Lazima tuwe na busara, tusiwe watu wa kukurupuka. Ikiwa ni kamati ya mambo ya nchi za nje ya bunge la umoja wa ulaya na lililojadili uchaguzi wa Tanzania na kutolewa michango tena na wajumbe wachache katika kamati hiyo, kumemfanya waziri wetu wa mambo ya nchi za nje kuja na kuwajibu kwa ubabe!
Nadhani hii si hekima na pia si busara, kama hayo yaliyosemwa ndiyo msimamo wa nchi zao na serikali zao hapo tungeweza kujitetea, lakini ni kamati tu ya bunge inajadili jambo kuhusu nchi yako wewe kama waziri unaanza kujimwambafai!
Ikiwa kama nchi ambayo ndiyo kwanza tunaambiwa kuwa tumeingia kwenye uchumi wa kati na tuna safari ndefu ya kuufikia huo uchumi wa kati wa kweli, basi ni lazima tuwe tunajua jinsi ya kufanya siasa zetu za ndani na za nje, tusije kuwa kama seremala kila tatizo tutatue kwa nyundo.
Watu wa hekima wanasema "Kila sehemu kuna neno lake na kila neno lina sehemu yake", haya maneno ya kusema Tanzania hatujawahi kushindwa vita ni maneno ya kuwaambia majirani zetu kama Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, Msumbiji n.k. Siyo maneno ya kuwatolea watu waliyotutawala kwa miaka na kutupa uhuru bandia, ndiyo ni uhuru bandia kama tungekuwa tuna uhuru kamili hiyo kamati ya bunge isingetujadili na bajeti zetu zisingetegemea misaada kutoka kwao.