Prof. Kabudi aieleza Jumuiya ya Kimataifa kuwa Tanzania haijawahi kushindwa vita ya aina yoyote

Prof. Kabudi aieleza Jumuiya ya Kimataifa kuwa Tanzania haijawahi kushindwa vita ya aina yoyote

Ipeleke twitter, wao nao safari hii wamejipanga kujibu kila eneo.

Tatizo sio kujibu bali unajibu nini. Watu wanataka majawabu na sio majibu. Je umemuona Kabudi akitamka kuhusu hizo €27m, zaidi ya kuongea kwa jazba kuhusu kudhalilishwa na hela? Mifano mingi ya enzi za Nyerere ambayo ni irrelevant na issue zilipo hivi sasa. Halafu asituchanganye watanzania wote na wanaccm wenzake.
 
Nadhani Kabudi hana kumbukumbu sahihi. Tanzania hatujawahi kushinda kwenye vita yoyote ya kiuchumi dhidi ya mabeberu. Mara zote tulisalimu amri, tukawapigia magoti na kuwalamba viatu.
 
Nilitaka kumaanisha yeye anafahamu sheria si amesomea na kuja kuwa mwalimu?

All in all, yeye ameongea na kama EU watajibu basi twangojea hio.

Kama hao wahuni wachache wataendelea kuongea huko mitandani pia tuvute subira.

Richard, kufahamu sheria ni jambo moja, na kuzitekeleza sheria ipaswavyo ni jambo jingine. Chini ya rais huyu ni ngumu kutekeleza sheria zinavyopaswa, kwake sheria yoyote inayombana huivunja bila hofu yoyote, kwa kisingizio cha kuwa inamchelewesha.

Kwa maneno marahisi, hakuna mlevi wa madaraka anayeheshimu sheria. Alichokuwa anaongea Kabudi inafahamika kabisa kinatoka wapi, maana alichoonyesha sio msimamo bali kiburi.
 
Thubutu, hasira zao huwa zinaishia JF na Twitter tu tofauti na hapo hamna kitu

Ahaaa ahaaa nimecheka kwa nguvu, watu hawawezi kuandamana, lakini serikali ndio hiyo inaonyesha jazba ya wazi kwa ajili ya watu wa mitandaoni!
 
Kukaa kimya ni kama wanakubali huo upuuzi unaongelewa, ni vyema kuwajibu mapema kila mtu aelewe ukweli, kuendelea kuacha upande mmoja tu kuongea ni ujinga, acha serikali na wao kujibu mashambulizi na kutoa ufafanuzi, kwa nini wapenzi wa CDM hawafurahii kuona serikali ikitoa ufafanuzi na kujibu upotoshaji?

Haitakiwi ufafanuzi, inatakiwa €27m zirudi maana Tanzania hakuna covid fullstop.
 
Nadhani Kabudi hana kumbukumbu sahihi. Tanzania hatujawahi kushinda kwenye vita yoyote ya kiuchumi dhidi ya mabeberu. Mara zote tulisalimu amri, tukawapigia magoti na kuwalamba viatu.

Nimemsikiliza nikacheka kwa nguvu, anasema Nyerere alirudisha hela kuonyesha kuwa alishinda, ila hajui kuwa tunakumbuka kuwa tulivaa hadi viraka na kujipaka mafuta ya kula, kwa hiyo misimamo yake. Ni vyema wakati anaongea, angetuonyesha deposit slip ya €27m kurudi EU ili tuamini msimamo wake.
 
Ahaaa ahaaa nimecheka kwa nguvu, watu hawawezi kuandamana, lakini serikali ndio hiyo inaonyesha jazba ya wazi kwa ajili ya watu wa mitandaoni!
Tunaandamana mtandaoni serikali yenyewe inaandamana barabarani imesahau nyakati hizi watu ni kupress button tu mambo kwisha wao waendelee kuzururisha hao maaskari wao barabarani
 
Haitakiwi ufafanuzi, inatakiwa €27m zirudi maana Tanzania hakuna covid fullstop.
Kama wanataka zirudi waseme tu zitarudishwa, Ila hatutakubali pesa za masimango, wawe wazi na wanachokitaka ila serikali imeshaweka red line hatutaki masimango tena.
 
Zimejenga hospital na vituo vya afya

Toka wamechukua hela hakuna miezi minne, hivyo vituo vilivyojengwa ni vya matope? Rudisheni pesa majizi wakubwa. Kama mmeiba kura msidhani mtaaiba na hela za wazungu.
 
Siku zote kabla hujafanya jambo au hujazungumza kitu lazima utazame mwisho wake ni nini. Hasa kwa viongozi wetu, lazima wazingatie maneno yao kwani wanaweza kuathiri taifa zima.

