BabaMorgan
JF-Expert Member
- Dec 18, 2017
- 4,869
- 13,137
[emoji23][emoji23][emoji23] kwani uongo?Ahaaa fala wewe uliniona??
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji23][emoji23][emoji23] kwani uongo?Ahaaa fala wewe uliniona??
Ukiwaona yeye na mkewe afya zao hazieleweki....prof ngozi ya uso imekosa nuru kabisa sijui anashida ganiJamaa amekuwa ana frustration huyo sio wa kumuamini sana. Eti hata kunywa maji ni hatari kwa afya.
Yaani pale usitegemee kukojozwa .ni mbaya kiafya[emoji23][emoji23][emoji23] kwani uongo?
Mkwewe yukoje mkuu.??Ukiwaona yeye na mkewe afya zao hazieleweki....prof ngozi ya uso imekosa nuru kabisa sijui anashida gani
Upewe maua yakoNyumbani kwake kunapikwa kweli?? Sijui kama hata kuna jiko
Mbona mkewe kisu vile aisee profesa hana show mbovu .kaoa miss kabisaUkiwaona yeye na mkewe afya zao hazieleweki....prof ngozi ya uso imekosa nuru kabisa sijui anashida gani
Hakuna kitu kama hiko. Kwahiyo Mtaalam akikuambia kitu we unatekeleza tu bila hata kufikiria. Haya madhara ya kunywa maji mengi ni nini?
Hivi tule nini sasa, majini kama ng’ombe au?Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo na Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi amesema Wajawazito wanaojifungua Watoto Wanene wasidhani Watoto wao wana Afya njema.
Amesema "Pale Wodini unakuta mtu amejifungua Mtoto ana Kilo 4, ndugu wanasema Mashallah, hapo hakuna Mashallah, Mtoto ni 'Over Weight' huyo, si jambo la kufurahia ni tatizo hilo.
Ameongeza kuwa unene uliopitiliza kwa Mtoto unamuweka hatarini kuja kupata Magonjwa Yasiyoambukiza yakiwemo ya Figo, Moyo, Shinikizo la Juu la Damu pamoja na Kisukari anachoweza kupata kutoka kwa Mama.
Aidha, ameshauri Wajawazito kuzingatia ulaji mzuri wa Vyakula kwasababu una athari za moja kwa moja kwa Mtoto atakayezaliwa.
=============
Pia, mama anapokuwa mnene zaidi wakati wa ujauzito kutokana na ulaji wa mara kwa mara, hususan ulaji wa wanga kwa wingi, mafuta na mayai pamoja na chips, hatari yake ni uwezekano wa kujifungua mtoto mnene kupita kiasi.
Profesa Janabi, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), aligusia suala hilo juzi usiku wakati wa hafla uzinduzi wa Taasisi ya Profesa Jay jijini Dar es Salaam, yenye lengo la kuchangia fedha za matibabu ya wagonjwa wa figo.
Taasisi hiyo imeanzishwa na Mbunge wa zamani wa Mikumi (Chadema) na msanii wa Hip Hop, Joseph Haule maarufu Profesa Jaybaada ya kuugua ugonjwa wa figo uliomfanya kulazwa hospitalini siku 462, matibabu aliyosema yalikuwa ya gharama kubwa.
Katika maelezo yake, Profesa Janabi alisema ugonjwa figo ambao Profesa Jay anapambana nao chanzo chake kikubwa ni ugonjwa wa kisukari ambao unaendana na mfumo mbovu wa maisha.
Akifafanua, alisema huo mfumo wa maisha unaoleta madhara hadi kuambukiza mtoto aliyeko tumboni.
Alitolea mfano, kuwa mama mwenye kisukari ni rahisi kuzaa mtoto mwenye uzito kupita kiasi kwa kutokana na ile sukari inayozalishwa kwenye damu kumfikia.
“Mtoto aliyezaliwa na uzito mkubwa yuko hatarini kupata magonjwa yasiyo ya kuambukiza na jamii haipaswi kufurahi mama anapojifungua mtoto mwenye uzito mkubwa kwa kuwa ni hatari kiafya.
"Pale wodi ya wazazi unaona mtu amejifungua mtoto mwenye kilogramu nne, ndugu wanasema mashallah, hapo hamna mashallah mtoto ni over weight (amezidi uzito), si jambo kufurahia ni tatizo,” alisema.
Profesa janabi alisema “si sahihi kwa mtoto kuzaliwa akiwa na uzito mkubwa kupita kiasi, tujitahidi kupunguza uzito.”
Alisema ukiwa mzazi mnene hali hiyo unaiambukiza kwa mtoto.
