PreGE2025 Prof. Eginald PAN Mihanjo: CCM ijiandae kuwa chama cha upinzani

PreGE2025 Prof. Eginald PAN Mihanjo: CCM ijiandae kuwa chama cha upinzani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Hamjazoea kusikia wasomi kama huyu bobezi wa historia, stratejia akiongelea udhaifu wa CCM na dhana potofu kuwa wapo wengi.

Tunahitaji wazee kama hawa tuwasikilize wajitokeze wahojiwe walio tofauti na wapiga stori Prof. Palamagamba Kabudi
Hana stratejia yoyote,zaidi ya kufanya anayoelekezwa,hakuwa na mamlaka ya kufanya statejia katika chama tawala wala nchi,angalia profile yake na ulizia kwa waliokalia nyadhifa hizo,strategia kidogo katika utekelezaji wa majukumu aliyopewa katika eneo lake la utendaji ambalo ni doooogooooo, sio kubwa kama CCM katika sura ya taifa au nchi kama nchi
 
Mikakati na ukweli juu ya CCM ni chama dola siyo chama cha siasa imedhihirika
 
Ye mwenyewe ndio dhaifu, amesoma na kuendelezwa chini ya ccm, halafu leo mbwa huyu anaiona ccm kituko, mbaaaf kabisa huyu!
Ila hukubali kuna siku ccm itaondoka kama itakavyoondoka dunia ukiwemo wewe?
 
27 Aprili 2025
Vikosi vya paramilitary /police kusambazwa katika mitaa ni kutishia umma ?
1745830022789.jpeg

SACP Jumanne Muliro asema ni ulinzi wa kawaida, hakuna kitu cha ajabu. Tunatekeleza majukumu yetu ya usalama, SACP Muliro mkuu wa Kanda Maalum ya Kipolisi jijini Dar es Salaam, Tanzania asisitiza.

1745830297653.jpeg
 
25 Aprili 2025


View: https://m.youtube.com/watch?v=wbk2XLS77j8
Ushindi haupatikani kwa kutegemea 'chawa' wala wingi wa kadi. Watu wana kadi na mapenzi kwa vyama hata vitatu. CCM iwe makini wanatakiwa wasiwe na mazoea.

CHADEMA kimekaa muda mrefu kama chama cha siasa, sasa kimekuja kivingine kama MOVEMENT / VUGUVUGU 2025

anasema Prof. Mihanjo na anadadavua kwa kina :
  • 2015 CCM ilikuwa ipotee
  • Kanda ya Ziwa ilibeba CCM chini ya JPM
  • Rais wa sasa aliyeingia kwa ajali, awe makini sana
  • Rais aliyepo atapitia wakati mgumu March 2025 - June 2025
  • No Reforms No Election ni Hoja kubwa sana
  • Wapinzani wasiiache No Reforms No Election
  • Wananchi wamekosa matumaini maisha ni magumu
  • CCM kuwa madarakani miaka 60 ni fursa lakini ni changamoto kubwa kwa CCM
  • CCM inabebwa na structures, miundo mifumo onayoikibeba
  • Vijana ambao ndiyo wengi wanaona kuwa matatizo yote ya kukosa ajira, masoko na maisha magumu ni sababu ya CCM
  • Ikiwa vijana wengi watajitokeza kupiga kura 2025, itakuwa balaa kubwa kwa CCM
  • Mkutano Mkuu wa CCM kuvunja katiba yake kuteua mgombea uchaguzi na mgombea mwenza ni ulevi wa madaraka
  • Kuna vipindi katiba inakanyagwa, wakati wa Mkapa tunajua majina 5 yaiingia Halmashauri Kuu kuchaguliwa
  • Jakaya Kikwete asingepita ikabidi Mkapa acheze mchezo na alisaidiwa na 'vyombo' majina matatu yakapitishwa Salim Ahmed Sal8m , Jakaya Kikwetw , Prof. Mwandosya
  • Samia Hassan asingepita kuwa mgombea wa CCM January, ilibidi 'vyombo' wafanye namna kuvunja katiba
  • Kuvunjwa katiba ina athari mtambuka inagusa Kidiplomasia, kiulinzi na Kisiasa
  • Ndiyo maana No Reforms No Election imepata nguvu
  • Tundu Lissu anaongea lugha onayoeleweka na vijana, na anatakiwa kupanua wigo akusanye makundi yote
  • Tundu Lissu na viongozi wenzake CHADEMA waongeze hamasa vijana wajitoke kukiunga mkono CHADEMA na wajitokeze kupiga kura
  • CHADEMA wazungumzie matatizo ya Wakulima, Wavuvi, wafugaji wanafunzi wa vyuo ili kugusa mahitaji ya kila kundi
  • Tunaangalia stratejia za CCM na Wapinzani
  • Marafiki zangu Lowassa, Bernard Membe, mwalimu wangu Kingunga Ngombale Mwiru walijitoa CCM walinipigia simu kabla ya kuhama na kuekezea sababu zao ..
  • Tumeandika katika sekretarieti ..