Ukiwa kiongozi ukizungumza neno manake taifa limeongea. Sasa hizi kauli ni za kujenga taifa hili au za kubomoa?? Tanzania haipo peke yake ulimwenguni. Tunahitaji uhusiano mzuri na mataifa yote especially kwa mataifa yanayo changia kifedha, kiteknolojia na kiuchumi katika taifa letu. Serikali inapofanya jambo ni lazima itathmini yote hayo ama sivyo tutaingia katika janga baya sana.

Viongozi wetu lazima watangulize maslahi ya taifa mbele na sio maslahi yao binafsi. Kauli za namna hii huenda zikamnufaisha yeye binafsi kuonekana kuwa anafanya kazi nzuri wakati huku kalitokomeza taifa. Kazi ya kiongozi ni kufanya kazi kwa mujibu wa katiba ya nchi na maslahi ya nchi na sio kumfurahisha bosi wake.
 
Kama wanataka zirudi waseme tu zitarudishwa, Ila hatutakubali pesa za masimango, wawe wazi na wanachokitaka ila serikali imeshaweka red line hatutaki masimango tena.

Hutaki masimango kisha unasimanga wasiokusujidia?
 
Taifa letu limekosa viongoz waadilifu na wenye huruma kwa wenzao ,100% ya misaada inalenga kwa wananch wanaitwa wanyonge wanaimba wao ni viongoz wa wanyonge ila wanayoyafanya hawana ata chembe ya huruma n hao wanyonge ,binafs naumia kwa sababu najua madhara tutakayoyapata sio wao ,leo hii tunasaidiwa ila bado hali dhoofu je tukikosa kabisa ,viongoz wetu wawafikirie watu wa hali duni wasitake kuwapa mzigo wa makodi na mfumuko wa bei
Mnyonge mjinga dawa yake ndio hiyo ili akili zikae sawa
 
Lazima tuwe na busara, tusiwe watu wa kukurupuka. Ikiwa ni kamati ya mambo ya nchi za nje ya bunge la umoja wa ulaya na lililojadili uchaguzi wa Tanzania na kutolewa michango tena na wajumbe wachache katika kamati hiyo, kumemfanya waziri wetu wa mambo ya nchi za nje kuja na kuwajibu kwa ubabe!

Nadhani hii si hekima na pia si busara, kama hayo yaliyosemwa ndiyo msimamo wa nchi zao na serikali zao hapo tungeweza kujitetea, lakini ni kamati tu ya bunge inajadili jambo kuhusu nchi yako wewe kama waziri unaanza kujimwambafai!

Ikiwa kama nchi ambayo ndiyo kwanza tunaambiwa kuwa tumeingia kwenye uchumi wa kati na tuna safari ndefu ya kuufikia huo uchumi wa kati wa kweli, basi ni lazima tuwe tunajua jinsi ya kufanya siasa zetu za ndani na za nje, tusije kuwa kama seremala kila tatizo tutatue kwa nyundo.

Watu wa hekima wanasema "Kila sehemu kuna neno lake na kila neno lina sehemu yake", haya maneno ya kusema Tanzania hatujawahi kushindwa vita ni maneno ya kuwaambia majirani zetu kama Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, Msumbiji n.k. Siyo maneno ya kuwatolea watu waliyotutawala kwa miaka na kutupa uhuru bandia, ndiyo ni uhuru bandia kama tungekuwa tuna uhuru kamili hiyo kamati ya bunge isingetujadili na bajeti zetu zisingetegemea misaada kutoka kwao.
 
Zilijenga hospital na vituo afya kuwa siku corona ikitokea ikute hospitali zipo

Kwenye hiyo report ya €27m mtaviweka hivyo vituo vinavyongoja ugonjwa urudi. Wakati huo huo ww weka hiyo list ya hizo hospitali hapa, na ujenzi wake umeanza baada ya kupokea hiyo hela.
 
Kwenye hiyo report ya €27m mtaviweka hivyo vituo vinavyongoja ugonjwa urudi. Wakati huo huo ww weka hiyo list ya hizo hospitali hapa, na ujenzi wake umeanza baada ya kupokea hiyo hela.
Niweke hapa hiyo list kwani hapa ni bunge la ulaya? Hizo pesa hazikutolewa na bunge ulaya ripoti haiendi kwao. Inaenda kwa waliotoa pesa kazi ya bunge la ulaya sio kutoa pesa za misaada halina hela. Hela bunge walizonazo ni za wao kulipana mishahara na posho tu
 
Back
Top Bottom