Mzee baba hapo kwenye red sijakupata.
IPO HIVI,
Ukila wanga/Complex Sugar(mahindi, viazi, mihogo etc) mwili unaibadilisha kua glucose/Simple Sugar na unautumia kupata nguvu,
Ukisindilia sana mwili kwa kutumia INI unakusaidia kuhifadhi huo wanga/glucose kupeleka katika mfumo wa glycogen ambayo ndio mafuta sasa kwa namna nyingne.
Kwanini hubadilishwa???
huwezi ukahifadhi katika mfumo wa glucose, maana itayeyuka itarudi kwenye damu nakujaa/zidi matokeo yake ni KISUKARI sasa, ndio maana Katika kupima Sukari mwilini wanasema Blood glucose/sugar level, yaani kiwango cha sukari kwenye damu,
Pindi mwili ukiishiwa nguvu/mfano umechelewa kula au hujala, ile glycogen inatolewa kule ilikohifadhiwa kwa kutumia hormone ya glucagon kuileta kwenye mfumo wa glucose ambao ndio unatumiwa na mwili kupata nguvu.
Kwa nini mtu anazidi kunenepa? Kwa kula wanga,
Sbb ni kwamba kila siku anakula wanga iliyozidi kiasi kinachohitajika, matokeo yake inaendelea kuhifadhiwa/jaa kama mafuta kwenye mwili...
Haya tuconnect Dots..... sasa...,
Unapozungumzia wanga unazungumzia Sukari/sugar na ukizungumzia sukari unazungumzia glucose na ukizungumzia glucose unazungumzia Nguvu.
Glucose iliyozidi ni Mafuta, mafuta yaliyozidi ndio huo ubonge na madhara yake anayozungumzia prof.
Ushawahi jiuliza kwa nini wachezaji wanapewa glucose uwanjani sio Dona???