Prof. Kabudi afafanua serikali tatu katika Jenerali on Monday

Prof. Kabudi afafanua serikali tatu katika Jenerali on Monday

Natuanze mchakato wa katiba yetu ya Tanganyika mapema. Hatutaki Vodafasta! Zanzibar wanayoyakwao sisi yetu imepitwa na wakati toka mkoloni.
 
Kwa hiyo Zanzibar na Tanganyika zitakuwa majimbo? Jimbo la Zanzibar litakuwa na gavana wake, bunge lake, mahakama yake, mamlaka yake ya mapato, nk? Na jimbo la Tanganyika litakuwa na gavana wake, bunge lake, mahakama yake, na mamlaka yake ya mapato?

Halafu tutakuwa na serikali kuu (ya Tanzania) yenye rais, makamu wa rais, baraza la mawaziri, bunge, mahakama, mamlaka ya mapato, na kadhalika?

Kifupi swali lako limeshajibiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambayo ina kiongozi wa juu mwenye mamlaka kamili, katiba, bunge, wizara, nk. Sasa bado tu kuunda katiba ya Tanganyika kwa utaratibu huo huo wa Zanzibar.

Maana yake ndio hiyo, ingawa utaratibu wa mfumo wenye serikali tatu unaweza ukawa tofauti, mfano kama UK na USA ingawa nchi zina serikali kadhaa lakini mifumo ni tofauti.

Zanzibar wana Katiba, yao, bunge lao, hali kadhalika wizara zao, tatizo nini kwa Tanganyika kuwa na zao kisha zikawa hazina mamlaka kimataifa ila serikali kuu ya Tanzania?
 
Marekani wana serikali 53, 52 za states na 1 serikali kuu. Kila state ina mtawala mwenye mamlaka kamili, katiba inayoongoza state, senator, congress na bendera yake. Wana bajeti yao na kuna baadhi ya shughuli za uchumi katika kodi kuchangia serikali kuu. Kama hao wameweza nchi moja kuwa na serikali 53, kwa nini tushindwe kuwa na serikali tatu?

UK nako wana serikali kadhaa ikiwemo ile ya Scotland, Ireland, na England.

Miaka nenda rudi wanaendesha shughuli zao vizuri tu na wameweka taratibu ambazo hazileti migongano na mambo ni poa kabisa, nini tatizo wabongo tushindwe wakati Zanzibar tayari wameshafanikiwa na tumebaki watanganyika tu?

Mkuu,

Naomba kukurekebisha kidogo kuhusu haya masuala ya states au majimbo na country au province ambayo ni sehemu ya nchi husika.

Wamarekani wao waliamua kuwa na majimbo hayo 53 ni majimbo au states na kila jimbo ndio lina gavana wake. Kuna baadhi ya mambo fulanifulani kama vile hukumu za kifo kwa majimbo kama Texas wana sheria yao kwamba mtu akiua lazima ahukumiwe kifo cha kudungwa shindano.

Hii habari ya UK na Ireland au England ni tofauti kidogo.

Ireland ni nchi kamili husika na inajitegemea labda ulimaanisha Northern Ireland ambayo ni sehemu ya Uingereza na ni wananchi wa kiprotestant ndio waliotaka kuwa sehemu ya Uingereza na kuachana na wale wale Ireland ya kusini ambayo leo hii ni jamhuri ya Ireland ambayo ina raisi wake na waziri mkuu.

Lakini ugomvi upo mpaka leo wa wale wakatoliki kukataa kuwa chini ya Uingereza na kutaka nchi yao kamili kama wenzao wa Ireland wanavyofaidi.

Sheria ilitungwa bungeni kabisa mwaka 1949 kutohalalisha kujitenga kwa sehemu hiyo bila ya ridhaa ya wananchi walio wengi. Hivyo hadi leo sehemu hiyo ni moja ya nchi zinazounda Uingereza.

Northern Ireland hawana serikali kule Belfast ina wana wabunge wanaowakilisha mawazo bungeni yasiyo ya kitaifa na wana wawakilishi wao Bunge la kitaifa pale Westminster.

Scottland tunaweza kuichukulia kama ni Zanzibar ambao ni nchi kabisa (na sio jimbo au state) ambayo ni sehemu ya Uingereza.

Hii ni nchi ilokuwa ufalme ambayo hapo kabla iliungana na ufalme wa Uingereza, muungano uloitwa Personal Union na baadae ikaja kuwa Political Union ulopelekea kuwepo kwa United Kingdom of Great Britain.

Lakini muungano huu haukuja tu bali ni kutokana na makubaliano ya muungano au Treaty of Union ambayo yalibeba kila moja ya hati yaani Acts of Union kutoka Scottland na kutoka Kingdom of England na kujadiliwa na mabunge ya nchi zote hizo ( Scottland, Northern Ireland na Kingdom of Great Britain)kisha kupitisha sheria inayotambua nchi moja ya United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland.

