Prof. Kabudi aieleza Jumuiya ya Kimataifa kuwa Tanzania haijawahi kushindwa vita ya aina yoyote

Kabudi Tumeporwa kifaru na waasi wa ISS huko mpakani na msumbiji, askari wetu kwa mamia wanakufa na wengine wanamejeruhiwa,
Kuna Hatari ya kuipoteza mtwara na Lindi, acha porojo na vitisho

Sasa unaeleza mafanikio ya JWTz ili kuwatisha EU wakati ndo wanalivalisha kulilisha na kulipa siraha jeshi lenu
 
Duh! Watu wengine ni hatari "kujimwabafy".
 
Wewe jamaa ni mjinga sana. Nadhani wewe ni kijana ila una akili ya babu kizee wa enzi za ukoloni.
Mkuu hii demokrasia mnayoihubiri ipo wapi sasa kama unanitukana kwa kuusema msimamo wangu.... [emoji3][emoji3] msimamo wangu unakuumizaje sasa mkuu unaye hubiri haki na amani?

Wewe ungekuwa kiongozi tayari ungeshanikamata kwa kesi ya utakatishaji.....
 
Boss, tambo lazima ziwepo unapoingia ulingoni😂😂
 
Kwa uelekeo huu lazima tutapata katiba tunayoitaka watanzania
 
Bunge la ulaya limejadili udanganyifu uliofanyika kwenye uchaguzi. Kabudi badala ya kujibu hoja anaongea vitisho. Wewe unapiga makofi na kumpongeza. Huoni kama ni ujinga huo?
 
Kabudi ni mlevi wa madaraka naona keshashindwa kujibu hoja za hao wanakamati
 
Tuliambiwa na Balozi wetu wa Ubelgiji kuwa hakuna kitu kama Mjadala wa Kamati ya Mambo ya nje ya EU illiyotuongelea - eti ni uongo tu. Sasa waziri wetu naye amejibu kisichokuwepo au?

Nani mkweli hapa kati ya balozi na waziri?
 
Kwa jinsi unavyo tia huruma kukosa misaada sina shaka kabisa ukipewa uongozi wa nchi nadhani utaendesha nchi kwa misaada aisee

Africa mna kila kitu lakini kwa nini bado mnaendekeza misaada?
Hao Mabeberu wanaitegemea Africa kuendesha viwanda vyao na vyakula toka barani Africa, mbona msijiamini?
Ata wasipotoa misaada lazima waje tu hata kwa mfumo mwingine wa KIBIASHARA na bado Dola zao mnazipata tu,
Magufuli kaonesha kabisa kujiamini na inabidi hata wengine tujiamini na tulicho nacho bhna
Sisi tuna rasilimali kibao na wakisusia Western tutafanya biashara na Mchina wetu bhana asie kuwa na NONGWA kama wengine.
 
Bunge la ulaya limejadili udanganyifu uliofanyika kwenye uchaguzi. Kabudi badala ya kujibu hoja anaongea vitisho. Wewe unapiga makofi na kumpongeza. Huoni kama ni ujinga huo?
Tatizo lako ni moja....

Unataka niwasikilize wabunge wa EU na kuwaelewa kama unavyotaka wewe.

Nimsikilize Kabudi kisha nimwelewe kama unabyotaka wewe. Demokrasia ipi mnahubiri mkuu?

Bado naenda na msimamo wa waziri...utu wa taifa langu unakuja kwanza..
 
Kwamba ni bora kufa ukiwa umesimama,kuliko kuishi ukiwa umepiga magoti.Ila watakaoumia ni maskini. Mawaziri wataendelea kupata mishahara yao minene. Wale wenzangu na mie maisha yataendelea kukaza.
 
Hoja kubwa iliyopo ni kuwa kuna ukiukwaji wa haki katika chaguzi za Tanzania na hii si mara ya kwanza. Hakuna hoja ya vita ya kiuchumi.
Kuna tatizo ambalo Tanzania imelikuza si EU

Wabunge wa Tanzania wanaoongelea EU n.k wana haki kama Wabunge na ndiyo kazi yao.
Wana haki ya kumhoji Waziri wa Mambo ya nje, wana haki ya kusema lolote lile kama Wabunge

Wabunge wa EU wameongelea hoja ya uchaguzi na pesa za COVID-19 ambazo ni zao katika Bunge lao
EU wana haki ya kuongelea suala lao katika Bunge lao.
Hivyo, hilo lipo katika wigo wao halijuvuka na kuingia katika mkondo wa kidiplomasia.

Nimeshangaa Balozi ameomba kuzungumza na viongozi wa Bunge! kwa tatizo gani?
Hili suala halijaingia katika mzunguko wa diplomasia, na wala hakuna Diplomatic Row au statement ya EU.

Waziri anapoongea anali ingiza suala katika mkondo wa kidiplomasia na kauli yake ni ya kidiplomasia.
Hapa ndipo tatizo linapoanza, kwamba, waziri anachochea mgogoro ambao haupo kwa kuanzia

Wabunge wa EU wanaoongea kwanini kuna panic Tanzania?
Hatuwezi kuwapangia Wabunge wa EU nini cha kuongea

JokaKuu Mag3
 
Kama hayo yametamkwa na Kabudi, basi ana muda mfupi sana wa kukaa kwenye hiyo Wizara... Nina hakika atapumzishwa soon. Ngoja hizo kauli ziwafikie mabeberu..
 
Kuwa Nchi Huru sio kigezo Cha kukiuka haki za binadamu au kuvunja Katiba.

Aidha, kuwa Nchi Huru ni suala moja. Kuwa Nchi ya inayohejiheshimu na kuhfpeshimu utawala wa sheria ni suala jingine. Sisi ni Nchi Huru Ila tumeshindwa kujiheshimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…