Prof. Janabi apiga marufuku wagonjwa kusukumwa kwenye vitanda Muhimbili

Prof. Janabi apiga marufuku wagonjwa kusukumwa kwenye vitanda Muhimbili

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Ameagiza miili ya marehemu kupelekwa chumba cha kuhifadhia maiti kwa gari la wagonjwa (Ambulance), badala ya utaratibu uliokuwepo wa kusukuma vitanda ili kutoa heshima kwa marehemu kwa njia hiyo.

Prof. Mohammed Janabi aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), pia amesema Wagonjwa waliotoka Kitengo cha Dharura watabebwa na gari la wagonjwa kupelekwa wodini.

Kwa mujibu wa Prof. Janabi, mabadiliko hayo yanalenga kuwapunguza kazi na mizunguko Wagonjwa na Watendaji wa idara zinazopokea wagonjwa Hospitalini hapo pamoja na kuboresha huduma za Afya.

=======================

Miili ya marehemu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), sasa itapelekwa chumba cha kuhifadhia maiti kwa gari la wagonjwa Ambulance’, badala ya utaratibu wa kutumia vitanda.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Prof Mohammed Janabi, wakati alipokuwa anawaaga wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), alisema mabadiliko mengine ni wagonjwa wanaotolewa katika kitengo cha dharura watabebwa na Ambulance kupelekwa wodini.

“Ambalo tumeanza nalo leo ni kwamba bahati mbaya ikitokea mgonjwa amefariki mwili wa marehemu utachukuliwa na Ambulance kwenda kuhifadhiwa chumba cha kuhifadhi maiti.

“Wagonjwa waliotoka kitengo cha dharura watakuwa wanabebwa na gari la kubebea wagonjwa kupelekwa wodini.

“Kwa sababu ni hospitali kubwa, kwanza tutaanza kuboresha kwa wafanyakazi, itakuwa rahisi mwili kubebwa na Ambulance, kuliko kusukuma, kukiwa na vifo, mwili mmoja uko Kibasila, mwingine uko Sewahaji wanachoka wafanyakazi. Pia kutoa heshima kwa marehemu tunawahifadhi kwa njia hiyo,” amesisitiza Prof Janabi.

Amesema miongoni mwa vipaumbele vyake ni kuboresha huduma za afya na kuiendekeza Muhimbili kuwa hospitali ya Taifa.

Habari LEO
 
Mwanzo mzuri
Ila naona ni kuongeza gharama zaidi.. Wagonjwa wanaotoka na kuingia EMD, ICU, na Kwenye vipimo kama Xray, ct scan na wanaokufa ni wengi kwa ujumla wao.. Hizo Ambulance zitakuwepo ngapi?
Zile corridors za muhimbili zilisha kosewa. Ilifaa ziwe pana kiasi cha kuruhusu vigari vidogo kama vya kwenye kombe ka dunia kupita..

Nashauri ajikite kuboresha maisha ya wafanyakazi wake.. Awalipe Residents hela zao za calls, awape wafanya kazi motisha siku za siku kuu "kama zile za JKCI",
Ni aibu mfanyakazi hospital ya taifa kuwa na njaa-njaa😂😂..

Rejea case ya madaktari kuhama na wagonjwa waende nao private..

Lakini pia apunguze baadhi ya gharama za vipimo vya msingi.. "basic investigations"
Bado kuna malalamiko kuhusu flow ya taarifa kuhusu hali za wagonjwa.. Kuna baadhi ya wagonjwa wanaweza lazwa hata wiki, hata hawaelekezwi kinacho endelea, wanakuja kushtuka bili hiyooo...
 
Zile korido Kuna gari itapita mle,au mnadanganya watu
Kwa jinsi ilivyojengwa. Kila wadi inaweza fikiwa na gari.. Siyo kupitia kwenye corridor.. Kama ni kusukumwa basi itakuwa ni mita chache tu...

So wakiamua kuweka wese la kutosha na ambulance nyingi. Inawezekana
 
Back
Top Bottom