BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Rapa Mkongwe na Mbunge wa zamani wa Mikumi, amesema hayo na kuongeza kuwa safari yake ya kuugua tatizo la Figo ilifanya afikie hatua ya kutobolewa Koo ili kuondoa uchafu uliokuwa ukisababisha ashindwa kuongea, pia, alikuwa akichoma Sindano inayogharimu Tsh. Milioni 5 ambapo alitakiwa kuchoma Sindano 10.
Akizungumza zaidi, Msanii Black Rhyno ambaye ni mdogo wa Prof. Jay amesema kuna wakati kaka yake alipata hali ya Moyo kusimama mara 3 katika vipindi tofauti lakini juhudi za Madaktari na huruma ya Mungu zilimnusuru na kifo mkongwe huyo.
Aidha, Prof. Jay akizungumza na #CloudsFM amesema Ugonjwa wa Figo ulifanya apelekwe hadi Hospitali ya Apollo India lakini pia, umempa funzo na ndio maana ameanzisha 'Foundation' itakayohusika na masuala ya kusaidia Watu wanaosumbuliwa na Ugonjwa huo.