Prof. Kabudi: Kura za CCM ziko Kanda ya Ziwa, huko (kwenye kanda nyingine) ni za kuongezea ongezea tu!

Prof. Kabudi: Kura za CCM ziko Kanda ya Ziwa, huko (kwenye kanda nyingine) ni za kuongezea ongezea tu!

Siyo kila jambo huzungumzwa.
Mengine unayajua, unayahifadhi kichwani na kuyafanyia kazi kimya kimya.
Wahenga walisema kwamba, unapokula na kipofu usimshike mkono.
 
Sidhani kama hii ni sahihi kwa kanda moja moja ila siyo sahihi kusema kuliko kanda zote kwa ujumla wake.

Dar es salam pekee ina voters almost 1/3 ya voters wa kanda ya ziwa yenye mikoa ya mara, shinyanga, simiyu, geita, mwanza na kagera.
Population ya kanda ya ziwa ni kubwa kuliko maeneo mengine yote yaliyobaki kwa pamoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii kauli ya Kabudi ina maana nyingi mbaya sana.
1 ccm inaelekeza maendeleo kanda ya ziwa kwa sababu ndipo walipo wapiga kura wake

2 kanda zingine hata kama hazitaichagua ccm bado itashinda kwa sababu ccm ni ya kanda ya ziwa.

3 sasa rasmi shughuli za kisiasa zimepata baraka za viongozi wetu kwa kuzingatia ukanda na ukabila.

A worthless Professor this country have ever had.

Kumbukumbu iwekwe, kuwa Leo tena kwa maneno haya ya Kabudi, ndio mwanzo wa ukabila na ukanda wa wazi.

Mungu amrehemu Mwalimu Nyerere, alilipiga vita kwa nguvu zake zote, lakini leo ile juhudi yake imefifishwa na pengine hata kufa.

The beginning of a bad history for my beloved Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafiti ya twaweza inasema ccm inapata kura nyingi kwa watu wasioelimika wajinga bila kujali wanatoka kanda ipi sitaki kuamini kuwa kanda ya ziwa kuna wajinga wengi!
Huo ni ukweli hata kama ni mchungu, Twawezi ndio majibu.
 
Hii siyo kweli kanda ya ziwa toka vyama vya upinzani vianze ndiyo kanda pekee ambayo huwa inapiga jura objectively.

Hii ndiyo kanda pekee iliyombeba Mrema, ikaja ikambeba na Dr Slaaa na katika vipindi vyote hivyo ndiyo ukanda uliotoa wabunge wengi wa upinzani ukilinganisha na kanda zingine zote toka vyama vingi vianzishwe hapa nchi Zanzibar excluded.
Nakupata data.
1995.
1 Mabere Nyaucho Marando
2 John Momose Cheyo
3 Danny Makanga
4 Mtungirehi
5 Ndobo
6 Abraham Msina.
7 Wilfred Lwakatare.
8 Ndimara Tegambwage.
Hawa wote walikuwa kanda ya ziwa.

2000.
1 Mtungirehi
2 Phares Kabuye
3 John Momose Cheyo
4 Danny Makanga alirejea tena. Baadae akahamia ccm
5 Walid Aman Kaborou

2005
1 John Momose
2 Zito Zubery kabwe.
3 Phares Kabuye
4 Said Amour Arfi
5 Chacha Wangwe
6 John Mwera aliyerithi jimbo la Chacha Wangwe.

2010
1 Zito zubrey kabwe
2 John Shibuda
3 Salum Oporukwa
4 John Dibogo Wenje
5 Machemli
6 Moses Machali
7 Felix Mkosamali
8 Henry Kiwia
9 Slyvester Kasulumbay
10 Dr Anthony Mbasa
11 Professor Kahigi
12 Said Amor Arfi
13 Nyerere

2015.
1 Wilfred Lwakatare
2 Emanuel Mkundi kabla hajaunga juhudi
3 Zito Zubery Kabwe
4 Esther Matiko
5 John Heche
6 Marwa yule w Rorya kabla hajaunga juhudi
7 Magdalena Sakaya
8 Esther Bulaya
9 Kasuku Bilago RIP


Kwa trend hiyo ni kanda ipi nyingine imekuwa consistency katika kuchagua wapinzani kama kanda ya ziwa ?

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni upinzani wanaaminika zaidi kanda ya ziwa kuliko kanda nyingine yoyote hapa nchini sema chuki zenu binafsi dhidi ya wasukuma zinafanya msahau kuwa kura nyingi za upinzani hutoka kanda ya ziwa bila kujali ni vijijini au mjini wakati kanda zingine upinzani una nguvu mjini tu.

Tusiishi kea hisia tukashindwa kuona uhalisia wenyewe.

NB
Kanda ya ziwa inapiga kura objectively zaidi kuliko kanda nyingine.
Na hii ni kweli, na ndio maana UMASIKINI, UJINGA, na maradhi au magojwa na ushirikina umajaa huko kanda la ziwa, Ndio sababu wako nyuma ajabu, shule watoto wanakalia mawe chini ya miti, wengi katika kanda la ziwa hata darasa la 7 hawakufika, je unatarajia akili za watu kama hao ziwe aje??? ndio umasikini wa ajabu umekita mizizi huko kanda la ziwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo kanda ndiyo upinzani hubeba kura nyingi kuliko kura zingine.

Tuacheni chuki binafsi.
Sasa unabisha nini wakati twaweza walishasema ccm inazoa kura kwa watu wasiokua na uelewa sasa mikoa nilikutajia hapo unaona wananchi wake wanauelewa?


Sent from my iPhone using JamiiForums

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio maana nchi kama Marekani hawaruhusu majority votes ndio wahamuwe uchaguzi wa kiongozi wa Marekani.President anachaguliwa na maseneta wanaochaguliwa majimboni on ratio basis hili kuondoa sintofahamu ya President asichaguliwe kutoka kwenye majimbo yenye population kubwa.
Huo ni uongo wa wazi kabisa Masenetor hawausiki kumpitisha raisi wa Marekani bali kuna chombo wao wanakiita Electoral collage,Members wake wanaitwa Electors ndo wana muiendose raisi wa Marekani!
 
Back
Top Bottom