Prof. Janabi: Kujifungua Mtoto 'Bonge' si nzuri Kiafya

Prof. Janabi: Kujifungua Mtoto 'Bonge' si nzuri Kiafya

Proffesa kanena vyema,Ila hapo kwenye sababu za matatizo ya Figo ndipo kapuyanga! kushindwa kumweleza ukweli tu Bwana Joseph Haule na wengineo,wengi wanaosumbuliwa na matatizo yanayofanana na hayo kuwa unywaji wa pombe uliopitiliza ndio Sababu! proffesa vp Tena?
calling a spade,spade not a big spoon
 
Mkitukanwa mnalalamika. Sasa hapo umejibu nini? Nakuuliza tena, yapi madhara ya kunywa maji mengi?
Figo haziwezi chuja maji endapo utakunywa mengi sana, zitazidiwa. Ukinywa maji mengi kiasi figo huchuja madini yabaki mwilini na maji ya ziada pamoja na takamwili zitoke nje kama mkojo.
Ukinywa maji mengi figo zitazidiwa utatoa maji nje yakiwa na madini kama Sodium yanayohitajika kwenye damu. Mwili utazidiwa maji utatapika, kupata kizunguzungu, ubongo kushindwa kufanya kazi vizuri mfano ukasahau kitu, kujishikiza uvivu, kuzirai au na kupelekea hadi kufariki.
 
Mtoto akitoka mdogo nayo inakuwa nafuu kwa mama kusukuma, sasa akiwa bonge si ndio maumivu makubwa ikiwemo kuchanika msamba? Wamama wale vyakula bora wakati wakiwa wajawazito
Haya mambo wazee walishayaona hata kabla ya ujio wa wakoloni.

Ndipo tulisikia masharti ya kuwatia hofu ili wasile vyakula fulani fulani maana hakukuwa na data za kisayansi za kuwasaidia waache uroho kipindi cha ujauzito.

Ndio maana kukawa na miiko ya ulaji. Mfano mjamzito alikatazwa kulanvyakula vya protini kama samaki, mayai, nyama, kipindi cha ujauzito ila walimkazania sana ulaji wa vyakula vya wanga, matunda na mboga za majani.

Waliwapa shuhuda za kutisha kama watoto kufia tumboni, au kuzaliwa hawana nywele/viparang'oto, watoto kuwa wafupi, etc.

Sayansi ilikuwapo Africa tena muda mrefu sana ila ni vile tulichagua kuipuuza.
 
Figo haziwezi chuja maji endapo utakunywa mengi sana, zitazidiwa. Ukinywa maji mengi kiasi figo huchuja madini yabaki mwilini na maji ya ziada pamoja na takamwili zitoke nje kama mkojo.
Ukinywa maji mengi figo zitazidiwa utatoa maji nje yakiwa na madini kama Sodium yanayohitajika kwenye damu. Mwili utazidiwa maji utatapika, kupata kizunguzungu, ubongo kushindwa kufanya kazi vizuri mfano ukasahau kitu, kujishikiza uvivu, kuzirai au na kupelekea hadi kufariki.
Hahaaaa, wacha weeeee. Kwahiyo kunywa maji yanaweza sababisha umauti?
 
Kwanza ajiangalie yeye mwenyewe afya gani ile, ashukuru ana kazi nzuri na anafanya kazi kwenye sekta ya afya tofauti na hapo iko afya nzuri
 
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo na Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi amesema Wajawazito wanaojifungua Watoto Wanene wasidhani Watoto wao wana Afya njema.

Amesema "Pale Wodini unakuta mtu amejifungua Mtoto ana Kilo 4, ndugu wanasema Mashallah, hapo hakuna Mashallah, Mtoto ni 'Over Weight' huyo, si jambo la kufurahia ni tatizo hilo.

Ameongeza kuwa unene uliopitiliza kwa Mtoto unamuweka hatarini kuja kupata Magonjwa Yasiyoambukiza yakiwemo ya Figo, Moyo, Shinikizo la Juu la Damu pamoja na Kisukari anachoweza kupata kutoka kwa Mama.

