Prof. Janabi: Sijanywa juisi aina yoyote takriban miaka 20

Huyu mwamba sijui watoto wake wanamuonaje!
 

Kwahiyo anataka kutuambia nini? Maana naona kama ngozi yake hata nuru inakosa. Unaachaje kula kwa staha sababu ya kuogopa utakufa?
Ngoja tuyaone
 
Juice za viwandani sio nzuri kwa afya, alitakiwa kuwaambie watu watumie juice walizotengeneza wenyewe.

Lakini viwanda vina sababu ya kuwepo. Sio kila sehemu kuna matunda mengi kama Tanzania. Prof anajichanganya. Dunia hii kila mtu aishi miaka zaidi ya 70 ili iweje?
Kuna watu toka wanazaliwa wagonjwa. Na kuna wengine mpaka wanazeeka hawajui ugonjwa. Tusichanganye mambo hapa. Kufa na kuzaliwa ni ahadi na anayetoa ni Mwenyezi Mungu tu. hata tukipenda vipi maisha, kufa lazima
 
uko sawa lakini kuchukua tahdhari ni muhimu, vinywaji vya viwandani vina madhara madhara kiasi gani ni jinsi unavyotumia.
 
uko sawa lakini kuchukua tahdhari ni muhimu, vinywaji vya viwandani vina madhara madhara kiasi gani ni jinsi unavyotumia.

Tahadhari muhimu. Ila sio kudanganyana hapa kwamba lishe imekuwa kitu rahisi kwa kila mtu. Ukiwaona wanaoshindia mlo mmoja kwa siku sababu hawana option ya kula tofauti, utaelewa maana halisi ya ugumu wa maisha.
Akipata juice za box, atakunywa kwa raha zake. Kinachosikitisha ni kama vile assumption ni wote tuko level ile ile kwa kipato na maisha
 
Pole sana mkuu
 
Kwamba Prof Janabi ni mbobevu kwenye masuala ya Lishe kuliko wataalam wa Lishe? Kwamba hajui mchanganyiko wa aina flani ya matunda yakichanganywa pamoja yanatengeneza alkali na kupunguza kiasi cha acid tumboni?
Ajikite kwenye mambo ya Moyo aachane na mambo ya Lishe...Kuna wakati ma2zo yake yanapotosha waziwazi alafu wataalam hawamwambii ukweli sijui wanamwogopa kisa ni boss wao?
 
huyu siku hizi amekua mtu wa spinning kama makonda
 
Ukiondoa, Kula , kunywa na Ngono,....hii Dunia haina maaana kabisaaaa,....

muhudumu,..lete kitimoto kilo, na ndizi nne za kuponda,.....usisahau juice ya pasion jagi mbili,..

unafukiwa na kifusi ukiwa na Afya yako tele,..na msaada hupati...
janabi🚮
 
Basi afunge zile canteen zote zilizopo MNH, tujuwe moja kuwa hakuna kula
 
Yule Mzee sijui hata kama familia yake inakulaga hata nyama, hachelewi kuwalisha maharage Mwaka mzima 😜
Mungu amekupa mwili na appetite halafu unaanza kumkosoa MUNGU??

Mbona kufa kupo tu? Kwani mtu aishi miaka mingapi? Mungu katupa mamlaka kwenye wanyama watembeao na watambaao pia na mimea.

Kwanini uishi kwa shida na kujinyima bila sababu? Unataka uishi kama Methuselah wa kwenye biblia??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…