Gamba La Nyoka, tuseme unakutana na wakulima katika kijiji kimoja Tanzania, ambao soko huria limewacha hoi bin taaban, suala la soko huria kuwacha 70% ya watanzania HOI sidhani kama lina mjadala; Sasa, katika mjadala wako na wakulima/maskini hawa wa watu, juu ya hali zao ki-uchumi, ki-jamii n.k, mmoja wao anatoa hoja kwamba Azimio La Arusha (1967 – 1992) lilikuwa ni la Wananchi, na Azimio la Zanzibar (1992 – 2011) ni la Watawala, utamjibu nini? Jibu hilo nalo litatusaidia sana to shed more light katika huu mjadala wetu on Azimio la Arusha.
Hilo ni swali ambalo haujanipatia majibu bado. Naomba ukipata muda, unirudie na hilo.
Vinginevyo, upo sahihi kwamba mjadala unaoegemea itikadi za vyama hauwezi kuwa na tija. Ninachojaribu jadili lakini ni suala ambalo kwa mtazamo wangu linagusa taifa kwa ujumla, hata kama mwanzilishi wake alikuwa TANU. Nitajitahidi kuepuka mijadala ya kiitikadi, na badala yake kuelekeza nguvu zaidi kwenye masuala yenye maslahi ya taifa. Niwie radhi napoenda kinyume.
Naomba nianze kwa kujibu hoja ifuatayo, halafu nitakurudia kwenye hoja zako nyingine baadae kidogo, bila ya kusahau suala la Equality and the Declaration, kama nilivyoahidi.
Umeniuliza kwamba ningemjibu vipi Mwalimu kuhusiana na maadili ya viongozi?- infact ningemjibu wazi kwamba, pamoja na kwamba ni kiongozi lakini nina haki ya kutumia ujuzi wangu mwingine kwa malipo halali ya kazi yangu, kisha ningemweleza wazi kwamba sioni mantiki ya mimi kutokuweza kupangisha nyumba yangu niliyoijenga kwa jasho langu mwenyewe, kwani kwa kufanya hivyo sijaiibia serikali!.
ndo maana nimeweka vipengele viwili vilivyofanyiwa mabadirisho na Azimio la Zanzibar najinukuu hapa chini, kisha naomba maoni yako kuhusiana na vipengele hivyo...
Hoja yako kwamba mwaka 1967, kama kiongozi wa taifa huru lenye miaka 6 tu, una haki ya kutumia ujuzi wako mwingine mahali popote, popote wapi? katika uchumi upi Gamba La Nyoka? Soko lipi wakati 95% ya nchi ni vijiji/wakulima? au una maanisha bwana shamba binafsi? Unazijua takwimu za uchumi za aliotuachia Mkoloni zilikuwaje Gamba La Nyoka? Social conditions pia?
Sina uhakika kama nitakuw asahihi kutamka kwamba, umejisahau kabisa kwamba taifa lilikuwa ndio kwanza jipya kwa kila hali, hapakuwa na incentives zozote za maana in the economy (tofauti na Kenya kwa mfano), to exploit other opportunities in any meaningful way – mfano, aggregate demand/purchasing power, however we should put it, ni kama haikuwepo;
In 1967, population ilikuwa around 9 million, with 95% (about 8.5 million Tanganyikans) vijijini/wakulima; and only 5% (about 50,000) of the population as urbanites; Mbali ya hilo, kulikuwa na uhaba wa wataalam – engineers, walimu, madaktari, almost an absence of a tax base, thereby mapato ya nchi yakiendelea kutegemea kumkamua wakulima (95%) of the population, kwa mtindo ule ule wa producing what we don't consume (e.g. pamba, mkonge..) and consume what we don't produce (e.g. skuna, kaniki…
😉, a system inherited from mkoloni, only 6 years before, huku watanganyika 8.5 million wakiwa bado na kumbukumbu za ahadi za Mwalimu juu ya nini atawafanyia iwapo watapambana kumwondoa mkoloni - ajira, huduma za kijamii…; hata kama Mwalimu alilemewa na huduma hizi, na mashirika ya umma yasio na ufanisi – there is one thing that he did –
Hakuvunja ahadi yake kwa watanganyika ya huduma bure za afya na ajira kwa wengi, suala ambalo hata chama makini kama CHADEMA kimeliona in 2010;
