Prof. Janabi: Kujifungua Mtoto 'Bonge' si nzuri Kiafya

Prof. Janabi: Kujifungua Mtoto 'Bonge' si nzuri Kiafya

Prof Janabi unatakiwa uelezee aina za vyakula na uzito wa kina Mama na mtoto kwa kuanzia mwezi wa kwanza mpaka kipindi cha kujifungua kuelezea hivi hivi tu bila kutatua tatizo ni sawa na wanasiasa haya tufanyeje ili kutatua hilo tatizo kwa Watoto watakaozaliwa hapo baadae njoo na Suluhuhisho sio vitisho tu kila kukicha...
Aelezee mara ngapi sasa kila siku anaelezea watu wapunguze au waache kula wanga na sukari
 
Kwahiyo yeye ndio mtaalam peke yake? Ukinywa maji mengi yana shida gani sasa?
Unapoteza madini mengi ya sodium kwa njia ya mkojo hajasema watu wasinywe maji amesema wasinywe kupitiliza ila kala mwili una kiu kunywa mpaka kiu ikate
 
Ni kweli kabisa
Unauliza kwa kejeli ila kunywa maji mengi kupitiliza ni hatari kwa afya.
Kwa taarifa yako kila kitu kizuri mwilini kinahitaji kiasi, sio excess.

Hata Oxygen gas hii tunayovuta nayo haitakiwi kuzidi inabidi ichanganyike kidogo na hewa nyingine. Ukivuta Oxygen ikiwa peke yake 100% unapata Oxygen poisoning na unaweza kufa.

Sasa wasiojua wanabisha na kuleta ujuaji kwenye afya. Professor halazimishi mtu yeye kafanya kazi yake, asiyetaka kufuata aache
 
Prof. Dr. Janabi hana huruma, yeye ni weka tuweke, yani ni ile simba wanasema UBAYA UBWELA anawavamia hadi watoto wadogo wasi na uwezo wa kujitetea 😂😂😂😂.

Marehemu waliofariki Wakiwa Wanene sana hawataingia PEPONI, maana watachelewa kufika, mioyo yao itakua imenyong’onyea sana.
 
Nyie mnaocomment negative hamjaenda muhimbili alfajiri kila siku uone mrundikano wa watu wenye matatizo ya moyo na figo wakihudhuria clinic na foleni zake. issue zote anazozisema Dr huwa anaclarify vizuri labda kama mtu unadandia mada ndio utachukulia na kulibeba kama kijujuu.
Exactly kiburi cha afya njema kinapotosha watu
 
Maoni yangu binafsi
huyu Prof awekewe brake, amegeuza udakitari sehemu ya kuchambana, anawajengea wananchi hofu kwenye maisha yao, japo kwake anagain cheap popularity, nahisi pia anatafuta umaarufu wa mitandaoni

Nafahamu alisoma huko nje, nafahamu pia alikua dakitari na swahiba wa Rais mstaafu, nafahamu pia........
Lakini hana mamlaka ya ku conclude kuhusu afya za watu, kuna watu ni wembamba tu lakini pressure yao, kisukari Chao, japo nafahamu anamaanisha ukiwa mnene unaongeza risks, sasa je anataka watu wanene genetically wajione walikosea kuumbwa, yeye amshukuru tu mungu yuko hivyo alivyo lakin asibeze wengine ambao hawawez kupunguza maumbile yao kirahisi , otherwise yeye angei insist tu mazoezi na diet lakin si kutaka dunia nzima watu wafanane,

Nafikiri pia anatafuta umaarufu wa kwenye mitandao kwa kuzingatia hali ya sasa ya dunia, na amewin
mimi ni mwembamba kiasi kama yeye lakini sifurahii namna amekuwa mtu wa kuconclude masuala ya kiafya, kama ana wakubwa zake wamshauri tu, uprofessor si mwisho wa kila kitu,
Au wampe nafasi ya Mobhare Matinyi, au ile ya Ummy Mwalimu, anaonekana ndiyo kazi anayoiweza vizuri kwa sasa, amekua na matamko yanayofuatana kuna nn nyuma yake..? akili kumkichwa
Wabongo hatuupendi ukweli sijui kwanini,mimi ushauri wake umeisaidia sana kuondoa kitambi na unene na kushusha digit za presha na kisukari nilikua naimani potofu kua mwili wangu ni wa asili,live long profesa janabi God bless u
 
Back
Top Bottom