunge lisipitishe matakwa ya CCM na Serikali yake ije ipitishe matakwa ya Chadema? Kila chama lazima kisimamie ilani na maslahi yake, Sasa hapo shuruti inatoka wapi? Hata CDM ingekua na wabunge wengi ingelinda maslahi yake.

Unasema mbowe na Lissu wanaongelea vichochoroni. Hivi kichochoro kwako wewe ni kipi? Ulitaka wakaongelee wapi ambapo sipo kichochoroni? Cha kujiuliza hata kama wanaongelea huko kichochoroni ujumbe wao unafika kwa Jamii au haufiki? Au umeshawahi kuzuiliwa usifike?

Hii hoja ya mabox ya kura kuibiwa ni hoja muflisi na imepitwa na wakati. Toka upinzani unaanzishwa hii ndo ilikua hoja yao kwenye kila chaguzi wanaposhindwa. Wewe subiria wakati utakupa somo zuri sana kuhusu huu upinzani uchwara unaopigania kwenye mitandao. Kina mbowe wanapiga hela wewe unakesha humu kuwapaka mafuta.

Alamsiki.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kuwa wengi haimaanishi unachopitisha lazima kiwe sahihi. Isitoshe wingi wa ccm huko bungeni unatokana na mifumo mibovu ya kupatikana kwao. Kama wingi huo unatokana na mfumo mbovu, hila na dhuluma ni wazi hata watakachokuwa wanapitisha kitakuwa cha shuruti.

Nasema hivi, humu ni vichochoroni na ujumbe unafika kwa umma kwa uchache sana. Je hujui kuwa kwa sasa vyombo vya habari rasmi vimeingiwa na woga baada ya kutishiwa na kuchukuliwa hatua kadha wa kadha ili kukomolewa?

Hoja ya mabox ya kura kuporwa na kwenda kujazwa kura za ccm ni kweli ni ya muda mrefu, je kwakuwa ni ya muda mrefu tuache kuisema wakati tunaiona kwa macho kisa ni ya muda mrefu? Kwahiyo unataka tuikubali kwa kuwa ni ya muda mrefu! Hebu nipe tofauti ya huu upinzani uchwara na chama tawala, maana bado nchi yetu ni masikini chini ya hicho chama tawala unachokiona ni imara. Ni kweli kina Mbowe wanapiga hela kisha mimi naishia kuwapaka mafuta, kwani ww hao unaowatetea huwa unatembea nao kwenye hayo maVX? Au ww unafungu lako rasmi la kuwatetea, ili na mimi nije niwasifie nipate fungu kama ww?
 
Maprofesa wawili mulioko ndani ya CHADEMA munafahamika vizuri sana kwa ubobezi wenu. Prof. Baregu ni mzuri sana katika sayansi ya siasa, umewafundisha wengi na wamefanikiwa. Prof. Safari yuko vizuri katika sheria. Ni kesi nyingi umeonesha umwamba wake. Wanasheria wengi ni matokeo ya juhudi zako na uwezo wako. Wote munastahili sifa.

Watu hawa wawili nimekuwa nikiwatumainia sana muisaidie CHADEMA. Sifahamu kwanini kipindi hiki mumekuwa kimya kiasi kwamba msaada wenu hauoneakani. Yawezekana msada wenu hauhitajiki. Muelekeo wa CHADEMA kwa sasa ni aibu kwenu ambao mulistahili kuonesha muelekeo unaofaa.

Binafsi nahisi labda mulifanya makosa kuona malengo ya CHADEMA yalikuwa ni yapi. CHADEMA hawako ktk siasa, wako ktk biashara na bahati mbayamaprofesa wawili, kwa pamoja. Biashara ya udanganyifu hamuiwezi.
Sheikh hata ukiona madudu yanafanyika utakaa Kimia
 
Hao walishajiondoa kwenye ujumbe kamati kuu na kujivua vyeo vyote ndani ya chama

Sent using Fly in any Weather.
Hakika sikujua kama CDM ilishapoteza vichwa hivi. Sijui sababu ya Mbowe kuendelea kujimwambafy ni nini? Naweza ,usema ni mmoja wa watu wa hovyo kabisa ktk uongozi. Mtindo huu ndo unadhalilisha wanachama na nchi kwa ujumla maana CCM haitakuja kuwa na wapinzani wanaojifahamu. Wananchi tunachokiona ni uhuni na uharibifu wa pesa za serikali.

