Hi guys kutoka Helsinki
MSIBA WA KUSHUTUA SANA
Mimi kama member wa UDASA-nimezipata habari za kifo cha professor-kupitia UDASA mails kwa mshituko mkubwa sana. Professor Othman alinifundisha pia alikuwa ni mshauri wangu katika mambo ya academic hasa hasa masomo yangu ya PhD. Alikuwa ni mtu wa watu, hana majungu, hana fitina, hana majigambo hata kama alikuwa ni professor wa kimataifa, he was a very humble person, he was the wisest person, I have ever met, alikuwa hakuulizi kabila lako, wala dini yako hata umri wako, alipenda kuheshimu watu wote wakubwa na wadogo. Nilipenda sana kumtembelea ofisini kwake kuongea kuhusu mambo mbali mbali ya Africa na dunia, hakuwa mchoyo wala mtu wa kujidai-PENGO HALIZIBIKI MAANA NI VIGUMU KUPATA MTU MWENYE C.V kama hii-maana hata chuo kikuu cha DSM wanalijua hili- wakubwa wanataka kukaa juu na wadogo wakaa chini lakini professor Haroub alikuwa tofauti kabisa-mungu muweke mahali pema peponi
Rest in peace!
Rest in Peace!
Frateline Kashaga
PhD student
Department of social policy
University of Helsinki-Finland