Prof. Kabudi aieleza Jumuiya ya Kimataifa kuwa Tanzania haijawahi kushindwa vita ya aina yoyote

Prof. Kabudi aieleza Jumuiya ya Kimataifa kuwa Tanzania haijawahi kushindwa vita ya aina yoyote

Kabugi anatangaza vita yeye kama nani? .... tulitegemea haya yatamkwe na mkuu mwenyewe!
NB: Their role model, Mwalimu, could not do the same today! ... ROBOTS 🤖👾🤖😳
 
It is much easier to win the war than peace - Georges Clemenceau.

Georges Clemenceau, Premier of France, Far-Seeing Statesman, Indomitable Leader and , Eloquent Orator. Georges Clemenceau (1841‒1929) served France as prime minister several times.

(1) Georges Clemenceau, L'Homme Libre (4th June 1914)​

When I am told that we should live in peace with our neighbours, I agree, but let us not forget that it needs two to make peace. The great mistake of the revolutionary Socialists is to think themselves superior to the rest of mankind because they are not prepared to bend their ideology before the irreducible realities of human nature
 
Kimsingi, watu mmoja mmoja na hata serikali wana UHURU wa kutenda mema, lakini hawako HURU kutenda mabaya. Kwa mfano, miaka ya 1960 -1995, sovereign state ya Africa ya Kusini haikuwa na UHURU wa kuendekeza apartheid. Na Tanzania tuliishutumu sana.

Kimsingi, nchi ina haki ya kukataa kufanya kosa, lakini haina HAKI ya kutokosolewa. Alichopashwa kufanya Waziri Kabudi ni kukataa kwamba tumekosa (kama hilo linawezekana) na sio kuchachamaa eti sisi ni sovereign country na hivyo hatupashwi kukosolewa.

Mwalimu alikataa masharti, hakukataa kukosolewa. Ni kumkosea haki Mwalimu kama tutalinganisha kukosolewa kwa wizi wa kura na kupangiwa foreign policy yetu iweje.

Bunge la EU lina UHURU wa kutukosoa. Kama madai yao sio kweli, basi Waziri aliyetulia hujibu kwa kuonyesha ni kwa namna gani madai yao sio ya kweli. Kuonyesha GHADHABU tu kama alivyofanya Waziri Kabudi ni diplomatic immaturity.

Uchaguzi umefanyika, Kabudi na sisi sote tunajua kwamba CCM iliiba kura, na kwamba waliotaka kupinga wizi huo kwa kuandamana wamepachikwa kosa la ugaidi.

Mtazamo wa Waziri Kabudi kwamba sisi ni taifa huru kwa hivyo EU na dunia nzima hakuna kukemea hilo ni ujinga kupita maelezo.
 
1965 alichokataa Nyerere sio kuhusu haki za binadamu wala demokrasia. Kinachotupiga leo ni uvunjifu wa misingi ya binaadamu. Pia kwa ushindani hata wa kikanda tunajichimbia kaburi kubwa.
Halafu kutoa mimacho , kufoka na kurusha mimate haisaidii hapa. Nimeona ujinga tu na comedy. Afadhali sikufundishwa na hii takataka.
Turudishe misingi yetu.
 
Saturday, November 21, 2020
Dodoma, Tanzania

PROF. KABUDI : TUTASHIRIKIANA NA TAIFA LOLOTE LINALOIHESHIMU TANZANIA​

1606014084762.png


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amesema Tanzania itashirikiana na nchi yoyote duniani ambayo inatambua na kuheshimu Uhuru wa nchi na utu wa watu wake.


Prof. Kabudi ametoa kauli hiyo jijini Dodoma alipozungumza na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na taasisi zake tangu alipoteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuwa Waziri wa Mambo ya Nje.

"Tutafanya kazi na nchi zote ambazo zinatuheshimu, zinatutambua kama Taifa huru, kutuheshimu sisi kama binadamu wa mataifa mengine, hatutakubali kudharauliwa, kutokuheshimiwa utu wetu na kudharauliwa kwa sababu ya misaada au pesa’, amesema Prof. Kabudi

Ameongeza kuwa Tanzania itasikiliza taifa lolote duniani na kujadiliana nalo kwa heshima kwani mapungufu hayapo upande mmoja tu.