Ruzuku kwa vyama hivi iondolewe. Huwezi kuwapa ruzuku kwa miaka zaidi ya 20 halafu hawakui na hata wanapokufa hakuna kinachobaki. DP, UDP, TLP, CUF, CHADEMA, nk. wote walishakula ruzuku na leo hii hakuna cha kuoneana!
 
Kuwa wengi haimaanishi unachopitisha lazima kiwe sahihi. Isitoshe wingi wa ccm huko bungeni unatokana na mifumo mibovu ya kupatikana kwao. Kama wingi huo unatokana na mfumo mbovu, hila na dhuluma ni wazi hata watakachokuwa wanapitisha kitakuwa cha shuruti.

Nasema hivi, humu ni vichochoroni na ujumbe unafika kwa umma kwa uchache sana. Je hujui kuwa kwa sasa vyombo vya habari rasmi vimeingiwa na woga baada ya kutishiwa na kuchukuliwa hatua kadha wa kadha ili kukomolewa?

Hoja ya mabox ya kura kuporwa na kwenda kujazwa kura za ccm ni kweli ni ya muda mrefu, je kwakuwa ni ya muda mrefu tuache kuisema wakati tunaiona kwa macho kisa ni ya muda mrefu? Kwahiyo unataka tuikubali kwa kuwa ni ya muda mrefu! Hebu nipe tofauti ya huu upinzani uchwara na chama tawala, maana bado nchi yetu ni masikini chini ya hicho chama tawala unachokiona ni imara. Ni kweli kina Mbowe wanapiga hela kisha mimi naishia kuwapaka mafuta, kwani ww hao unaowatetea huwa unatembea nao kwenye hayo maVX? Au ww unafungu lako rasmi la kuwatetea, ili na mimi nije niwasifie nipate fungu kama ww?
This is another rubbish!
 
Hujui kama safari alishajivua nafasi zote kwenye chama na sasa yupo kama mwachama wa kawaida?

Na alishauli kuwa CHADEMA ichukue hatua kujilekebisha pale ilipokosea tena kabla hata ya uchaguzi wa mwenyekiti wa chama.

Wa kuulizwa sasa ni prof Baregu.
Mbowe akitangaza kwamba Ile Mikutano ambayo iliairishwa kwa Sababu ya Korona, sasa Kwakuwa Korona Imepungua, Mikutano inaanza upya UTAONA KORONA NAYO ITAANZA UPYA KWA MUJIBU WA CCM
 
Mbowe akitangaza kwamba Ile Mikutano ambayo iliairishwa kwa Sababu ya Korona, sasa Kwakuwa Korona Imepungua, Mikutano inaanza upya UTAONA KORONA NAYO ITAANZA UPYA KWA MUJIBU WA CCM

Mikutano gani sasa, atahutubia watoto au?
Kumbuka kwao tu walimshusha jukwaani mwezi wa pili.
 
"wenzetu nchi zilizoendelea" je hii ni nchi iliyoendelea? Pili jiwe aliposema siasa mpaka 2020 Ulielewa nini? Unaweza kuwa na kichwa lakini kikabaki cha kufugia nywele tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahiyo kwasbbu hii nchi siyo miongoni kwa nchi zilizoendelea, basi hatupaswi kuiga mazuri ya nchi zilizoendelea. Hii Demokrasia yenyewe tunayoipractise hapa imetoka huko huko kwenye nchi zilizoendelea.

Wewe kutokana na uelewa wako mdogo ndo ulishindwa kuielewa kauli ya Mhe.Rais ya siasa mpaka 2020. Siasa uliyoengelewa ni zile za majukwaani ambazo huwezi kuzitofautisha na kampeni. Yale maoperesheni ya mbowe ya kuwapiga hela Chadema. Infact, Siasa zinaendelea kama kawaida wabunge hajakatazwa kufanya siasa kwenye majimbo yao. Vile vile, bungeni siasa zinaendelea watu wanapingana kwa hoja n.k vyombo vya habari vinaendelea kuripoti matukio ya kisiasa kila yanapojiri. Halikadhalika, mitandao ya kijamii ni forums zinazotumiwa sana na wanasiasa kupenyeza ajenda zao.

Sasa sijui Nyinyi mlitaka siasa za aina gani? Mlitaka mumuone Mwamba anazunguka na helkopta majimboni halafu baadae anapeleka deni kwenye chama alipwe hela ya kukodi helkopta.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom