Prof. Janabi: Kitu hatari zaidi ni sukari na wanga. Ataka watu kula wakihisi njaa kwani mwili hauendeshwi na ratiba ya chakula

Prof. Janabi: Kitu hatari zaidi ni sukari na wanga. Ataka watu kula wakihisi njaa kwani mwili hauendeshwi na ratiba ya chakula

Kwenye kula tusipangiane kabisa ,, Mimi nakula nyama sana Yani kula kilo Moja na nusu ya kitimoto ni kitu Cha kawaida sana na ndizi nne ,pili pili kachumbali ,, kula tusipangiane tafadhari
 
Mmh haya naomba unisimlie hiyo ya form three inavo elezewa tuache ujuaji?
Tukiwaambia walimu wengi mlikuaga vilaza olevel mnalalami kuwa tunawakashifu. Na ukweli utabaki hivyo.

Twende kwenye issue uliotaka nikuelekeze. Nenda form three biology kuna topic inaitwa Coordinatation, humo utasoma sense organs zote ukimaliza Sasa ndio utagusa kipengele cha reflex action ambayo ni instant response to stimulus. Hapo pia utasoma classical (conditioned) reflex action ambayo ni an automatic response to a stimulus that differs from that initially causing the response, but that has become associated with it by repetition.

Sasa basi hapo my best biology teacher Madam Macha akakisanua mfano akatoa kulikuwa Russian scientist Ivan Pavlov. Yeye aliwatumia mbwa kutengeneza tabia ambayo ingejirudia lakini baada ya mbwa kunifunza hiyo tabia. (Salvation due to food). Alichofanya kila alipotaka kuwapa msosi mbwa aligonga kengele, mara za mwanzo mbwa hawakuwa wakitokwa na mate ya msosi ila aliporudia hicho kitendo kwa muda mrefu mbwa wakaunganisha chakula na kengele na wakajifunza kumbe kila wasikiapo kengele kuna msosi na hivyo wakawa wanatokwa udenda hata pale ilipogongwa kengele na chakula kutowekwa.

Brother acha kunichosha sisi wengine shule tulipekuwa vitabu vyote. Utakuta wewe hapo ndio mwalimu wa mwanangu pooooorer poooore[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Mkurugenzi wa hospitali ya Muhimbili, Profesa Mohammed Janabi amesema mpaka sasa wanawake 100 wamewekewa puto na wanaume wachache. Prof ameongeza kuwa puto ni kitu kimoja lakini nidhamu kwenye chakula ni kitu kingine.

Janabi amesema kitu hatari zaidi kwenye mwili ni sukari na wanga na wala si mafuta kwasababu mwili hautunzi wanga wala sukari bali huvibadilisha kuwa mafuta. Ametaka watu kupunguza matumizi ya vitu vyenye sukari, utamu mkubwa na sukari yenyewe.

Prof Janabi amesema matatizo ya kushindwa kupata watoto, moyo, kiharusi, magonjwa ya kupumua, vifo vya ghafla asilimia mkubwa vinachangiwa na uzito usio sahihi na kula mara kwa mara. Profesa amesisitiza kutopeleka mwili kwa utaratibu wa chakula bali wale chakula wanapohisi njaa.
Nikiangalia picha zake ni kama yeye prof ndie anaumwa kwa kukosa kula wanga na sukari, hakuna kisicho na faida au hasara muhimu kula wastani huo ndio mlo bora, matunda na mbogamboga kiasi, wanga kiasi kwa ajili ya kuleta nguvu mwilini n.k
 
Mzee baba hapo kwenye red sijakupata.

IPO HIVI,

Ukila wanga/Complex Sugar(mahindi, viazi, mihogo etc) mwili unaibadilisha kua glucose/Simple Sugar na unautumia kupata nguvu,

Ukisindilia sana mwili kwa kutumia INI unakusaidia kuhifadhi huo wanga/glucose kupeleka katika mfumo wa glycogen ambayo ndio mafuta sasa kwa namna nyingne.

