Prof. Kabudi afafanua serikali tatu katika Jenerali on Monday

Prof. Kabudi afafanua serikali tatu katika Jenerali on Monday

Serikali tatu ni wazo la kijinga sijapata kuona!!

Na kama tukikubali muundo wa hivyo tutakuwa mazumbukuku tusio na uti wa mgongo!!

Ni kweli . Muungano wa kweli ni wa serikali moja. Hatujafikia hapo kwa bahati mbaya Bali ni matokeo ya usaliti, ubaguzi na unafiki wa viongozi waliopewa dhamana kutuongoza, ambao kwa miaka mingi wameshindwa kusoma hisia na matakwa ya wananchi, hususan, wasio na sauti.
 
Serikali tatu ni wazo la kijinga sijapata kuona!!

Na kama tukikubali muundo wa hivyo tutakuwa mazumbukuku tusio na uti wa mgongo!!

Mimi sijui nipoje.hawa maprofesa watz huwa siwaelewi kabsaaa...

Binafsi naamini katika "NCHI MOJA, WATU WAMOJA, SERIKALI MOJA" Hayo mambo ya serikali 3 yanatoka wapi!?!? watz hebu tuache kujitoa ufahamu. Prof Kabudi i salute you kama best Tanzanian graduate katika field ya sheria. Mambo gani hayo unafanya
 
Mkuu unadhani zanzobar wange/watakubali serikali moja? Never over my dead body! Wametumia busara sana wazee hawa kuamua serikali tatu
 
Hofu inajitokeza kwa kuwa hatujaingia bado kwenye serikali tatu. lakini kwa hali ilivyokuwa hakukuwa na namna nyingine. kutakuwa na changamoto mara muundo huo utakapoanza. lakini ikiwa mamlaka kuu itakuwa katika serikali ya muungano na katiba zilizopo zitafuatwa bila kuingiliana nchi itakwenda. ikumbukwe kuwa vyombo vyote vya dola vitakuwa chini ya muungano, yapo mambo ya muungano yatakayofanyika chini ya wizara ambayo yatkuwa muhimili wa muungano. atakayetenda kinyume kutoka upande mmoja atakuwa muasi na hivo sheria zitachukuliwa dhidi yake maana amirijeshi mkuu ni rais wa muungano na atatiiwa na majeshi yote. ukitafakari sana utaona tatizo si kubwa kihivyo.
 
Nipo namfatilia. Kwa jinsi anavyochambua hyo rasimu ya pili ya katiba ni ngumu sana kwa mwananchi wa kawaida kuielewa.. Too complicative..

Waziri mkaazi..!!??

Wat tha hell is this??

Sidhani kama hii ratiba ita restore amani inayopotea.
complicative ina maanisha nini?
 
Mtahangaika sana na serikali mbili ila wananchi wanataka serikali tatu
 
Serikali tatu ni wazo la kijinga sijapata kuona!!

Na kama tukikubali muundo wa hivyo tutakuwa mazumbukuku tusio na uti wa mgongo! UKITUKANA BILA HOJA HAIRAIDII.

Wavivu wa kufikiri na kusoma wamejaa matusi vinywani mwao.Mchangiaji mwenye matusi hajasoma rasimu kasikia tu kwa watu wengine ni wakumsamehe tu uvivu wa kufikiri na kuchambua hoja unamsumbua.
 
Serikali tatu ni wazo la kijinga sijapata kuona!!

Na kama tukikubali muundo wa hivyo tutakuwa mazumbukuku tusio na uti wa mgongo! UKITUKANA BILA HOJA HAIRAIDII.
Inaelekea tumejawa na hofu ya serikali tatu bila sababu za kutosha. Suala ni serikali tatu si mataifa matatu kwa maana ya sovereign states. it will be just as organizational structure under one country Tanzania, labda kama alivoshauri Ulimwengu neno rais libadilishwe maana ni zito sana tutafute lingine labda gavana. ikiwa akili zetu zitajiandaa kwa maana hii tutadumu. tatizo naloliona ni wakati wa bunge la majadiliano ikiwa wengi watasukumwa na hofu ya serikali tatu basi hatari yake ni kubwa kupita kiwango! kwa wale waliotahiriwa watajua hofu iayompata kijana kabla ya tendo lakini tendo lenyewe ni jema likikamilika ni ushujaa. Hata hili la katiba linawatia hofu watu lakini likikamilika tutakuwa mashujaa na JK atatoka kidedea na atakumbukwa kwa ushujaa.
 
