Prof. Kabudi: Ndege ya Tanzania, Bombardier Q400 imekamatwa Canada na kesi ipo Mahakamani

Hiki kikundi kilitumia pesa nyingi South Africa ikiwemo kutembeza Rushwa hakifai kupelekwa popote gharama zake ni kubwa mara mia kupunguza Deni kuliko kugharamia hicho kikundi kwenda tena Canada.
Duh! Kwa hiyo serikali inayopiga vita rushwa inatoa rushwa ? Kama kule Bondeni wamelijua hilo heshima yetu imevunjika kabisa.
Kwa nini awamu ya tano kila kona inatutia aibu na wenye kuisema hawaisemi bali kuisifia kwa mgongo wa chupa kama mazuzu?
Hivi kweli viongozi mnadiriki kumvua nguo mama (Tanzania) ili kusitiri uchi wa mfalme? Mna akili nyie?
 
kinachonishangaza sana mh.waziri, mwanasheria nguli kuilaumu serikali ya canada wakati anajua wazi hayo ni mambo ya kimahakama. wenzetu wanaheshimiana ktk mihimili. hata afrika ya kusini serikali ya kule haikuiingilia walimalizana mahakamani!!!.kwa nini tusingizie mabeberu na kesi ni ya miaka mingi!?! na jamaa huyuhuyu mkulima alishinda kesi hii hapahapa kwetu TZ. huko kwingine anakazia tu hukumu yake. jamani tumewapa madaraka hayo mtusaidie kuipeleka nchi mbele sio kutupotosha na siasa zenu za miaka ya cold war. muiteni mkulima mkae naye chini muyamalize. vinginevyo jamaa atatuendesha sana, wenzetu huko nje hawana janjajanja nyingi kwenye sheria. Rais anashtakiwa na kushindwa mahakamani, ije iwe kesi zetu hizi!!!. uvunje uhusiano na canada!!! jiulize kwanza nani atapata hasara?!?. jifunze CHINA VS MAREKANI, IRAN VS MAREKANI. Ng'wamishaga mhola bang'wise
 
Kwenye kila chonganishi kuna sababu na hapa sababu kuu ni DENI ..tulipe tu
 
Hii nchi ya ajabu sana sijui watu uzalendo wameweka wapi hapa mtaani kwangu kuna uchaguzi Wa Mwenyekiti Wa mtaa mpaka SAA hii naona box LA kupigia kura kuna kura moja iliyopigwa SAA 12 watu wanapita tu na shughuli zao
 
Inakuwaje kulipa deni unaita MAKOSA?
 
Kama Ndege sio ya ccm kwanin wakati wa mapokezi wapinzani urushiwa vijembe na kutukanwa ? kwani wao hawalipi kodi katka nchi hii?
 
Naunga mkono Hoja yako kwa 100% hii Tabia ya kutumia Neno uzalendo mabeberu kuharalisha dhuluma ubabe wa kishamba haitasaidia Nchi zaidi ya wajanja kupiga pesa kwa kisingizio cha kusuruhisha kumaliza kesi, pesa inayotumika kupambana na mkulima wa kizungu ni kubwa kuliko kupunguza Deni, wapo wanufaika wa usumbufu huu na hao ndiyo wanamchochea mtukufu malaika azidi kuendeleza ligi na Mzungu.
 
Inakuwaje kulipa deni unaita MAKOSA?
Deni la Mzungu sasa ni Dili la wajanja huko CCM, magufuli mtukufu alizuia safari za nje lakini sasa wanasafiri na kulipwa posho pesa nyingi kwa visingizio vya kumaliza Deni la mkulima wa kizungu, wapo wajanja wanapiga pesa kupitia fursa hii hii
 
Hawa hawanaga tofauti na wale wanaume ambao mtoto akifanya vizuri ni wa kwake ila akifanya mbaya ni wa mwanamke, yaani leo imekamatwa ni ndege ya Watanzania ikifika salama ni Magufuli kanunua ndege, kama kweli ndege ni Watanzania je utaratibu ulifuatwa kununua hizo ndege au ni hela zimechukuliwa tu kama vile baba anafanya shopping za familia
 
Kwani nani aliwalazimisha kushindwa kumlipa huyo mkulima?
Watanzania tupo milioni zaidi ya 50 tunalipa kodi ili kuleta maendeleo nchini
Tunanunua ndege SGR umeme rufiji nk
Leo unachonganisha eti ndege yetu ikamatwe kama kuna mtanzania anafanya hivyo ni laana tu Lilah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…