Kwanini hubadilishwa???
huwezi ukahifadhi katika mfumo wa glucose, maana itayeyuka itarudi kwenye damu nakujaa/zidi matokeo yake ni KISUKARI sasa, ndio maana Katika kupima Sukari mwilini wanasema Blood glucose/sugar level, yaani kiwango cha sukari kwenye damu,

Pindi mwili ukiishiwa nguvu/mfano umechelewa kula au hujala, ile glycogen inatolewa kule ilikohifadhiwa kwa kutumia hormone ya glucagon kuileta kwenye mfumo wa glucose ambao ndio unatumiwa na mwili kupata nguvu.

Kwa nini mtu anazidi kunenepa? Kwa kula wanga,

Sbb ni kwamba kila siku anakula wanga iliyozidi kiasi kinachohitajika, matokeo yake inaendelea kuhifadhiwa/jaa kama mafuta kwenye mwili...

Haya tuconnect Dots..... sasa...,
Unapozungumzia wanga unazungumzia Sukari/sugar na ukizungumzia sukari unazungumzia glucose na ukizungumzia glucose unazungumzia Nguvu.

Glucose iliyozidi ni Mafuta, mafuta yaliyozidi ndio huo ubonge na madhara yake anayozungumzia prof.

Ushawahi jiuliza kwa nini wachezaji wanapewa glucose uwanjani sio Dona???
Umeelezea vizuri lakini glycogen siyo mafuta. Glucose ya ziada inahifadhiwa kama glycogen (form of glucose) au mafuta. Hayo mafuta ndio yanatufanya tuwe na viriba tumbo na unene
 
Mwili hautaki kula, wewe ndio unaujengea hiyo tabia. Mwili unacrave kitu unachouzoesha mara kwa mara!
Acha kulishwa ujinga wewe. Mwili hautaki kula? Wendawazimu kabisa huo mnadanganywa. Haya amua kutokula sasa uwe unashinda njaa tu ili mwili uzoee kutokula kwa week 2 tukuone. Bwege sana.
 
Kweli tunahitaji elimu me nilikuwa najua wanga inachakatwa kuwa lactose (glucose) iliyochangamka kumbe wanga kama makande bila marage na hayana kiini yanasababisha mafuta. ni hatari kwa kweli.

Kuna natamani kuuliza kwa idadi ya Tanzania wangapi wanakula wangu kwanini idadi ya wagonjwa ni chache. au kuna miili wakila wanga tatizo linatokea?
Wengi wana maisha magumu ndio maan hata wakila wanga na sukari havi waathiri sana sababu bado wana tumia nguvu kufanya shughuli zao za kila siku , kwa maana huchoma hiyo sukari wanao ila kila siku .Kama utafuatilia walio na maisha bora wengi wana magonjwa ya Moyo na kisukari hiyo ina dhihirisha kama unavyo sikia matatizo ya nguvu za kiume yaivyo kithiri ,kutokana na ulaji mbovu na wengine wako kwenye hatari ya kupata matatizo haya , ambapo kwa sasa wako kwenye ila hali tunaita ya kuwa na insulin resistant , ambapo niwako na ukaribu wakupatwa na ugonjwa wa kisukari na magonjwa mengine mengi yasio ambukiza .Hivyo ukitaka maisha bora, masuala ya wanga na sukari ni sio jamb salama.
 
Hapa kuna maelezo yanakosekana,kula wanga kama wewe ni mtu wa pilika pilika au mazoezi ya kutosha haina shida,shida iko kwa watu wanaokula wanga na maisha yao hayana mazoezi au shughuli zao ni za kukaa muda mwingi,Mfano mzuri watu wa kule vijijini wanatembea sana,unakuta mtu anatembea mpaka kilometer 10 kwa siku huo wanga au sukari vitamdhuru vipi..
Vijiji gani watu hutembea sana wakati pikipiki zimejaa vijijini
 
Huyu baba kwake kuna jiko kweli
Yuko against chochote kinachoenda mdomoni.
Kuhusu sex anasemaje??
Hahahaa anajua sana kuuza hofu. Hapo kwenye kukazana nahisi atasema kila ukitomba unapunguza mwaka mmoja wa kuishi.
 
Back
Top Bottom