Hivi wewe unaamini kabisa kuwa Nyerere alijiuzulu uwaziri mkuu baada ya miezi mitatu tu ya uhuru eti akaimarishe chama?. Nyerere alijiuzulu ili kwenda kusuka mipango ya kuifanya Tanganyika iwe Jamhuri , akiwa busy kuandika katiba ya Tanganyika ambayo mkuu wa nchi ni rais. Na pia kumpa nafasi mtu mwingine kufanya "Africanization", kuondoa wazungu kwenye nafasi nyeti na kuweka waafrika. Nyerere hakutaka kuonekana mbele ya muingereza kuwa ni that radical!. Kawawa aliifanya hiyo kazi lakini hakuifanya jeshini na ndiyo maana miaka michache baada ya Nyerere kuibuka na kuwa Rais sasa alinusurika kupinduliwa na wanajeshi wa jeshi la Tanganyika Rifles waliokuwa wanaona bado hawawi promoted kwa kasi waliyoitegemea katika kipindi cha kudai uhuru. Kupendwa kwake na muingereza kulimlipa ndiyo maana maasi yale yalizimwa na jeshi la muingereza!