Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jalala litabaki kuwa jalala na Mungu atabaki kuwa Mungu.Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi amefafanua vizuri kauli yake ya kutoka jalalani mpaka kuwa Waziri.
Ikumbukwe hapo awali wafuasi wa CHADEMA kwa upofu wa kutokujua neno la Mungu nikimaanisha Biblia wengi walisema kwamba, Prof. Kabudi alimaanisha jalalani ni UDSM na mtu anae watoa watu jalalani ni JPM.
Leo hii akitoa shukrani zake baada ya kuapishwa amesoma Zab 113 na kueleza jinsi Mungu anavyoweza kumnyanyua mtu kumwinua na kupata cheo, hata kama ni mtu hohe hahe.
Jambo la kujifunza hapa ni kwa wafuasi na viongozi wa CHADEMA watambue kuwa, Mungu ndie humwinua mtu na kumtoa jalalani, hivyo wasiwe wanakurupuka na kuropoka hovyo.