Prof. Janabi: Kujifungua Mtoto 'Bonge' si nzuri Kiafya

Prof. Janabi: Kujifungua Mtoto 'Bonge' si nzuri Kiafya

Kwani wewe ungependa mtoto mdogo awe na uzito kupitiliza? Kimsingi haitaji taalumu ya kidaktari kujua uzito uliopitiliza ni hatari kwa afya
Watz tukibiwa ukweli tuna makasiriko hadi balaa! Ni ukweli wa kisayansi ambao hata yeye Prof km binadamu si rahisi kuuishi, tumpongeze kwa elimu anayoendelea kuitoa kuna wengi itakaowasaidia!

Kwani kumeza dawa ni kazi rahisi?! 😄
 
Achana na watoto wadogo my dear.ukijifungua agha khan ukijifungua kichakani kutoka salama na mtoto ni mipango ya Mungu
Nimemuuliza makusudi maana najua hajawahi kuingia leba nadhani ni mwanaume angekuwa mwanamke yeyote tena anaye jua Leba basi angejua kuchanika hakuhusiani na mahali unajifungua

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli Mtaalamu lakini kitu kikiongelewa hivi na Prof pana haja ya kuwa wazi zaidi sijui kama umenielewa maana Kliniki zetu unazijua sehemu zingine pana kesi watu wameshindwa kumhudumia Mgonjwa kisa laki na nusu sidhani kama pana Mama mjamzito ataenda hapo kupata Elimu na atapewa vizuri labda hizi Hospital za Private...
Hiyo no siku ya kujifungua,ila kuanzia miezi mitatu inabidi ahudhurie kliniki,kuna kila elimu hatua kwa hatua
 
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo na Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi amesema Wajawazito wanaojifungua Watoto Wanene wasidhani Watoto wao wana Afya njema.

Amesema "Pale Wodini unakuta mtu amejifungua Mtoto ana Kilo 4, ndugu wanasema Mashallah, hapo hakuna Mashallah, Mtoto ni 'Over Weight' huyo, si jambo la kufurahia ni tatizo hilo.

Ameongeza kuwa unene uliopitiliza kwa Mtoto unamuweka hatarini kuja kupata Magonjwa Yasiyoambukiza yakiwemo ya Figo, Moyo, Shinikizo la Juu la Damu pamoja na Kisukari anachoweza kupata kutoka kwa Mama.

Aidha, ameshauri Wajawazito kuzingatia ulaji mzuri wa Vyakula kwasababu una athari za moja kwa moja kwa Mtoto atakayezaliwa.

=============

Pia, mama anapokuwa mnene zaidi wakati wa ujauzito kutokana na ulaji wa mara kwa mara, hususan ulaji wa wanga kwa wingi, mafuta na mayai pamoja na chips, hatari yake ni uwezekano wa kujifungua mtoto mnene kupita kiasi.

Profesa Janabi, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), aligusia suala hilo juzi usiku wakati wa hafla uzinduzi wa Taasisi ya Profesa Jay jijini Dar es Salaam, yenye lengo la kuchangia fedha za matibabu ya wagonjwa wa figo.

Taasisi hiyo imeanzishwa na Mbunge wa zamani wa Mikumi (Chadema) na msanii wa Hip Hop, Joseph Haule maarufu Profesa Jaybaada ya kuugua ugonjwa wa figo uliomfanya kulazwa hospitalini siku 462, matibabu aliyosema yalikuwa ya gharama kubwa.

Katika maelezo yake, Profesa Janabi alisema ugonjwa figo ambao Profesa Jay anapambana nao chanzo chake kikubwa ni ugonjwa wa kisukari ambao unaendana na mfumo mbovu wa maisha.

Akifafanua, alisema huo mfumo wa maisha unaoleta madhara hadi kuambukiza mtoto aliyeko tumboni.

Alitolea mfano, kuwa mama mwenye kisukari ni rahisi kuzaa mtoto mwenye uzito kupita kiasi kwa kutokana na ile sukari inayozalishwa kwenye damu kumfikia.

“Mtoto aliyezaliwa na uzito mkubwa yuko hatarini kupata magonjwa yasiyo ya kuambukiza na jamii haipaswi kufurahi mama anapojifungua mtoto mwenye uzito mkubwa kwa kuwa ni hatari kiafya.

"Pale wodi ya wazazi unaona mtu amejifungua mtoto mwenye kilogramu nne, ndugu wanasema mashallah, hapo hamna mashallah mtoto ni over weight (amezidi uzito), si jambo kufurahia ni tatizo,” alisema.

Profesa janabi alisema “si sahihi kwa mtoto kuzaliwa akiwa na uzito mkubwa kupita kiasi, tujitahidi kupunguza uzito.”

Alisema ukiwa mzazi mnene hali hiyo unaiambukiza kwa mtoto.

“Sasa hivi tunashuhudia watoto wadogo wanakuja Muhimbili figo zimeharibika tunalazimika kuwapandikiza,” alisema Profesa Janabi.