Prof. Eginald P.A.N. Mihanjo. PhD, MA in History, BA (Hon.) Educ. (UDSM) amewahi kuwa Kaimu Makamu Mkuu Wa Chuo na mhadhiri mwandamizi kama mkurugenzi wa mafunzo wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa NDC, chuo cha Diplomasia cha Tanzania na Msumbiji Foreign Relation Kurasini.. pia ni mtaalamu wa Usuluhishi wa Migogoro kimataifa na kikanda ..

Historia inatabia ya kujirudia. Hata upige mateke vipi ni kama ya A Dyinh Horse
 
Sasa Lissu huo wigo atapanulia wapi wakati yu ndani na hukumu yake ndio ile inayosemwasemwa?
Sasa Lissu huo wigo atapanulia wapi wakati yu ndani na hukumu yake ndio ile inayosemwasemwa?

Hata Nelson Mandela alipanua wigo wa Wafuasi wake na kukubalika kwake wakati akiwa yupo ndani gerezani katika gereza la Kisiwa Cha Roben kule Mjini Cape Town. Alipotoka Gerezani moja kwa moja aliingia Ikulu mjini Pretoria.

Kumbuka: Ukweli mchungu daima huwa una kawaida ya kuishi milele hata kama utakataliwa na Watu wote kabisa katika Jamii!
 
Prof. Eginald P.A.N. Mihanjo. PhD, MA in History, BA (Hon.) Educ. (UDSM) amewahi kuwa mkurugenzi wa mafunzo wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa NDC,
Fahamu chuo cha ulinzi wa taifa NDC kwa undani :

TOKA MAKTABA:

Mkuu wa Chuo Cha Ulinzi wa Taifa-NDC Meja Jenerali Ibrahim Mhona Aeleza Mafanikio..​



View: https://m.youtube.com/watch?v=YGH4z19yylk
TOKA MAKTABA :

26 Julai 2015
Rais Jakaya Kikwete amekitaka chuo cha taifa cha ulinzi Tanzania-NDC- kuwekeza katika tafiti za hali ya juu zitakazosaidia kutatua matatizo ya nchi za Afrika husasani katika changamoto zinazotokana na maswala ya kisiasa, usalama, uchumi na ulinzi....


View: https://m.youtube.com/watch?v=57BOq_N-ZHc
 
Prof. Eginald P.A.N. Mihanjo. PhD, MA in History, BA (Hon.) Educ. (UDSM):- Rais wa ajali aliyepo atapitia wakati mgumu March 2025 - June 2025

28 Aprili 2025
Mahakama ya Hakimu
Mkazi Mkuu
Kisutu, DSM

Kesi ya Tundu Lissu yahairishwa hadi tarehe 6 May 2025 kutoa hukumu ya mapingamizi yaliyowasilishwa na pande mbili za Jamhuri na ule wa utetezi upande wa Tundu Lissu


View: https://m.youtube.com/watch?v=VnAzCM16aQo
 
25 April 2025

Prof Mihanjo: Lissu ni tishio kwa CCM Vijana wakihamasika CCM wataondoka​


View: https://m.youtube.com/watch?v=5E0XtcICUMM

CCM waliposema wanataka shule kila kata, nikawaambia wakati huo mtapata kura lakini miaka 10 baadaye Elimu kwa wote madhara yake ni kuwa hupelekea watu kutaka mabadiliko, tunaiona hiyo sasa baada ya miaka kumi kupita, 2025 vijana wengi hawaielewi CCM wanataka mabadiliko .. Prof. Eginald P.A.N. Mihanjo

Huyu Mihanjo popote alipo anywe bia bili kwangu
 
Back
Top Bottom