Hapo kwenye red haikubaliki! Mtawala wa Tanganyika, taifa lile kuu, hatapigiwa mizinga 21? Tukatae ujinga huu, Kiongozi wa Tanganyika lazima apate heshima anayostahili; Tanganyika ndiyo itakayolisha muungano kwa kila kitu, kuanzia watoto kwenda chooni hadi ulinzi dhidi ya maadui wa nje - halafu nini? Sielewi!

Ahahahahahaaaaaaaaaaaaaa
Hahaahaaaaaaaaaa hahahahahahhaaaa
Kwi kwi kwi kwi kwiiiiiiiiiiiiii
Ka ka ka ka kaa kaaaaaaaaaaaaa
Heheheehheheheheheeeeeeeeee
Huhuhuhuhuuhuuuuuuuuuuuu
Yeree uuuuuuuuuuuuuuuuuwi.....
Woy woy woy woooooooy.....

Jamanii eeeeeeeeeeh mbavu zangu.
Mbavu zangu jameniiiiiiiiii

Yaani cha muhimu umeona ni mizinga tu ktk mambo yoooooooote.

Teh teh te te te teeeeeeeeee

Hahahaaaàaaaaaaa
 
Serikali moja kila kitu, kama wazenj hawataki kuiua zenj yao waondoke watuache na Tanganyika yetu, hizi serikali tatu zitaleta more confusions
 
Ni kweli . Muungano wa kweli ni wa serikali moja. Hatujafikia hapo kwa bahati mbaya Bali ni matokeo ya usaliti, ubaguzi na unafiki wa viongozi waliopewa dhamana kutuongoza, ambao kwa miaka mingi wameshindwa kusoma hisia na matakwa ya wananchi, hususan, wasio na sauti.
Mkuu nafarijika sana nikiona wanaoamini katika serikali moja kama mimi., nilipendekeza iwe hivyo ila ndo basi tena
 
Zanzibr haitaki tena kutawaliwa na mkoloni mweusi,tokea mwanzo wa huu ukoloni zanzibar imejionyesha kuwa haitaki kutawaliwa,cha ajabu watanganyika hawaelewi,hapo kwenye tatu tunafahamu kuwa watanganyika hamkubali kwa hiyo ukoloni wenu mtauacha na kushughulikia tanganyika yenu maana lile koti la muungano halina msaada kwenu na hapo ndipo mtakapo uvunja wenyewe watanganyika,lengo la zanzibar huru limetimia,zanzibar kwanza.
 
prof.kabudi katizima sura ya nje hebu atizme sura ya ndani ktk serekali 3 halafu atizame kipi zanzibari itazidi kukipoteza kwa uwakilishi wawo kama taifa la kizanzibary kiutamaduni na kihistoria. ndio maana wawo wanataka jinamizi hili la kupewa serikali isiyonamadaraka kamili liwaepuke,na wanaomba uck na mchana kama alivyo omba Yesu kuepushwa na kombe la umauti.
 
Anaendelea na kipindi now. Anasema baadhi ya watu wanaona serikali mbili kama ushirikina au dogma ya kila kitu katika tanzania kitu ambacho sio sahihi
Prof asitubabaishe na dhana ya ushirikina .Serekali tatu za rasimu ni bomu.Prof aeleze
1)Serekali ya shirikisho itaanzaje kabla ya katiba na serekali ya tanaganyika?uhalali huo utatoka wapi?tanganyika itaongozwaje?2)Ikulu na bunge kwa ajili ya shiriksho vitakuwa wapi maana tanganyika itachukua vitu vyake?Zanzibar itachangia nini katika shirikisho wakti idadi yake ya wstu ni 2.9%,pato la taifa 1% na eneo 0.3%?3)vipi zenj wapewe 27% ya viti bungeni?
 
Serikali tatu ni wazo la kijinga sijapata kuona!!

Na kama tukikubali muundo wa hivyo tutakuwa mazumbukuku tusio na uti wa mgongo!!

Na Sisi Serikali 2 au 1 hatukubali hata siku moja maana nyie Vibaraka wa CCM mnajifanya Wasomi sana kumtumikia Bwana Wenu CCM mnaojifanya mna Hati miliki ya nchi
 
Serikali tatu ni wazo la kijinga sijapata kuona!!

Na kama tukikubali muundo wa hivyo tutakuwa mazumbukuku tusio na uti wa mgongo!!

Marekani wana serikali 53, 52 za states na 1 serikali kuu. Kila state ina mtawala mwenye mamlaka kamili, katiba inayoongoza state, senator, congress na bendera yake. Wana bajeti yao na kuna baadhi ya shughuli za uchumi katika kodi kuchangia serikali kuu. Kama hao wameweza nchi moja kuwa na serikali 53, kwa nini tushindwe kuwa na serikali tatu?

