Prof. Kabudi ahudhuria hafla ya uzinduzi ripoti ya BBI nchini Kenya inayopendekeza uwepo wa cheo cha Waziri Mkuu na Kiongozi wa Upinzani Bungeni

Well said mkuu! 100% true

na ndio hasa kinachoendelea humu,membe hakuvunja kikosi chake yeye na uncle wake.
wale vijana waliokuwa wakishindana kuweka likes wakati wa mchuano wa ndani wa ccm,wenzake waliyavunjilia mbali baada ya uteuzi kukamilika ila huyu alikuwa na bado ana ndoto za kuukwaa urais.

sasa vijana wzke wanafanya attack kwa kila mtu ndani ya ccm anayeonekana ku fit na kuifanya taswira ya JPM iimarike.
basi huyo anaundiwa section humu JF.

ukiongeza na hawa wengine wa makundi ya mbowe na zitto na wale wadada wakosa fursa kina sarungi na Fyatu basi inakuwa shida kabisa ujinga ukinga ujinga.
 
Badala ya kuwaponda wakenya alitakiwa kuwapongeza kwa kuwa mfano wa kuigwa Africa na Tanzania pia.
Unataka kuiga nini kwenye siasa za Kenya?
Kuua wanaokatalia password ya kuchakachulia matokeo ya kura?
Unajua Chriss Msando aliko?
Nyie watu waajabu sana, Mnaropokaropoka tu mambo msiyoyajua
 
Mkuu kwa uhakika kabisa hakuna kiongozi wa kenya amemtaja kiongozi wa awamu ya 5 wa Tanzania kama mfano wa kuigwa.

Nyerere katajwa

Mkapa.katajwa

Kikwete katajwa

Jiulize.awamu ya tano kuna tatizo gani?

Hatumchukii prof kabudi tuna mchukia prof kabudi mchumia tumbo.

Huyu anakaa kwenye baraza la mawaziri kupanga kuharibu uchaguzi wa serikali za mitaa na leo.mmesikia eti hii ndio demokrasia.
Kwa taarifa yako BBI was not on tribalism... BBI inataka kuifanya kenya iendelee mbele baada ya kutambua demokrasia ndio njia sahihi ya maendeleo.
Tanzania inahitajika BBI kwa sababu tunako elekea tunaenda kufunga ndoa na burundi.
 
Profesa kasema kweli kuhusu hali yetu wakenya anayetoa ushauri sio lazima awe malaika. La busara ni kupashana ukweli
 
Nchi inayojinasibu ya kidemokrasia kama Kenya inaingia kwenye chaguzi na mandate ya viongozi wa kikabila kuungana ili kushawishi kura; badala ya utaratibu wa kunadi sera za chama na mgombea sahihi anaekubalika na wote.

Hawa kweli ndio wa kuifananisha na Tanzania

Hila Kabudi lazima ajifunze speech language he is too direct, msomi wa sheria at Phd level ajui achague maneno gani ya kutumia kutokana na hadhara husika.

It’s official diplomatic lexicon is a major problem for Kabudi.
 
the truecaller, Matatizo ya Tanzania ni makubwa kulikoya kenya

Acha kujifariji

Kenya ndio nchi pekee africa mashariki yenye demokrasia wakati Tanzania bado imelala na chama kimoja.

Ukabila Tanzania unarudi taratibu nadhani tunaelekea kufunga ndoa na Burundi.
 
Kizungumkuti ambacho kilisababisha Raila ajiapishe ni mfumo wa kisiasa wa 'winner takes it all'. Yaani mshindi kwenye uchaguzi wa urais huwa anakula minofu yote, wali na kachumbari pia, huku walioshindwa wakimezea mate kwa umbali.

Jambo ambalo ni hatari kwenye siasa za nchi kama Kenya ambapo anayeshinda kwenye uchaguzi huwa unafanya hivyo kwa margin ndogo. K.m, U.Kenyatta 50.3% R.Odinga 44%. Alafu juu yake cheo cha zamani cha kiongozi rasmi wa upinzani kilipunguzwa uzito na wagombea urais nao pia sio wabunge. Kumaanisha baada ya uchaguzi, walioshindwa na asilimia kubwa ya Wakenya, wafuasi wao, huwa wanatupwa kwenye kaburi la sahau kisiasa.