Gamba La Nyoka, naomba usisahau hii takwimu - katika watanganyika takriban milioni tisa (9) in total (1967), watanganyika kama 8,500,000 wapo vijijini/wakulima, only 50,000 ndio wapo mijini, baadhi yao ndio hao viongozi wa TANU ambao wamebahatika to occupy ajira zilizoachwa na mkoloni, majumba ya mkoloni,
lakini wakitegemea the rural sector - the 8,500,000 vijijini ndio wawalishe chakula (food crops production), lakini pia vilevile mazao yao ya kilimo ndio yalipatie fedha za kigeni kunulia magari ya kifahari ya watawala, na kuwalipa posho na mishahara watawala;
Gamba la Nyoka, hivi kweli, ukiwa pale mezani na Mwalimu (1967) kumpinga on his Leadership code embedded in the Azimio La Arusha, unakuwa na uelewa wa hali halisi kweli - picha halisi ya Tanganyika in a socio-economic context, in 1967 ipo vipi na kama inaweza accommodate all that; Kwa kweli, in my humble opinion, wale wote wanaoshindwa kuelewa hili hata baada ya kui digest mara kadhaa, hakika wana haki ya kumwona Mwalimu alikuwa na matatizo kimaamuzi in 1967, na kwamba alilipoteza taifa hili, taifa ambalo kiuchumi leo hii halina tofauti na wenzetu walioamua kuingia soko huria 1962 (sio ujamaa kama sisi), moja kwa moja kama Kenya. Human Development Index Kenya puts us on the same league na wao; Hii haitoshi kutuambia kwamba tatizo letu sote waafrika sio Ujama au Ubepari bali ni the unfair integration of our societies into the global capitalist system? Ni vigumu kuelewa kwanini bado kuna watanzania wanaomlaumu Nyerere;
Otherwise, ni dhahiri kwamba kwa wakati ule (1967), hata kama viongozi, wangepewa haki ya kujitafutia riziki zao as you rightly put it Gamba La Nyoka, uchumi and the market for that haukuwepo, sana sana viongozi hao wangeishia tu kuiba mali ya umma. Akina kina Charles Njonjo pale Kenya, walikuwa wanawafanya watawala wetu Tanganyika, wadondokwe na mate kwa kutamani na wao wafaidi MATUNDA YA UHURU kama wenzao Kenya. Gamba la Nyoka, in 1967, matunda ya uhuru is for whom, the 50,000 Tanganyikans? The 8,500,000…?
Mimi nina imani kabisa kwamba hatua ya Mwalimu wa done on justified grounds; Kwani hata mwaka 1962, mwaka mmoja tu baada ya uhuru, aliwaondolea uvivu viongozi wenzake, kwa kuwapa maneno yafuatayo – TANU NA RAIA, 1962:
["Wakoloni walipokuwa hapa walipanga mishahara bila ya kujali uwezo wetu kuilipa mishahara hiyo, na bila kuilinganisha mishahara hiyo na mapato ya watu wetu. Lakini wao ilikuwa ni ada yao kufanya hivyo. Serikali ya wageni haiwezi kujali maisha ya raia. Serikali ya ilikuwa ni serikali ya ubwana na ufahari; na walijitimizia ubwana wao na fahari yao, bila ya kujali uwezo wa watu wetu wa kugharamia ubwana huo na fahari hiyo.
Lakini baadhi yetu tulikuwa hatutambui jambo hilo. Waafrika wengi tulikuwa tumekwisha kusahau kwamba mzigo ule wa ubwana na ufahari ni mzito mno na watu wetu hawawezi kuubeba. Kilichokuwa kikituuma ni kwamba ubwana ule na fahari ile wazungu waligawana wenyewe tu, bila kutugawia na sisi pia; baadhi yetu hatukuwa tunadai uhuru ili uwapunguzie watu wetu mzigo huu wa ubwana na ufahari, bali tama yetu ilikuwa ni kukalia viti vile vya ubwana na ufahari. Tamaa yetu haikuwa kushika vyeo tu, vilivyokuwa vimeshikwa na wazungu hapo zamani, tulitaka na mishahara pia iliyokuwa ikifuatana na vyeo bila kujali kama watu wetu wanaweza kulipa mishahara hiyo, na bila kujali maisha ya watu."]
JKN, Tanu na Raia, 1962.
********
Ntakurudia juu ya hoja zako nyingine.