Prof. Baregu na Prof. Safari mpo wapi katika kuanguka huku kwa CHADEMA?

Kwanini hamtaki tume huru kama unahisi chadema imepoteza mvuto? Hamtaki chama kifanye siasa, siasa mnafanya nyie lakini bado mnaogopa kuweka tume huru

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"wenzetu nchi zilizoendelea" je hii ni nchi iliyoendelea? Pili jiwe aliposema siasa mpaka 2020 Ulielewa nini? Unaweza kuwa na kichwa lakini kikabaki cha kufugia nywele tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kuwa wengi haimaanishi unachopitisha lazima kiwe sahihi. Isitoshe wingi wa ccm huko bungeni unatokana na mifumo mibovu ya kupatikana kwao. Kama wingi huo unatokana na mfumo mbovu, hila na dhuluma ni wazi hata watakachokuwa wanapitisha kitakuwa cha shuruti.

Nasema hivi, humu ni vichochoroni na ujumbe unafika kwa umma kwa uchache sana. Je hujui kuwa kwa sasa vyombo vya habari rasmi vimeingiwa na woga baada ya kutishiwa na kuchukuliwa hatua kadha wa kadha ili kukomolewa?

Hoja ya mabox ya kura kuporwa na kwenda kujazwa kura za ccm ni kweli ni ya muda mrefu, je kwakuwa ni ya muda mrefu tuache kuisema wakati tunaiona kwa macho kisa ni ya muda mrefu? Kwahiyo unataka tuikubali kwa kuwa ni ya muda mrefu! Hebu nipe tofauti ya huu upinzani uchwara na chama tawala, maana bado nchi yetu ni masikini chini ya hicho chama tawala unachokiona ni imara. Ni kweli kina Mbowe wanapiga hela kisha mimi naishia kuwapaka mafuta, kwani ww hao unaowatetea huwa unatembea nao kwenye hayo maVX? Au ww unafungu lako rasmi la kuwatetea, ili na mimi nije niwasifie nipate fungu kama ww?
 
Sheikh hata ukiona madudu yanafanyika utakaa Kimia
 
Hao walishajiondoa kwenye ujumbe kamati kuu na kujivua vyeo vyote ndani ya chama

Sent using Fly in any Weather.
Hakika sikujua kama CDM ilishapoteza vichwa hivi. Sijui sababu ya Mbowe kuendelea kujimwambafy ni nini? Naweza ,usema ni mmoja wa watu wa hovyo kabisa ktk uongozi. Mtindo huu ndo unadhalilisha wanachama na nchi kwa ujumla maana CCM haitakuja kuwa na wapinzani wanaojifahamu. Wananchi tunachokiona ni uhuni na uharibifu wa pesa za serikali.

Ruzuku kwa vyama hivi iondolewe. Huwezi kuwapa ruzuku kwa miaka zaidi ya 20 halafu hawakui na hata wanapokufa hakuna kinachobaki. DP, UDP, TLP, CUF, CHADEMA, nk. wote walishakula ruzuku na leo hii hakuna cha kuoneana!
 
This is another rubbish!
 
Mbowe akitangaza kwamba Ile Mikutano ambayo iliairishwa kwa Sababu ya Korona, sasa Kwakuwa Korona Imepungua, Mikutano inaanza upya UTAONA KORONA NAYO ITAANZA UPYA KWA MUJIBU WA CCM
 
Mbowe akitangaza kwamba Ile Mikutano ambayo iliairishwa kwa Sababu ya Korona, sasa Kwakuwa Korona Imepungua, Mikutano inaanza upya UTAONA KORONA NAYO ITAANZA UPYA KWA MUJIBU WA CCM

Mikutano gani sasa, atahutubia watoto au?
Kumbuka kwao tu walimshusha jukwaani mwezi wa pili.
 
"wenzetu nchi zilizoendelea" je hii ni nchi iliyoendelea? Pili jiwe aliposema siasa mpaka 2020 Ulielewa nini? Unaweza kuwa na kichwa lakini kikabaki cha kufugia nywele tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahiyo kwasbbu hii nchi siyo miongoni kwa nchi zilizoendelea, basi hatupaswi kuiga mazuri ya nchi zilizoendelea. Hii Demokrasia yenyewe tunayoipractise hapa imetoka huko huko kwenye nchi zilizoendelea.

Wewe kutokana na uelewa wako mdogo ndo ulishindwa kuielewa kauli ya Mhe.Rais ya siasa mpaka 2020. Siasa uliyoengelewa ni zile za majukwaani ambazo huwezi kuzitofautisha na kampeni. Yale maoperesheni ya mbowe ya kuwapiga hela Chadema. Infact, Siasa zinaendelea kama kawaida wabunge hajakatazwa kufanya siasa kwenye majimbo yao. Vile vile, bungeni siasa zinaendelea watu wanapingana kwa hoja n.k vyombo vya habari vinaendelea kuripoti matukio ya kisiasa kila yanapojiri. Halikadhalika, mitandao ya kijamii ni forums zinazotumiwa sana na wanasiasa kupenyeza ajenda zao.

Sasa sijui Nyinyi mlitaka siasa za aina gani? Mlitaka mumuone Mwamba anazunguka na helkopta majimboni halafu baadae anapeleka deni kwenye chama alipwe hela ya kukodi helkopta.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…