“Sasa hivi tunashuhudia watoto wadogo wanakuja Muhimbili figo zimeharibika tunalazimika kuwapandikiza,” alisema Profesa Janabi.
Mariana Luvanga, mama mwenye watoto watatu alisema mara zote anapokuwa mjamzito hujitahidi kuzingatia maelekezo anayopewa kliniki na hajawahi kukutana na changamoto ya kupata mtoto mwenye uzito mkubwa au mdogo kupita kiasi.
“Ninachofahamu msisitizo mkubwa kwa mama mjamzito ni kula lishe bora ili kutoa virutubisho muhimu kwa mtoto anayekua tumboni. Hii ni pamoja na kula matunda, mboga, nafaka nzima, nyama, samaki, maziwa na bidhaa za maziwa.
“Kingine ni mazoezi mepesi ambayo ni msaada kwa mama hata kuufanya mwili wake usichoke na kumuondolea uwezekano wa kujifungua kwa upasuaji. Binafsi sijawahi kukutana na changamoto kubwa zaidi ya zile za kawaida za miezi mitatu ya mwanzo,” alisema Mariana
Wakati Mariana akieleza hayo, mmoja wa wazazi ambaye amewahi kupata mtoto mwenye uzito mkubwa aliliambia gazeti hili kwa miaka 11 mtoto wake ameendelea kuongezeka uzito, hali inayomfanya kuwa mvivu.
“Mtoto wangu alizaliwa na kilo 5.8 na alizaliwa kwa upasuaji, hadi sasa hatujagundua ugonjwa wowote ila naweza kusema mwili wake unamfanya kuwa mvivu. Sio mtu wa kujichanganya na licha ya kufanya mazoezi kidogo lakini uzito wake unaendelea kuongezeka,” alisema mzazi huyo ambaye hakutaka jina lake liwekwe wazi.
Gazeti hili lilizungumza na mkunga mstaafu, Salome Milinga aliyesema yapo mambo yanayochangia mjamzito kujifungua mtoto mwenye uzito kupita kiasi, ikiwemo mama kuwa na asili ya uzito mkubwa kabla ya ujauzito, kuongezeka uzito kupita kiasi wakati wa ujauzito na mama kuzaliwa na uzito mkubwa.
“Uzito wa mama unachangia kwenye uzito wa mtoto atakayezaliwa, ndiyo maana wakati wote kliniki huwa tunawasisitiza wazingatie mlo kamili, wasiache kula kwa sababu ni kipindi ambacho mwili unahitaji chakula lakini lazima iwe ni kiasi, si kutwa vyakula vya wanga na mafuta.
Sababu nyingine, anasema hutokea kwa akina mama wenye kisukari kwa sababu kwenye damu ya mama, hapa upo uwezekano wa mtoto kuzaliwa na uzito mkubwa kwa sababu anapata glucose nyingi mno kutoka kwenye damu,” alisema mkunga huyo.
MWANANCHI
Asante sana Mkuu kwa taarifa.Kg 3 mkuu hadi 3.5
KiaziKama kawaida Profesa uchwara..hahahahaha
Kiki zina mwisho na mwisho wake ni mbaya...
kikubwa ni tahadhariTutakufa hakika uwe mnene au mwembamba.
Siyo hiko ni hicho!?..unajua maana ya 'mtaalam'!?Hakuna kitu kama hiko. Kwahiyo Mtaalam akikuambia kitu we unatekeleza tu bila hata kufikiria. Haya madhara ya kunywa maji mengi ni nini?
Google madhara ya kunywa maji mengiHakuna kitu kama hiko. Kwahiyo Mtaalam akikuambia kitu we unatekeleza tu bila hata kufikiria. Haya madhara ya kunywa maji mengi ni nini?
Tahadhari ya kifo?kikubwa ni tahadhari
nazungumzia matatizo ya Watanzania mkuu sio mimi..Katafute wataalam wa lishe
Ni kweli Mtaalamu lakini kitu kikiongelewa hivi na Prof pana haja ya kuwa wazi zaidi sijui kama umenielewa maana Kliniki zetu unazijua sehemu zingine pana kesi watu wameshindwa kumhudumia Mgonjwa kisa laki na nusu sidhani kama pana Mama mjamzito ataenda hapo kupata Elimu na atapewa vizuri labda hizi Hospital za Private...Wahudhurie kliniki,kuna kila kitu
Msomi wa MMU Bwana. Eti wewe ndio msomi wa Kiislamu.Siyo hiko ni hicho!?..unajua maana ya 'mtaalam'!?
Google madhara ya kunywa maji mengi
[emoji23][emoji23]Yaani pale usitegemee kukojozwa .ni mbaya kiafya