Aidha, ameshauri Wajawazito kuzingatia ulaji mzuri wa Vyakula kwasababu una athari za moja kwa moja kwa Mtoto atakayezaliwa.

=============

Pia, mama anapokuwa mnene zaidi wakati wa ujauzito kutokana na ulaji wa mara kwa mara, hususan ulaji wa wanga kwa wingi, mafuta na mayai pamoja na chips, hatari yake ni uwezekano wa kujifungua mtoto mnene kupita kiasi.

Profesa Janabi, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), aligusia suala hilo juzi usiku wakati wa hafla uzinduzi wa Taasisi ya Profesa Jay jijini Dar es Salaam, yenye lengo la kuchangia fedha za matibabu ya wagonjwa wa figo.

Taasisi hiyo imeanzishwa na Mbunge wa zamani wa Mikumi (Chadema) na msanii wa Hip Hop, Joseph Haule maarufu Profesa Jaybaada ya kuugua ugonjwa wa figo uliomfanya kulazwa hospitalini siku 462, matibabu aliyosema yalikuwa ya gharama kubwa.

Katika maelezo yake, Profesa Janabi alisema ugonjwa figo ambao Profesa Jay anapambana nao chanzo chake kikubwa ni ugonjwa wa kisukari ambao unaendana na mfumo mbovu wa maisha.

Akifafanua, alisema huo mfumo wa maisha unaoleta madhara hadi kuambukiza mtoto aliyeko tumboni.

Alitolea mfano, kuwa mama mwenye kisukari ni rahisi kuzaa mtoto mwenye uzito kupita kiasi kwa kutokana na ile sukari inayozalishwa kwenye damu kumfikia.

“Mtoto aliyezaliwa na uzito mkubwa yuko hatarini kupata magonjwa yasiyo ya kuambukiza na jamii haipaswi kufurahi mama anapojifungua mtoto mwenye uzito mkubwa kwa kuwa ni hatari kiafya.

"Pale wodi ya wazazi unaona mtu amejifungua mtoto mwenye kilogramu nne, ndugu wanasema mashallah, hapo hamna mashallah mtoto ni over weight (amezidi uzito), si jambo kufurahia ni tatizo,” alisema.

Profesa janabi alisema “si sahihi kwa mtoto kuzaliwa akiwa na uzito mkubwa kupita kiasi, tujitahidi kupunguza uzito.”

Alisema ukiwa mzazi mnene hali hiyo unaiambukiza kwa mtoto.

“Sasa hivi tunashuhudia watoto wadogo wanakuja Muhimbili figo zimeharibika tunalazimika kuwapandikiza,” alisema Profesa Janabi.

Mariana Luvanga, mama mwenye watoto watatu alisema mara zote anapokuwa mjamzito hujitahidi kuzingatia maelekezo anayopewa kliniki na hajawahi kukutana na changamoto ya kupata mtoto mwenye uzito mkubwa au mdogo kupita kiasi.

“Ninachofahamu msisitizo mkubwa kwa mama mjamzito ni kula lishe bora ili kutoa virutubisho muhimu kwa mtoto anayekua tumboni. Hii ni pamoja na kula matunda, mboga, nafaka nzima, nyama, samaki, maziwa na bidhaa za maziwa.

“Kingine ni mazoezi mepesi ambayo ni msaada kwa mama hata kuufanya mwili wake usichoke na kumuondolea uwezekano wa kujifungua kwa upasuaji. Binafsi sijawahi kukutana na changamoto kubwa zaidi ya zile za kawaida za miezi mitatu ya mwanzo,” alisema Mariana

Wakati Mariana akieleza hayo, mmoja wa wazazi ambaye amewahi kupata mtoto mwenye uzito mkubwa aliliambia gazeti hili kwa miaka 11 mtoto wake ameendelea kuongezeka uzito, hali inayomfanya kuwa mvivu.