Scottland sasa hivi inataka kupiga kura kukubali rasimu ya kujitenga na Uingereza na kubakia kuwa Scottland kama Jamhuri na upigaji kura utafanyika mwezi September mwaka huu.

Moja ya sababu kubwa ya kutaka kujitenga na kuwa nchi ianyojitegemea kivyake ni kwamba wanataka kufuta ile Act of Union na kuleta kitu inaitwa Federalism yaani ushiriki na hiyo itakuwa federal government.

Hivyo kwetu sisi watanganyika, hoja ya serikali tatu haina uzito kwa kuzingatia kwamba Serikali ni moja ya Muungano na ile ya Zanzibar inakuwa serikali inayojitegemea huku ikishiriki mambo kadhaa ya kitaifa kwenye masuala ambayo yanajulikana ikiwa federal government.

Sidhani kama suala la serikali tatu litapata upenyo ndani ya Bunge isipokuwa ni ushindi wa CCM kiufundi katika kufanya kampeni kwani watasema walijitahidi kila kitu na kina Fulani tu ndo walokuwa wakishika mabango ya serikali tatu.
 
Kifupi swali lako limeshajibiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambayo ina kiongozi wa juu mwenye mamlaka kamili, katiba, bunge, wizara, nk. Sasa bado tu kuunda katiba ya Tanganyika kwa utaratibu huo huo wa Zanzibar.

Maana yake ndio hiyo, ingawa utaratibu wa mfumo wenye serikali tatu unaweza ukawa tofauti, mfano kama UK na USA ingawa nchi zina serikali kadhaa lakini mifumo ni tofauti.

Zanzibar wana Katiba, yao, bunge lao, hali kadhalika wizara zao, tatizo nini kwa Tanganyika kuwa na zao kisha zikawa hazina mamlaka kimataifa ila serikali kuu ya Tanzania?

Hivi ni lazima kuwa na huo muungano?
 
I am just thinking aloud: 1. Hilo shirikisho litakapokufa au kuvunjika (kwani hakuna muungano usioweza kuvunjika, hata ndoa huvunjika) hayo majeshi na vifaa vyake vya kivita tutagawana vipi? Kama ni nusu kwa nusu basi Wazenji watakuwa wametufanzia. 2. Sisi wabara jina la Tanganyika tulipewa na Waingereza wakiimanisha Tanga na Nyika. Kabla ya hapo Wajerumani walitupa jina la Ostoafrica. Jina la Tanganyika tulilizika baada ya Muungano. Sasa baada ya Muungano kufa na kuanzishwa hilo shirikisho nani kampa madaraka Waryoba ya kutaka turudie jina la Tanganyika? Kwa nini tusichague jina tunalopenda kuitwa? Nchi nyingi ziliachana na majina waliyopewa na wakoloni k.m. Nyasaland ikajiita Malawi, North Rhodesia ikawa Zambia, South Rhodesia ikawa Zimbabwe na kadhalika. Hii itakuwa ni fursa kwetu kujiita jina tutakalopenda. Napendekeza tuwe " East African Republic". Hii ni tofauti na jumuiya ya Africa Mashariki. Hii itakuwa kama Russia na Soviet Union of Russia. Soviet Union ilipokufa Russia inaendelea. Hivyo na jumuiya ya Africa Mashariki itakapokufa East Africa yetu itaendelea kubeba jina hilo. 3. Hivi kweli kero za Muungano ndizo zitaondolewa na Shirikisho au ndipo zitaongezeka? Kwani kupunguza mambo ya muungano na yakabaki kama matatu tu hivi (yale ya muhimu kama ulinzi na mambo ya nje) hakungemaliza kero hizo? 4. Rais wa bara ikulu yake itakuwa wapi? 5. Bendera, nembo na wimbo wa serikali ya bara umeshatayarishwa na tumeukubali? 6. Si shirikisho lisubiri kwanza hadi tutakapokuwa tumeunda serikali ya bara. 7. Hivi kweli Waryoba hakukurupuka kufanya mambo ambayo hakuwa ametumwa hivyo ku complicate the whole issue. Hayo mambo ya shirikisho yalikuwa ya kuwekewa kipengele kidogo tu ambacho kingetekelezwa baadaye kwa utaratibu wa kibunge. Au ni kutaka sifa na kuweka historia kuwa Tanganyika ilirejeshwa na Waryoba?
 