Hebu soma hii taarifa ya mwanasiasa Shahbal wa Mombasa ambaye alipata 44% ya kura zote ila akashindwa kwenye uchaguzi na gavana Ali Hassan 'Sultani' Joho.
 
Twende mbele turudi nyuma Prof ni mbaya kwa Kiswahili, hii lugha ni nzuri licha ya vijana wengi kuichukulia poa. Kama kuna mtu ana Mlaumu Prof jinsi aluvyoongea Kenya basi hao ni wale wameasilika na mambo ya Kenya, ushauri unaweza pewa hata na mtu wa kawaida ni wewe kuukubali au kukataa.
 
Tabutupu,
UPOTOSHAJI ULIOKITHIRI.

Haya uliyoyaandika ni kinyume kabisa na kilichotokea. Ukweli ni kwamba Hotuba ya Prof. Kabudi ndiyo iliyoshangiliwa kuzidi Hotuba zote na hivyo kuiinua dhana nzima ya BBI pale Bomas of Kenya. Ni Hotuba iliyotukuka.

Prof. Kabudi amewatendea haki sio wakenya pekee bali Watanzania na wananchi wote wa Afrika Mashariki. Hotuba yake imekuwa gumzo hata BBC kutokana na ufanisi wake.

Yawezekana una chuki binafsi dhidi ya Prof. Kabudi. Weka akiba, tafuta sababu nyingine ya kumlaumu; kwa Hotuba yake ya leo, hautaeleweka. Unajidhalilisha.
 
Hakuna uharaka wa kufanya haya mambo. Kama sisi ilikuwa kwa nadharia wao wakafanya kwa vitendo haraka haraka, ni jambo jema maana tunaona makosa yaliyomo kwenye nadharia kama yapo, na kuweza kurekebishwa kabla ya kufanywa.

Sio lazima kila kitu kitokee sisi tukione, tukiweka njia nzuri basi hata vizazi vijavyo vitafanya tu.
 
Tabutupu,
Wakenya ni watani zetu, kusema chochote ni ruksa. Lakini ujumbe wa Prof ulikuwa mzito.

Kawashikisha mikono huku wakiwa na shangwe mwanzo mwisho.
Mihemuko yako pia inakuponza
 
Tony254,

Proff ameliweza jukwaa, kongole kwake, amefanya jambo la maana sana kwakweli, pia ameiva sana lugha, zote yuko sawa.
Hata wewe Kiswahili chako hua kingumu saa zingine ...kwa nyuzi mingi huwa unachangia maneno chache but kila saa lazima some few words niangalie kwa kamusi[emoji1787][emoji1787]heko bro
 
Nimeipenda speech yake, kaongea kutoka moyoni
 
Mimi nimemnukuu tu. Ubishi wa kitoto ni kama huu hapa chini, wa kuingiza hadithi za ndoa na padre kwenye 'gethering' ya kujadili mambo ya maana.
"Kenya is endowed with dynamic people, innovators, people filled with talents and entrepreneurs."
Hayo hapo maneno ya waziri wao...
 
Tabutupu,



Waziri Kabudi anawanyima usingizii kweli kweli mbona walimpigia makofi! Mimi binafsi siwaamini wakenya hata watambike lakini sikuona ambacho Waziri Kabudi alifanya cha kutia aibu.

NB: Nafahamu kwa nini mnamchukia: Amesoma na kuwazidi hivyo mnamwonea wivu. Hizo ndio baadhi ya tabia za watu ambao elimu zao ni duni.
 
Mungu anisamehe kwa kukomenti bila kujitidhisha, Kabudi katoa speech nzuri sana na smrongea maneno ya kweli yanayojenga.
Magufuli stuka chuki hii inapofusha hata kuzuia kuona mazuri madogo
 
Reactions: Ole
Mungu anisamehe kwa kukomenti bila kujitidhisha, Kabudi katoa speech nzuri sana na smrongea maneno ya kweli yanayojenga.
Magufuli stuka chuki hii inapofusha hata kuzuia kuona mazuri madogo
 
Reactions: Ole
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…