UK nako wana serikali kadhaa ikiwemo ile ya Scotland, Ireland, na England.

Miaka nenda rudi wanaendesha shughuli zao vizuri tu na wameweka taratibu ambazo hazileti migongano na mambo ni poa kabisa, nini tatizo wabongo tushindwe wakati Zanzibar tayari wameshafanikiwa na tumebaki watanganyika tu?
 
Serikali tatu ni wazo la kijinga sijapata kuona!!

Na kama tukikubali muundo wa hivyo tutakuwa mazumbukuku tusio na uti wa mgongo!!

Serikali tatu sio wazo, bali ni nia kama ilivyowekwa kwa mujibu wa mkataba wa muungano miaka hamsini iliyopita. Kama ni suala la kijinga, kwanini basi mkataba wa muungano ulikuja na masuala ya muungano (yanayohitaji serikali yake) na masuala yasiyokuwa ya muungano (which means serikali shiriki ambazo ni mbili zilitakiwa ziyasimamie kivyao)?

Nadhani uzumbukuku usio na uti wa mgongo ni ule wa kudhania kwamba watanzania wataendelea kuwa wajinga wa kutawaliwa na mfumo kiini macho ambao pamoja na ukweli kwamba hata jaji warioba alikuwa mfuasi wa mfumo huu hata akiwa mwanasheria mkuu wa serikali, miaka 50 baadae kaona kiini macho husika, ingawa yeye anaujadili kama "koti".

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hoja kwamba serikali tatu zitavunja muungano ni hoja za ovyo sana kuwatisha wananchi;muungano ni wa wananchi, na iwapo kwa wingi wao wa 64% wamependelea mfumo wa serikali tatu, ni dhahiri kwamba wao ndio watakuwa ni walinzi wa mfumo huo. Vinginevyo walinzi wa mfumo wa kulazimisha kama wa sasa wa serikali mbili ni vyombo vya ulinzi na usalama.

Wenye hoja ya serikali moja - hiyo ndio njia ya haraka zaidi ya kuvunja muungano kwani the union question has always been the zanzibar question, hasa juu ya her sovereignty.

Hakuna mfumo ambao ni practical kuliko serikali tatu na tumeshajadili sana juu ya hili. Serikali mbili imekuwa ikilindwa na vyombo vya ulinzi na usalama badala ya wananchi, na serikali moja ni kama nilvyojadili hapa and elsewhere.

Ni muhimu tusijichanganye na hoja za marais wangapi kwani hapa, urais sio suala la msingi. Suala la msingi ni nchi shiriki kuwa na mamlaka ya kujiamulia masuala yake na pia kuwa na usawa katika kuchangia uendeshaji wa muungano.

Mwisho, suala la gharama za serikali tatu linajadiliwa kisiasa zaidi kuliko kiuchumi. Tumejadili sana juu ya ufinyu wa gharama utakaokuja baada ya adoption ya serikali tatu lakini kwa vile siasa has become supreme to kila kitu including common sense and rationality, wahusika wamekuwa ni mabingwa wa kutojibu hoja zetu.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Marekani wana serikali 53, 52 za states na 1 serikali kuu. Kila state ina mtawala mwenye mamlaka kamili, katiba inayoongoza state, senator, congress na bendera yake. Wana bajeti yao na kuna baadhi ya shughuli za uchumi katika kodi kuchangia serikali kuu. Kama hao wameweza nchi moja kuwa na serikali 53, kwa nini tushindwe kuwa na serikali tatu?

UK nako wana serikali kadhaa ikiwemo ile ya Scotland, Ireland, na England.

Miaka nenda rudi wanaendesha shughuli zao vizuri tu na wameweka taratibu ambazo hazileti migongano na mambo ni poa kabisa, nini tatizo wabongo tushindwe wakati Zanzibar tayari wameshafanikiwa na tumebaki watanganyika tu?

Kwa hiyo Zanzibar na Tanganyika zitakuwa majimbo? Jimbo la Zanzibar litakuwa na gavana wake, bunge lake, mahakama yake, mamlaka yake ya mapato, nk? Na jimbo la Tanganyika litakuwa na gavana wake, bunge lake, mahakama yake, na mamlaka yake ya mapato?

Halafu tutakuwa na serikali kuu (ya Tanzania) yenye rais, makamu wa rais, baraza la mawaziri, bunge, mahakama, mamlaka ya mapato, na kadhalika?
 
Back
Top Bottom