Prof Kabudi: Mwandishi mmoja wa kigeni aliandika kuhusu kifo cha Sokoine kwamba Nyerere alihusika au alifaidika na kifo hicho

Prof Kabudi: Mwandishi mmoja wa kigeni aliandika kuhusu kifo cha Sokoine kwamba Nyerere alihusika au alifaidika na kifo hicho

..hata Sokoine alikuwa anakwenda hukohuko.

..alikuwa mbioni kukubaliana na sera za kibepari ambazo Mzee Mwinyi alikuja kutozitekeleza.

..pia aligundua na kusikitishwa na makosa makubwa na uonevu wakati wa zoezi la kukamata wahudumu uchumi.

..lawama za operesheni dhidi ya uhujumu uchumi ziliangukia kwa Sokoine. Yeye alikuwa anajutia kilichotokea, lakini wananchi walikuwa wakimpenda kutokana na operesheni ile.
Uhujumu uchumi ilikuwa balaa
Ukikutwa na dawa ya meno,sabuni tu utaeleza 😄

Ova
 
Hivi wewe unaamini kabisa kuwa Nyerere alijiuzulu uwaziri mkuu baada ya miezi mitatu tu ya uhuru eti akaimarishe chama?. Nyerere alijiuzulu ili kwenda kusuka mipango ya kuifanya Tanganyika iwe Jamhuri , akiwa busy kuandika katiba ya Tanganyika ambayo mkuu wa nchi ni rais. Na pia kumpa nafasi mtu mwingine kufanya "Africanization", kuondoa wazungu kwenye nafasi nyeti na kuweka waafrika. Nyerere hakutaka kuonekana mbele ya muingereza kuwa ni that radical!. Kawawa aliifanya hiyo kazi lakini hakuifanya jeshini na ndiyo maana miaka michache baada ya Nyerere kuibuka na kuwa Rais sasa alinusurika kupinduliwa na wanajeshi wa jeshi la Tanganyika Rifles waliokuwa wanaona bado hawawi promoted kwa kasi waliyoitegemea katika kipindi cha kudai uhuru. Kupendwa kwake na muingereza kulimlipa ndiyo maana maasi yale yalizimwa na jeshi la muingereza!

..Kawawa angekuwa mroho wa madaraka angemgeuka Nyerere.

..wewe huoni jinsi Samia alivyowageuka wenzake, wakati makubaliano yalikuwa wanaondoka 2025, sasa anasuka mipango ya 2035.
 
Waziri wa Katiba na Sheria Prof Kabudi amesema baada ya Kifo Cha Sokoine Maneno mengi yalisemwa ikiwemo " aliuawa kwa njama"

Mwandishi mmoja wa kigeni aliandika Kifo Cha Sokoine Mwalimu Nyerere Alihusika au Alifaidika na Kifo hicho

Mwandishi huyo alisema Nyerere alihofia Sokoine akiwa Rais atape
Prof Kabudi anasema Mwalimu Nyerere alisikitika sana baada ya kusoma Makala hayo na kumwomba Mungu wa Mbinguni amsamehe Mwandishi yule

Source: Mwanahalisi Digital
Huyo Profesa Kabuti ni takataka kama hizi ndizo amebaki nazo kama sifa kwake?

Haya ndiyo maswala anayo weza kuyazungumzia kama waziri, ili watu wakumbuke kwamba kumbe naye bado anapumua?
 
..Kawawa angekuwa mroho wa madaraka angemgeuka Nyerere.

..wewe huoni jinsi Samia alivyowageuka wenzake, wakati makubaliano yalikuwa wanaondoka 2025, sasa anasuka mipango ya 2035.

Angemgeuka Nyerere kwa jeshi gani loyal kwake ?, na kwa wananchi gani?
Miaka ya 1960's Nyerere alikuwa maarufu kwa Watanganyika kuzidi kiasi.
Halafu Muingereza alikuwa anampenda Nyerere, Ingekuwa suicidal kwa Kawawa kujaribu hilo!
 
Angemgeuka Nyerere kwa jeshi gani loyal kwake ?, na kwa wananchi gani?
Miaka ya 1960's Nyerere alikuwa maarufu kwa Watanganyika kuzidi kiasi.
Halafu Muingereza alikuwa anampenda Nyerere, Ingekuwa suicidal kwa Kawawa kujaribu hilo!

..Kawawa naye alikuwa na base yake kwenye vyama vya wafanyakazi.

..Na kwa nchi za Kiafrika ukishashika usukani opportunities za kila aina za kujiimarisha zinajitokeza.

..Kuhusu jeshi wako wanaosema Kawawa angeendelea na Uwaziri Mkuu angeharakisha Africanization jeshini.

..Kuna habari kwamba Kawawa alikuwa muumini wa Africanization kuliko Mwalimu Nyerere.

..Wadadidisi wanasema maasi ya Tanganyika Rifles yalitokea kwasababu ya kusitasita kwa Mwalimu Nyerere kufanya Africanization jeshini.
 
Muulizeni Cleopa Msuya kabla ya ..,fa, huyu ndiyo kabakia katika master planners
Wewe naweza kukusikiliza, kwa hayo uliyo andika na kuyatafakari kwa kina.
Umetaja uhusika wa CCM, kwa vipi. Hao ulio taja majina ndio walikuwa ni CCM?

Sasa tungekuwa na waandishi nguli wa maswala ya uchunguzi; mengi ya haya ndiyo wange yatumia kuzama katika uchunguzi wao, na kutoka na bonge la kitabu au taarifa ya chapisho.

Na huyo Dube bila shaka yungali hai?
 
Wacha bhwanah!
Sasa tutatafutiza kila visababu hata visivyo kuwa na mwanzo wala mwisho! Nyakati hizo za kifo cha Sokoine, Kawawa awe na 'base' kwa wafanya kazi?

..nazungumzia wakati wa harakati za kudai uhuru, na mara baada ya uhuru kupatikana.

..Rashidi Kawawa alijiunga na Tanu akitokea ktk jumuiya za vyama vya wafanyakazi.

..hoja yangu ni kwamba Rashid Kawawa angeweza kung'ang'ania ktk Uwaziri Mkuu mwaka 1962 wakati Mwalimu Nyerere alipojiuzulu nafasi hiyo.

..sasa mimi nimejenga hoja kuwapinga wanaodai kuwa Rashidi Kawawa amehusika kumuua Edward Sokoine ili kutimiza dhamira yake ya kuwa mrithi wa Mwalimu Nyerere.
 
Back
Top Bottom