"Tuko tayari kuwasikiliza na kujadiliana nao kwa heshima na kama wanadhani kuna kitu kimepungua kwetu na sisi tunadhani kimepungua kwao," amesema Prof. Kabudi.

Amesema Tanzania haiwezi kumruhusu mtu yeyote atumie misaada ya fedha kuondoa uhuru wetu na kutokuthamini utu wetu.

Amesema Tanzania haiwezi kujitenga kama kisiwa na itaendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali za kidunia kama vile kulinda amani, kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kutunza mazingira.

"Hatutajitenga katika dunia hii, tutaendelea kujumuika katika kazi mbalimbali kama vile ulinzi wa amani, kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuhifadhi mazingira,’ alisema na kuongeza kuwa tumekuwa bandari ya amani kwa wakimbizi sio tu kutoka Afrika bali duniani kote na tutaendelea kuwa hivyo," Ameongeza Prof. Kabudi.

Prof. kabudi pia amewataka watumishi wa Wizara kusoma kitabu cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alichowaandikia watumishi wa wizara hiyo mwaka 1969 cha Usipayuke toa hoja ‘Don’t shout argue’ ili kutoa takwimu sahihi kwa wakati.

Amesema jukumu la kuieleza dunia kuhusu takwimu za vitu mbalimbali ni la watumishi wa Mambo ya Nje na hawana budi kuhakikisha wanaliekeleza hilo kwa ufasaha.

Mbali na kitabu hicho, Prof. Kabudi amewakabidhi wakurugenzi wa Idara mbalimbali Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), hotuba za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli wakati anafungu Bunge la 11 na hotuba ya ufunguzi wa Bunge la 12 na kuwataka kusimamia na kutekeleza maagizo yote yaliyopo kwenye hotuba hizo pamoja na maelekezo ya Ilani ya CCM.

Awali akimkaribisha Waziri kuzungumza na watumishi, Katibu Mkuu Wizara Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wibert Ibuge aliwapongeza watumishi utendaji mzuri wa kazi na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii na uadilifu.
Source: http://foreigntanzania.blogspot.com/2020/11/prof-kabudi-tutashirikiana-na-taifa.
 
mpaka saaa huwa nafikiria, hivi mwaka 2015 ccm ilikosa mgombea mwingine wa urais tofauti na john Magufuli?? kwa sababu huu ujinga wote wa kabudi umeletwa na john magufuli
 
"few hooligans....................." Jamani tukubaliane kuna shida pahala.
 
Uwakumbushe wafanyakazi hao kutembea vifua mbele kwani Tanzania siyo nchi ndogo kidiplomasia, kimsimamo, kiji-Geopolitiki na kiushawishi kimataifa...

HUU NDIO UKWELI. WAZUNGU WAKIPIMA FAIDA NA HASARA WSTACHAGUA FAIDA...

WANAJUWA KABISA WAO WAKISUSA MCHINA NA MRUSI WANAENDELEA KULA
 
Zimejenga hospital na vituo vya afya
Pesa zimetoka septemba na bunge lilikuwa limeshavunjwa,nani kaidhinisha ziende huko?Halafu hakuna hospitali mpya iliyoanza kujengwa septemba!CCM na ufisadi damu damu!
 
Watu wanauana kila kukicha Duniani sio Tanzania tu... na hili mnasababisha wenyewe wapiga mayowe....mnainfluence vijana wasio na hili wala lile na kuwaaminisha yasiyokuwepo.....

Kila serikali Duniani ina dosari zake.....ukiwa na kundi lisilofikiria lkapata viongozi wahemkaji tarajia vifo.

Hoja ya kura ni mfu....ninachojua mimi hata kura ungehesabu wewe JPM angeshinda awamu hii.

Hakuna mwenye tatizo na huyo jpm kushinda, anashindaje hapo ndio tatizo lilipo.
 
Back
Top Bottom