Prof. Kabudi aibuka. Aililia tembo kuvamia Mashamba ya Wananchi wa Kilosa
Mbunge wa Kilosa, Profesa Palamagamba Kabudi amesema wananchi wa Jimbo la Kilosa wamekuwa wakipata usumbufu mkubwa kwa tembo kuvamia mashamba na kuharibu mazao na miji ya watu na kwa muda mrefu wananchi hao hawajalipwa kifuta machozi kutokana na uharibifu huo.
Pia, ameomba Wizara ya Maliasili na Utalii kusimamia ili wananchi wake walipwe kifuta machozi chao.
Kabudi amesema hay oleo Jumatatu Juni 5, 2023 alipokuwa akichangia mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha 2023/2024, bungeni jijini Dodoma.