Mariana Luvanga, mama mwenye watoto watatu alisema mara zote anapokuwa mjamzito hujitahidi kuzingatia maelekezo anayopewa kliniki na hajawahi kukutana na changamoto ya kupata mtoto mwenye uzito mkubwa au mdogo kupita kiasi.

“Ninachofahamu msisitizo mkubwa kwa mama mjamzito ni kula lishe bora ili kutoa virutubisho muhimu kwa mtoto anayekua tumboni. Hii ni pamoja na kula matunda, mboga, nafaka nzima, nyama, samaki, maziwa na bidhaa za maziwa.

“Kingine ni mazoezi mepesi ambayo ni msaada kwa mama hata kuufanya mwili wake usichoke na kumuondolea uwezekano wa kujifungua kwa upasuaji. Binafsi sijawahi kukutana na changamoto kubwa zaidi ya zile za kawaida za miezi mitatu ya mwanzo,” alisema Mariana

Wakati Mariana akieleza hayo, mmoja wa wazazi ambaye amewahi kupata mtoto mwenye uzito mkubwa aliliambia gazeti hili kwa miaka 11 mtoto wake ameendelea kuongezeka uzito, hali inayomfanya kuwa mvivu.

“Mtoto wangu alizaliwa na kilo 5.8 na alizaliwa kwa upasuaji, hadi sasa hatujagundua ugonjwa wowote ila naweza kusema mwili wake unamfanya kuwa mvivu. Sio mtu wa kujichanganya na licha ya kufanya mazoezi kidogo lakini uzito wake unaendelea kuongezeka,” alisema mzazi huyo ambaye hakutaka jina lake liwekwe wazi.

Gazeti hili lilizungumza na mkunga mstaafu, Salome Milinga aliyesema yapo mambo yanayochangia mjamzito kujifungua mtoto mwenye uzito kupita kiasi, ikiwemo mama kuwa na asili ya uzito mkubwa kabla ya ujauzito, kuongezeka uzito kupita kiasi wakati wa ujauzito na mama kuzaliwa na uzito mkubwa.

“Uzito wa mama unachangia kwenye uzito wa mtoto atakayezaliwa, ndiyo maana wakati wote kliniki huwa tunawasisitiza wazingatie mlo kamili, wasiache kula kwa sababu ni kipindi ambacho mwili unahitaji chakula lakini lazima iwe ni kiasi, si kutwa vyakula vya wanga na mafuta.

Sababu nyingine, anasema hutokea kwa akina mama wenye kisukari kwa sababu kwenye damu ya mama, hapa upo uwezekano wa mtoto kuzaliwa na uzito mkubwa kwa sababu anapata glucose nyingi mno kutoka kwenye damu,” alisema mkunga huyo.

MWANANCHI
Wachaga ndio ambao wana tabia ya kuover feed wake zao wanapokuwa wajawazito,sasa atuletee takwimu za kuonyesha kuwa wachaga ndio wanao ongoza kupata hayo maradhi...
 
Nyie mnaocomment negative hamjaenda muhimbili alfajiri kila siku uone mrundikano wa watu wenye matatizo ya moyo na figo wakihudhuria clinic na foleni zake. issue zote anazozisema Dr huwa anaclarify vizuri labda kama mtu unadandia mada ndio utachukulia na kulibeba kama kijujuu.
 
Nyie mnaocomment negative hamjaenda muhimbili alfajiri kila siku uone mrundikano wa watu wenye matatizo ya moyo na figo wakihudhuria clinic na foleni zake. issue zote anazozisema Dr huwa anaclarify vizuri labda kama mtu unadandia mada ndio utachukulia na kulibeba kama kijujuu.
Hao ndio madaktari wa JF ujuaji mwingi
 
Mie nikiwa mjamzito nakula kama kiwavi jeshi tena chips ni kila siku na hua naongezeka uzito wa kutosha lakini watoto wangu hamna aliyevuka 3.3kg. Sijui chakula kinapoteleaga wapi kama anavyosema profesa maana kula hua nakula kweli kweli tena carbs
Kama unakuaga na kisirani au gubu ukiwa na mimba, kamwe huwez nenepa[emoji28]
 
Watu wanvyoendelea kumbishia hivyo,
Unauliza kwa kejeli ila kunywa maji mengi kupitiliza ni hatari kwa afya.
Kwa taarifa yako kila kitu kizuri mwilini kinahitaji kiasi, sio excess.

Hata Oxygen gas hii tunayovuta nayo haitakiwi kuzidi inabidi ichanganyike kidogo na hewa nyingine. Ukivuta Oxygen ikiwa peke yake 100% unapata Oxygen poisoning na unaweza kufa.

Sasa wasiojua wanabisha na kuleta ujuaji kwenye afya. Professor halazimishi mtu yeye kafanya kazi yake, asiyetaka kufuata aache sio kesi.
Ninachompendea Profesa huwa habishani nawajinga, atakwambia tu Gharama za matibabu then ufanye maamuzi.
 
Back
Top Bottom