Prof. Janabi: Sijanywa juisi aina yoyote takriban miaka 20

huyu alisoma mpk nafikiri akataka kuelekea kuwa.........
 
Wakuu!

Mmemsikia Prof. Mohamed Janabi, akiendelea kutupa madini ya kuzidi kulinda afya zetu? Ila hili limeniacha mdomo wazi kidogo kuhusu kunywa juice ambayo tuaamini ni sehemu ya kuboresha afya tena zile juice za kutengeneza mwenyewe.

==================

MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Mohamed Janabi, amesema ulaji wa chakula cha kila siku ndio unaotafsiri afya ya sasa na baadae, na kwamba walio na umri kuanzia miaka 35 ama 0 na kuendelea kuwa makini na aina ya mlo.

“Binafsi huwa sinywi juisi iliyotengenezwa au iliyotokea viwandani ni takribani miaka 20 tangu mwaka 2000. Sichanganyi matunda, nakula asubuhi tunda moja labda ndizi, mchana peazi na usiku kipande cha papai,” ameongeza.

“Jamii ibadili mtazamo kwamba uwekezaji wa maisha ya baadae, unaegemea kwenye uwekezaji wa mali, bali hatua hiyo inahitajika kwenye afya pia.”

Soma Pia: Tukifuata ushauri wa Professor Janabi tutaangamia kwa njaa

Prof. Janabi ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo, anayasema hayo kupitia ukurasa wake wa kijamii kuhusu maisha bora, ikiwa ni mwendelezo wa elimu kwa umma, kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza (NCDs) kama vile kisukari, presha na saratani.
Kwamba ndio ataishi milele au!?
 
Huyu mzee muongo
Atakuja kusema hata kuwagegedua wake zetu sio vizuri kiafya
 
Janabi hapa Mazembe Segerea.
Baada ya hapo nashushia tu'castle lite tuTANO
20241013_195653.jpg
 
Ndiyo maana uso wake hauna nuru, mtu gani Kila kitu yeye hataki tule

Juice hataki tunywe

Nyama hataki tule

Samaki hataki tule

Biryani hataki tule

Beer hataki tunywe

Ugali hataki tule

Juzi nilikuwa mitaa ya Ofisi yake, nilikuwa nimeagiza wali Samaki na kachumbali, kuona anakaribia kwenye Meza yangu akafanya hadi nizuge chakula hakikua changu maana alishaanza kunipa risala zake 🙌

Sasa sijui anataka tufe na njaa kabisa ama nini 🙌
acha uongo mzee janabi ukutane nae wapi wewe😁😁😁
 
Wakuu!

Mmemsikia Prof. Mohamed Janabi, akiendelea kutupa madini ya kuzidi kulinda afya zetu? Ila hili limeniacha mdomo wazi kidogo kuhusu kunywa juice ambayo tuaamini ni sehemu ya kuboresha afya tena zile juice za kutengeneza mwenyewe.

==================

MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Mohamed Janabi, amesema ulaji wa chakula cha kila siku ndio unaotafsiri afya ya sasa na baadae, na kwamba walio na umri kuanzia miaka 35 ama 0 na kuendelea kuwa makini na aina ya mlo.

“Binafsi huwa sinywi juisi iliyotengenezwa au iliyotokea viwandani ni takribani miaka 20 tangu mwaka 2000. Sichanganyi matunda, nakula asubuhi tunda moja labda ndizi, mchana peazi na usiku kipande cha papai,” ameongeza.

“Jamii ibadili mtazamo kwamba uwekezaji wa maisha ya baadae, unaegemea kwenye uwekezaji wa mali, bali hatua hiyo inahitajika kwenye afya pia.”

Soma Pia: Tukifuata ushauri wa Professor Janabi tutaangamia kwa njaa

Prof. Janabi ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo, anayasema hayo kupitia ukurasa wake wa kijamii kuhusu maisha bora, ikiwa ni mwendelezo wa elimu kwa umma, kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza (NCDs) kama vile kisukari, presha na saratani.
Profesa ana madini huyu!
 
Watu tunatofautiana asipangie watu wote kama tuko sawa
Ameishi na wagonjwa sana mpaka kachanganyikiwa anaona sisi wote wagonjwa

Nimevuka miaka 60 kitambo na nakunywa kila aina ya juice na coke cola na chai ya sukari lazima
Chakula chumvi lazima aje anikataze
Sina pressure wala nini
Huyu naona wagonjwa wamemuathiri sana na ana ugonjwa wa wasiwasi tu hakuna kingine
Sura haionyeshi ni mzima mbona
 
acha uongo mzee janabi ukutane nae wapi wewe😁😁😁
Hahaha..........Mkuu achana na ID fake

Piga picha umekaa Samaki Samaki Mlima city na Mimi Mzee Grahams tunakula monde, utajisikiaje Mkuu 🤗

Toka nje ya hizi ID fake, wale watu wa mitaani ndiyo hawa hawa kwenye hizi ID zetu 😜
 
Ha haaaa haaa. Hadi ulizuga chakula sio chako!? Kazi ipo
Akukute na msosi Mkubwa ule watu wa kanda ya Ziwa tunakula, lazima akupige risala

Hachelewi kusema mbona unakula ugali wa watu 4 peke yako

Atakwambia kachumbali zinaleta minyoo tumboni, wakati hapo hapo Kuna baadhi ya writings zinasema kula kachumbali ni dawa 🙌
 
Huyu mzee ndo maana afya yake ni same same na dr shika 400 itapendeza.kiufupi ana afya hafifu sababu ya mtindo wake mbovu wa kula.asubuhi ndizi moja kweli?kipande cha papai wakati unatakiwa kula papai zima na ugali nusu kilo nzima
 
Mzee analeta diet kwenye kula yake 🙌
 
Back
Top Bottom