“Mtoto wangu alizaliwa na kilo 5.8 na alizaliwa kwa upasuaji, hadi sasa hatujagundua ugonjwa wowote ila naweza kusema mwili wake unamfanya kuwa mvivu. Sio mtu wa kujichanganya na licha ya kufanya mazoezi kidogo lakini uzito wake unaendelea kuongezeka,” alisema mzazi huyo ambaye hakutaka jina lake liwekwe wazi.

Gazeti hili lilizungumza na mkunga mstaafu, Salome Milinga aliyesema yapo mambo yanayochangia mjamzito kujifungua mtoto mwenye uzito kupita kiasi, ikiwemo mama kuwa na asili ya uzito mkubwa kabla ya ujauzito, kuongezeka uzito kupita kiasi wakati wa ujauzito na mama kuzaliwa na uzito mkubwa.

“Uzito wa mama unachangia kwenye uzito wa mtoto atakayezaliwa, ndiyo maana wakati wote kliniki huwa tunawasisitiza wazingatie mlo kamili, wasiache kula kwa sababu ni kipindi ambacho mwili unahitaji chakula lakini lazima iwe ni kiasi, si kutwa vyakula vya wanga na mafuta.

Sababu nyingine, anasema hutokea kwa akina mama wenye kisukari kwa sababu kwenye damu ya mama, hapa upo uwezekano wa mtoto kuzaliwa na uzito mkubwa kwa sababu anapata glucose nyingi mno kutoka kwenye damu,” alisema mkunga huyo.

MWANANCHI
BIG BABY
 
ndiyo!
ndio maana japokuwa kila mmoja atakufa Ila tukitembea barabarani hatupiti katikati.
Unadhani watu hawapiti katikati sababu ya kifo? Sababu si kifo bali ni hakuna maslahi wala utamu wowote kupita katikakati ya barabara.

kifo huogopwa na wengi pale tu kisababishi cha hicho kifo kinapokosa maslahi au utamu.


Kama huamini Tangaza dau la malipo kwa kila anayepita katikati ya barabara uone kama hutapata wahusika wengi au ondoa utamu kwenye uke uone kama ukimwi utakuwa ni tatizo tena, Ondoa utamu kwenye junk food uone kama presha, kisukari itakuwa ni tatizo tena.

Suala si kifo, suala ni kisababishi cha kifo kina maslahi au utamu? Kama hakina kitaogopwa.
 
Nimewahi kumuuliza mnywa maji mmoja, kwanini anakunywa maji lita karibu 5 kwa siku anayapeleka wapi?


Akanijibu kuwa mwanadamu anatakiwa kunywa hizo lita 5 kwa siku.

Nikamwambia sidhani kama ni kweli (japo mimi si mtabibu) sababu wanadamu tuna miili tofauti, haiwezekani mimi wa kg 70 ninywe maji sawa na mtu mwenye kg 100 au kg 45.

Naamini labda hawa watamsaidia ndugu yangu yule. Maana naona anavyouchosha mwili wake bila yeye kujua.
 
Mie nikiwa mjamzito nakula kama kiwavi jeshi tena chips ni kila siku na hua naongezeka uzito wa kutosha lakini watoto wangu hamna aliyevuka 3.3kg. Sijui chakula kinapoteleaga wapi kama anavyosema profesa maana kula hua nakula kweli kweli tena carbs
 
Mie nikiwa mjamzito nakula kama kiwavi jeshi tena chips ni kila siku na hua naongezeka uzito wa kutosha lakini watoto wangu hamna aliyevuka 3.3kg. Sijui chakula kinapoteleaga wapi kama anavyosema profesa maana kula hua nakula kweli kweli tena carbs
Ukila na watoto wanakula sasa usiulize chakula kinaenda wapi maana unakua haupo peke yako Mama mjamzito unakua umebeba kiumbe kingine,
 
Back
Top Bottom