Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani zile tetesi kule mzena ni za kweli?Wako kisiasa zaidi kuliko kiuhalisia
Kumbe kagawa kazi kwa marafiki zako, lazimq umsifie tuu.Dr janabi huwa ni mtu smart sana .......hana uswahili, hapendi shobo za kifarafara, ukimuomba nafasi ya kazi kama ipo anakupa na kama haipo ankuweza wazi......wapo marafiki zangu wengi walio pata kazi kupitia dr janabi
Hospital ile ni kubwa umbal toka wodin had motuary n umbal wa kilometa moja au mbili au zaidi sasa ni kazi kubwa kwa muuguz mmoja kusukuma kitanda imagin labda cku iyo hilo wodi wana dead bodies zaid ya moja hiyo nenda rud huon kama ni kupoteza muda. Jaribu kulitafakari kwa upana hili jamboUfie wodini, mwili ubebwe na ambulance kwamba hizo gari zinaingia wodini? Najua mortuary ziko huko huko ndani ya majengo.
Hawa wasomi mbona wanatuchanganya?
Ameagiza miili ya marehemu kupelekwa chumba cha kuhifadhia maiti kwa gari la wagonjwa (Ambulance), badala ya utaratibu uliokuwepo wa kusukuma vitanda ili kutoa heshima kwa marehemu kwa njia hiyo.
Prof. Mohammed Janabi aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), pia amesema Wagonjwa waliotoka Kitengo cha Dharura watabebwa na gari la wagonjwa kupelekwa wodini.
Kwa mujibu wa Prof. Janabi, mabadiliko hayo yanalenga kuwapunguza kazi na mizunguko kwa Wagonjwa na Watendaji wa idara zinazopokea wagonjwa Hospitalini hapo pamoja na kuboresha huduma za Afya.
=======================
Miili ya marehemu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), sasa itapelekwa chumba cha kuhifadhia maiti kwa gari la wagonjwa Ambulance’, badala ya utaratibu wa kutumia vitanda.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Prof Mohammed Janabi, wakati alipokuwa anawaaga wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), alisema mabadiliko mengine ni wagonjwa wanaotolewa katika kitengo cha dharura watabebwa na Ambulance kupelekwa wodini.
“Ambalo tumeanza nalo leo ni kwamba bahati mbaya ikitokea mgonjwa amefariki mwili wa marehemu utachukuliwa na Ambulance kwenda kuhifadhiwa chumba cha kuhifadhi maiti.
“Wagonjwa waliotoka kitengo cha dharura watakuwa wanabebwa na gari la kubebea wagonjwa kupelekwa wodini.
“Kwa sababu ni hospitali kubwa, kwanza tutaanza kuboresha kwa wafanyakazi, itakuwa rahisi mwili kubebwa na Ambulance, kuliko kusukuma, kukiwa na vifo, mwili mmoja uko Kibasila, mwingine uko Sewahaji wanachoka wafanyakazi. Pia kutoa heshima kwa marehemu tunawahifadhi kwa njia hiyo,” amesisitiza Prof Janabi.
Amesema miongoni mwa vipaumbele vyake ni kuboresha huduma za afya na kuiendekeza Muhimbili kuwa hospitali ya Taifa.
Good job
Tulia kama hujui muhimbili ipoje unaweza ukaonekana una hoja na wajinga wenzako wakakuunga mkonoUfie wodini, mwili ubebwe na ambulance kwamba hizo gari zinaingia wodini? Najua mortuary ziko huko huko ndani ya majengo.
Hawa wasomi mbona wanatuchanganya?
Ambulance zipi zipo bize mkuu?niko hapa muhimbili hizo gari zimepaki hapo emagence kuna nyingine hata kuwashwa tu haijawashwa siku mbili au tatu mpk janabi anasema hayo amejua inawetekana hajakurupuka.Kwanza maiti huwa zinasukumwa kwa MACHELA MAALUMU AMBAZO ZIPO KAMA JENEZA toka wodin kwenda mortuary....kama watatumia magari itasaidia ila zile ambulance zipo busy sana aisee so ukizitumia kubebea maiti pia unaweza jikuta unashindwa kutimiza majukumu mengine unazunguka mule hospital kubeba miili maana wanaofariki wanakuwa location tofauti au waseme maiti ziwe zinaachwa mpaka USIKU ambulance ikapite kuzikusanya. So kama mtu kafariki leo na ndugu wana haraka na mwili wao kama waislamu inakuwa changamoto maana watalazimisha ambulance ikabebe maiti wakati ukute ina ratiba zingine. So ni wazo zuri ila ZISITUMIIKE AMBULANCE ILA HOSPITAL INUNUE KIGARI MAALUMU.
Kwaiyo unatakajeHakuna la maana hapo. Kuongeza gharama zisizo na msingi. Tutengeneze tu mapito yetu tungali hai mengineyo hayo ni kazi bure tu
Kwaiyo unataka ibebwe na niniAkili kisoda hana lolote, yaani utoe maiti wodini upeleke mortuary kwa Ambulance ? Duuuuuh hao ndio wasomi. Kwanza Ambulance haibebi maiti ni gari ya wagonjwa labda mgonjwa afe akiwa anawahishwa kwenye huduma.