Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Mtu ambaye anataka kucheza soka, ukimshinda katika tennis, halafu ukamcheka kwamba hajawahi kuwa mwanamichezo mzuri, unamuonea.
Yeye ni mwanamichezo mzuri katika mchezo wa soka.
Wewe unampima uanamichezo kwa kigezo cha tennis.
Waafrika hatukuwahi kuwa na mshawasha wa kutaka maendeleo ya kiuchumi.
Mshawasha wetu kwa miaka mingi sana umekuwa wa kutaka kuwa na mahusiano mazuri na wenzetu, kufanya subsistence farming, ufugaji wa kiushkaji, kumsifu chifu, siku zinaendelea.
Ndoyo maana mpaka leo rais anavunja katiba keft, right and center. Wananchi wanamshangilia. Wengi sana.
Ni utamaduni wetu huo, mkubwa hakosei.
Hata akikosea, usiseme kakosea, sema "washauri wake wamemshauri vibaya".
Ukisema kakosea, utaharibu "social harmony".
Hatukutaka mali sana, kwa sababu bara letu limejaa mali ni kitu tunachukulia for granted, hatuna haja yakulimbikiza mali. Utalimbikiza nyama iwe yako mwenyewe kwanza utaitynza wapi? Halafu wenzako wana njaa, utajisikiaje kuwa na nyama kibao wakati wenzako wana njaa?
Waziri Mkuu wa Uingereza Winstin Churchill alisema kwamba watu wa Uganda walikuwa hawana pressure na maisha, kwa sababu nchi yai mazao yanazaa mwaka mzima (hakuna winter) kuna misitu, mashamba na matunda mengi, maji kika mahali kuanzia mito mpaka ziwa, hawana tabu. Hawana pressure ya kulimbukiza mali, kwa sababu walijua wakikosa sana watachuma maembe watakula, maisha poa tu. Hawahitaji stock market.
Wageni wamekuja na model moya, weka nyama kwenye friji, kila mtu atajiju.
Sasa sie ambao hatuna utamaduni wa umimi, tukishindwa kujilimbikizia mali na kuendelea kiymuchumi, tunashindea mchezo ambao sio wetu.
Tumekua tunacheza soka.
Leo unatupima uanamichezo wetu kwa mechi ya tennis?
Ndiyo maana hata keo haya mambo ya kigeni ya vyama vya siasa, mara demikrasia, mara banking system, mara serikali ya mihimiki mitatu inayotazamana, mara bunge ka Westminster, mara kusoma Chuo Kikuu, kwa sehemu kubwa ni mambo ya maigizo tu. Si mambo ambayo yanatoka ndani kabisa ya utamaduni wetu.
Tunaigiza tu.
Mchezo wa tennis, wa kigeni. Unatushinda. Wa kwetu soka umetupwa.
Sasa kama sisi Waafrika hatukuwahi kuwa na mshawasha wa kutaka maendeleo ya kiuchumi, nini kinatufanya tusiendelee kuishi bila huo mshawasha?
Ila, historia ya falme na himaya za zamani inaonyesha kuwa mshawasha wa biashara na ujasiriamali ulikuwepo.
Hayo mambo mawili si ndo kiini cha maendeleo ya kiuchumi?