Marekani wana serikali 53, 52 za states na 1 serikali kuu. Kila state ina mtawala mwenye mamlaka kamili, katiba inayoongoza state, senator, congress na bendera yake. Wana bajeti yao na kuna baadhi ya shughuli za uchumi katika kodi kuchangia serikali kuu. Kama hao wameweza nchi moja kuwa na serikali 53, kwa nini tushindwe kuwa na serikali tatu?
UK nako wana serikali kadhaa ikiwemo ile ya Scotland, Ireland, na England.
Miaka nenda rudi wanaendesha shughuli zao vizuri tu na wameweka taratibu ambazo hazileti migongano na mambo ni poa kabisa, nini tatizo wabongo tushindwe wakati Zanzibar tayari wameshafanikiwa na tumebaki watanganyika tu?
Mkuu,
Naomba kukurekebisha kidogo kuhusu haya masuala ya states au majimbo na country au province ambayo ni sehemu ya nchi husika.
Wamarekani wao waliamua kuwa na majimbo hayo 53 ni majimbo au states na kila jimbo ndio lina gavana wake. Kuna baadhi ya mambo fulanifulani kama vile hukumu za kifo kwa majimbo kama Texas wana sheria yao kwamba mtu akiua lazima ahukumiwe kifo cha kudungwa shindano.
Hii habari ya UK na Ireland au England ni tofauti kidogo.
Ireland ni nchi kamili husika na inajitegemea labda ulimaanisha Northern Ireland ambayo ni sehemu ya Uingereza na ni wananchi wa kiprotestant ndio waliotaka kuwa sehemu ya Uingereza na kuachana na wale wale Ireland ya kusini ambayo leo hii ni jamhuri ya Ireland ambayo ina raisi wake na waziri mkuu.
Lakini ugomvi upo mpaka leo wa wale wakatoliki kukataa kuwa chini ya Uingereza na kutaka nchi yao kamili kama wenzao wa Ireland wanavyofaidi.
Sheria ilitungwa bungeni kabisa mwaka 1949 kutohalalisha kujitenga kwa sehemu hiyo bila ya ridhaa ya wananchi walio wengi. Hivyo hadi leo sehemu hiyo ni moja ya nchi zinazounda Uingereza.
Northern Ireland hawana serikali kule Belfast ina wana wabunge wanaowakilisha mawazo bungeni yasiyo ya kitaifa na wana wawakilishi wao Bunge la kitaifa pale Westminster.
Scottland tunaweza kuichukulia kama ni Zanzibar ambao ni nchi kabisa (na sio jimbo au state) ambayo ni sehemu ya Uingereza.
Hii ni nchi ilokuwa ufalme ambayo hapo kabla iliungana na ufalme wa Uingereza, muungano uloitwa Personal Union na baadae ikaja kuwa Political Union ulopelekea kuwepo kwa United Kingdom of Great Britain.
Lakini muungano huu haukuja tu bali ni kutokana na makubaliano ya muungano au Treaty of Union ambayo yalibeba kila moja ya hati yaani Acts of Union kutoka Scottland na kutoka Kingdom of England na kujadiliwa na mabunge ya nchi zote hizo ( Scottland, Northern Ireland na Kingdom of Great Britain)kisha kupitisha sheria inayotambua nchi moja ya United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland.
Scottland sasa hivi inataka kupiga kura kukubali rasimu ya kujitenga na Uingereza na kubakia kuwa Scottland kama Jamhuri na upigaji kura utafanyika mwezi September mwaka huu.
Moja ya sababu kubwa ya kutaka kujitenga na kuwa nchi ianyojitegemea kivyake ni kwamba wanataka kufuta ile Act of Union na kuleta kitu inaitwa Federalism yaani ushiriki na hiyo itakuwa federal government.
Hivyo kwetu sisi watanganyika, hoja ya serikali tatu haina uzito kwa kuzingatia kwamba Serikali ni moja ya Muungano na ile ya Zanzibar inakuwa serikali inayojitegemea huku ikishiriki mambo kadhaa ya kitaifa kwenye masuala ambayo yanajulikana ikiwa federal government.
Sidhani kama suala la serikali tatu litapata upenyo ndani ya Bunge isipokuwa ni ushindi wa CCM kiufundi katika kufanya kampeni kwani watasema walijitahidi kila kitu na kina Fulani tu ndo walokuwa wakishika mabango ya serikali tatu.