Prof. Janabi apiga marufuku wagonjwa kusukumwa kwenye vitanda Muhimbili

Prof. Janabi apiga marufuku wagonjwa kusukumwa kwenye vitanda Muhimbili

Ufie wodini, mwili ubebwe na ambulance kwamba hizo gari zinaingia wodini? Najua mortuary ziko huko huko ndani ya majengo.

Hawa wasomi mbona wanatuchanganya?
unazijua mortuary zilipo na utajiskiaje ndugu yako anatolewa wodini akikokotwa juu ya kitanda mpka chumba cha maiti ambacho kipo zaidi ya mita 300 kutoka wodini. kwangu naona janabi yupo sahihi ni kuweka mifumo sawa
 
Mortuary muhimbili iko mbali na unakouguzwa, janabi hataki upitishwe hadharani ukiwa mfu watu wakuone
Mkuu hebu tuelezee vizuri na sisi tulioko mkoani kwani mochwari hapo muhimbili ziko mbali sana na maeneo ya huduma za matibabu ni kwa umbali gani mfano??

Sent from my SM-G935F using JamiiForums mobile app
 
Ameagiza miili ya marehemu kupelekwa chumba cha kuhifadhia maiti kwa gari la wagonjwa (Ambulance), badala ya utaratibu uliokuwepo wa kusukuma vitanda ili kutoa heshima kwa marehemu kwa njia hiyo.

Prof. Mohammed Janabi aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), pia amesema Wagonjwa waliotoka Kitengo cha Dharura watabebwa na gari la wagonjwa kupelekwa wodini.

Kwa mujibu wa Prof. Janabi, mabadiliko hayo yanalenga kuwapunguza kazi na mizunguko kwa Wagonjwa na Watendaji wa idara zinazopokea wagonjwa Hospitalini hapo pamoja na kuboresha huduma za Afya.

=======================

Miili ya marehemu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), sasa itapelekwa chumba cha kuhifadhia maiti kwa gari la wagonjwa Ambulance’, badala ya utaratibu wa kutumia vitanda.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Prof Mohammed Janabi, wakati alipokuwa anawaaga wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), alisema mabadiliko mengine ni wagonjwa wanaotolewa katika kitengo cha dharura watabebwa na Ambulance kupelekwa wodini.

“Ambalo tumeanza nalo leo ni kwamba bahati mbaya ikitokea mgonjwa amefariki mwili wa marehemu utachukuliwa na Ambulance kwenda kuhifadhiwa chumba cha kuhifadhi maiti.

“Wagonjwa waliotoka kitengo cha dharura watakuwa wanabebwa na gari la kubebea wagonjwa kupelekwa wodini.

“Kwa sababu ni hospitali kubwa, kwanza tutaanza kuboresha kwa wafanyakazi, itakuwa rahisi mwili kubebwa na Ambulance, kuliko kusukuma, kukiwa na vifo, mwili mmoja uko Kibasila, mwingine uko Sewahaji wanachoka wafanyakazi. Pia kutoa heshima kwa marehemu tunawahifadhi kwa njia hiyo,” amesisitiza Prof Janabi.

Amesema miongoni mwa vipaumbele vyake ni kuboresha huduma za afya na kuiendekeza Muhimbili kuwa hospitali ya Taifa.

Habari LEO
Akili kisoda hana lolote, yaani utoe maiti wodini upeleke mortuary kwa Ambulance ? Duuuuuh hao ndio wasomi. Kwanza Ambulance haibebi maiti ni gari ya wagonjwa labda mgonjwa afe akiwa anawahishwa kwenye huduma.
 
Yaani hao wengine wote waliotangulia hawakuwahi kuona kuwa hii haikuwa sawa? Kulikuwa na gharama gani ya kumtoa mfu kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa gari, humo humo ndani ya Hospitali?

Kwa sababu ukiangalia vizuri gharama yake ni ndogo mno kiasi kwamba hata mtu binafsi tu anaweza akajitolea hela ya mafuta ya kusafirisha watu hao kwa mwaka mzima, na asiji-feel kupoteza chovchote.

Prof. Janabi ameanza na Mungu na Mungu azidi kumbariki AENDELEE NA MUNGU NA AKAMALIZE NA MUNGU
 
Yaani gari itoke kubeba maiti kisha ikabebe mgonjwa kutoka emergence kumpeleka wodini!! Kwa nini kusiwe na magari maalum ya kubebea hizo dead bodies ili kutofautisha gari za kubeba maiti na gari za kubeba wagonjwa.?
 
Kuna watu mnachangia hii mada kwa mihemko tu nenda pale muhimbili kwanza ndio uje kutoa maoni yako hapa,wodi zipo mbali sana na motuari na ilikuwa mtu akifa atasukumwa kwenye likitanda lipo kama friji linapiga kelele mpk kero alafu wagonjwa wakiliona tu wanajua limefuata maiti wanazudi kuingiwa na hofu.
 
Kwanin wanajenga mochwari mbali sana
 
Prof yuko sahihi wodini na mochwari ni mbali ...kusukuma lile likitanda njiani lazima apumzike mara 3 au 4....kabla kuamua jambo watu wamefanya utafiti wa gharama na ufaninsi so tusikurupuke kulaumu laumu tu
 
Back
Top Bottom