Serikali moja haiwezekani
serikali mbili ni kurudi kwenye matope baada ya kukaribia kutakakta
 
Mkuu nimeona kinachokusumbua ni kuacha kuwaza in big picture na kuwaza vitu vidogo. Kama Tanganyika na Zanzbar zitaitwa nchi,majimbo,kata,wilaya au mikoa hilo ni jambo dogo kujadili. Kama viongozi wake wataitwa marais,maseneta,makansela,wenyekiti nk hiyo sio issue. Mambo ya kuwaza ni madaraka,haki na wajibu wa kila sehemu.Nimeona wewe ni wale wanaoweza kukataa kuajiliwa kampuni au shirika flani sababu cheo hakina jina MANAGER mwishoni!.Kiongozi mkuu wa ujerumani anaitwa Kansela,haitwi rais!,viongozi wa majimbo yote marekani wanaitwa maseneta na si marais!.Sisi tukitaka tunaweza kusema tutakua na mawaziri wakuu wawili,tanganyika na zanzbar,kisha tutakua na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ambae ni amiri jeshi mkuu.Tubadilike ki fikra
Kwa hiyo Zanzibar na Tanganyika zitakuwa majimbo? Jimbo la Zanzibar litakuwa na gavana wake, bunge lake, mahakama yake, mamlaka yake ya mapato, nk? Na jimbo la Tanganyika litakuwa na gavana wake, bunge lake, mahakama yake, na mamlaka yake ya mapato?

Halafu tutakuwa na serikali kuu (ya Tanzania) yenye rais, makamu wa rais, baraza la mawaziri, bunge, mahakama, mamlaka ya mapato, na kadhalika?
 
Mimi sijui nipoje.hawa maprofesa watz huwa siwaelewi kabsaaa...

Binafsi naamini katika "NCHI MOJA, WATU WAMOJA, SERIKALI MOJA" Hayo mambo ya serikali 3 yanatoka wapi!?!? watz hebu tuache kujitoa ufahamu. Prof Kabudi i salute you kama best Tanzanian graduate katika field ya sheria. Mambo gani hayo unafanya

61% ya wachangiaji wametaka hivyo
 
Anaendelea na kipindi now. Anasema baadhi ya watu wanaona serikali mbili kama ushirikina au dogma ya kila kitu katika tanzania kitu ambacho sio sahihi


Wakati Mzee Warioba anawasilisha taarifa ya Tume, baadhi yetu tulijsahaulisha kuwa Warioba amezungukwa na nguli wa sheria akiwamo Prof. Kabudi, Mzee Salim Ahmed Salim na wengine kutaja wachache. Hata hivyo bado nina hofu endapo serikali ya CCM itaridhia mapendekezo haya maana tuna historia mbaya ya mapendekezo ghali yaliyotolewa na tume za kijaji kuishia kwenye makabrasha...Tusubiri tuone
 
Serikali tatu ni wazo la kijinga sijapata kuona!!

Na kama tukikubali muundo wa hivyo tutakuwa mazumbukuku tusio na uti wa mgongo!!

Kumbe kweli Nyani Ngabu hujarogwa kama ulivyotangaza hakuna mchawi wa kukuroga, yaani umeweza kuwa na mawazo mazuri kama ya kwangu. Niliwahi kusema kama hivi hapa JF nikatumiwa PM na MJINGA mmoja.
 
kumbe kweli nyani ngabu hujarogwa kama ulivyotangaza hakuna mchawi wa kukuroga, yaani umeweza kuwa na mawazo mazuri kama ya kwangu. Niliwahi kusema kama hivi hapa jf nikatumiwa pm na mjinga mmoja.

anaeamini serikali 3 sidhani kama yupo sawa kichwani...
 
Let's regain our sanity and stop this nightmare!: Serikali 3 haziwezekani. Z'bar wanadai mamlaka kamili. Na kwa jinsi tulivyo (TZ & ZBAR), siamini kama tutaweza kutenganisha mamlaka juu ya vyombo vya dola na masuala ya fedha na uchumi. Haitakuwa busara baadaye kusikia wengine wanaanzisha aina nyingine za KMKM n.k. Kama tumeshindwa serikali moja (ambayo kwangu mimi ndiyo kipimo pekee cha dhamira ya dhati ya kutaka muungano), basi tukubaliane kuwa na nchi zetu mbili tofauti zenye serikali zenye madaraka kamili kisha tujadili mkataba wa ushirikiano hasa kwa vile kumekuwa na muingiliano mkubwa sana wa kiraia na kiuchumi miongoni mwa wananchi wa nchi zetu mbili (sijui ndio kile wengine wanadai muungano wa mkataba?).
 
Twende tukishindwa tutarudi, tulipofika hatukuwa tumeshindwa ila tamaaa za wachache wapenda madaraka na sifa.
 
Serikali tatu ni hazikwepeki miaka 50 tayari tumeshindwa kutatua kero za mungano,warioba ametoa ufafanuzi mzuri na wa hali ya juu hata na wala haitaki uwe na digirii hata kama hukusoma unafaham fika kwamba Tanganyika imevaa joho la Mungano na kujifanya yeye ni mungano na baraza la mawaziri la mungano linawajibika kwa tanganyika na sio kwa taifa lote wakati wakijua kuwa serikali ya mungano kwa taifa zima,serikali ya mungano inapotafuta wafadhili na misaada kwa ajili ya tanganyika na hawafanyi kwa taifa zima,kamati za bunge hazijatembelea zanzibar kutembelea miradi ya maendeleo ya serikali ya jamuhuri wa Mungano tanzania,serikali ya tanganyika ipo imejificha tunataka isijifiche ikae hadharani
 
Back
Top Bottom