Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Wakuu!
Mmemsikia Prof. Mohamed Janabi, akiendelea kutupa madini ya kuzidi kulinda afya zetu? Ila hili limeniacha mdomo wazi kidogo kuhusu kunywa juice ambayo tuaamini ni sehemu ya kuboresha afya tena zile juice za kutengeneza mwenyewe.
==================
MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Mohamed Janabi, amesema ulaji wa chakula cha kila siku ndio unaotafsiri afya ya sasa na baadae, na kwamba walio na umri kuanzia miaka 35 ama 0 na kuendelea kuwa makini na aina ya mlo.
“Binafsi huwa sinywi juisi iliyotengenezwa au iliyotokea viwandani ni takribani miaka 20 tangu mwaka 2000. Sichanganyi matunda, nakula asubuhi tunda moja labda ndizi, mchana peazi na usiku kipande cha papai,” ameongeza.
“Jamii ibadili mtazamo kwamba uwekezaji wa maisha ya baadae, unaegemea kwenye uwekezaji wa mali, bali hatua hiyo inahitajika kwenye afya pia.”
Soma Pia: Tukifuata ushauri wa Professor Janabi tutaangamia kwa njaa
Prof. Janabi ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo, anayasema hayo kupitia ukurasa wake wa kijamii kuhusu maisha bora, ikiwa ni mwendelezo wa elimu kwa umma, kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza (NCDs) kama vile kisukari, presha na saratani.