Prof. Kabudi: Ndege ya Tanzania, Bombardier Q400 imekamatwa Canada na kesi ipo Mahakamani

Mabeberu na michezo yao ya kishetani

Wamemshindwa kwenye karatasi sasa wanavizia mali zetu


Rais Magufuli funga Ubalozi wa Canada Ndani ya saa 72 ili watoe Maelezo
Huwa nawashangaa sana mnapowapachika jina la beberu au mabeberu kila mnapoona hawaendani na mawazo yenu.

Hivi hamuelewi shughuli ya beberu? Mbona mnajitukana hivi?
 
Hahahaaaaaaa imebidi nicheke kwanza mkuu kwani umenena ukweli mtupu mahakama huko Tawala za nyuma ulikuwa huru ndiyo maana hata Mzungu alishinda kesi Nchini, na Leo hii huyo Mzungu angeendesha kesi chini ya mahakamaccm Nchini asingeshinda kesi kamwe, mahakamaccm chini ya utawala wa Naibu Rais Daud Bashite na mtukufu malaika haipo Huru mpaka 2026 wakitoka ikulu, Mahakama za Ulaya America Asia ni mahakama Huru haziingiliwi na Serikali zao kama Tanzania ndiyo maana kesi nyingi huamuliwa kwa haki.
 
Huwa nawashangaa sana mnapowapachika jina la beberu au mabeberu kila mnapoona hawaendani na mawazo yenu.

Hivi hamuelewi shughuli ya beberu? Mbona mnajitukana hivi?
Matumizi ya Neno uzalendo na ubeberu CCM ni kuharalisha dhuluma, pindi wakitaka kufanya dhuluma na vitendo haramu husingizia ni uzalendo hawakumbuki mtukufu magufuli alishasema watanzania siyo wajinga .
 
Mwaka 2026 atapona mwenye kinga pekee wengine wote akina Doto Daud Bashite na wenzao wataelekea segerea keko Ukonga kujutia matendo yao ya sasa
 
Njia rahisi ya kuuondoa ubeberu katika suala hili ni kumlipa salio analodai huyu mkulima Steyn toka Afrika Kusini. Au la tuongee naye kwa upole na kumrudisha aje aendelee kulima mashamba aliyotaifisha Mwalimu Nyerere
 
Watanzania tupo milioni zaidi ya 50 tunalipa kodi ili kuleta maendeleo nchini
Tunanunua ndege SGR umeme rufiji nk
Leo unachonganisha eti ndege yetu ikamatwe kama kuna mtanzania anafanya hivyo ni laana tu Lilah
Endeleeni tu kulishana matango pori, dawa ya deni ni kulipa
 
Duuh! Pascal ulienda Rom kwa Pop? Umepata nini? Hoja yako muruaaaa sana![emoji106]
 
Mwaka 2026 atapona mwenye kinga pekee wengine wote akina Doto Daud Bashite na wenzao wataelekea segerea keko Ukonga kujutia matendo yao ya sasa
Mkuu hata mwenye kinga atategemea zaidi nani yuko madarakani au nani wana nguvu bungeni. Kiongozi mwingine anaweza kuliomba bunge liondoe kinga kwa walao wiki tuu mtu ashughulikiwe kama alivyo fanyiwa Chiluba kule Zambia
 
Kabudi anaongea Pumba tu, serikali hii kesi ilishashindwa toka zamani sana na ikakubali kushindwa, ikaanza kulipa deni ikafika katikati inagoma kuendelea kulipa deni la watu, sasa wao kina Kabudi watuambia huko SA walishinda nini..
 
Oh prof kabudi ananishangaza, kwa elimu yake asingejiulza hayo maswali kwamba kwanini Canada? Na anamwita barozi wa Canada .prof ni mwanasheria suala likiwa mahakama anamwita barozi ili afanye Nini?
Kwani serikali ya Canada umekosea nini hapo hadi aseme tumekasirishwa sana?
 
Kabudi anaongea Pumba tu, serikali hii kesi ilishashindwa toka zamani sana na ikakubali kushindwa, ikaanza kulipa deni ikafika katikati inagoma kuendelea kulipa deni la watu, sasa wao kina Kabudi watuambia huko SA walishinda nini..
Pesa za mkulima wa kizungu ilitoka ikawa tayari kuwekwa kwenye A/c yake ndipo Kabudi Daud Bashite na wenzake wakamshauri mtukufu malaika waipore hiyo pesa kibabe na huyo Mzungu afukuzwe Nchini kwa njia haramu wapate kumdhulumu kirahisi, njama za dhuluma na vurugu zote zimepangwa na hao wana CCM, hawakuwaza kuna kesho waliangalia matumbo yao binafsi, sasa kesi imegeuka wanataka iwe ya kitaifa zaidi wakati wanaosababisha Tatizo ni wao binafsi.
 
Profesa kabudi kichwani hana taaluma tena kaishiwa maarifa, kero hii imesababishwa na Tamaa zake kumpora kumdhulumu mkulima wa kizungu na kumfukuza Nchini kwa njia haramu za kishetani, leo hii kageuka kuwatesa Balozi na watu wengine ambao hawahusiki na unyama wake binafsi, profesa wa aina hii ni sawa na yule profeselii wa Olijino comedy, Hii Tabia mbovu ya Serikali kufanya maamuzi mabaya lakini kuwatoa kafara wasiohusika inazidi kuota mizizi kwenye utawala huu dhalimu.
 
Makosa ya kuharalisha dhuluma kwa mkulima wa kizungu yamefanywa na profesa Kabudi hata pesa za mkulima zilizotoka zikapigwa mfaidika ni Kabudi iweje sasa anasaka huruma toka kwa watanzania kwa matendo yake haramu?
 
anadai fidia baada ya mali zake kutaifishwa na Serikali ya Tanzania mwaka 1980
Tokea mwak wa 1980 hadi leo kwa deni kutolipwa ni hatari kubwa kwa taifa kudaiwa na mtu. Hii inaonesha ni kiasi gani wanasiasa wanavyofanya makosa ya kimaamuzi na kukurupuka.
Baba wa Taifa ndo alikuwa Raisi wa wakati huo,lakini Makosa yake yanutugharimu sisi leo miaka 39 baadae.
Halafu na sisi bado tunaleta ubabe kukimbia ukweli huu,yatupasa kuchukuwa Tahadhari maana kweli Mabeberu ni wanyama,Lakini pia ni kweli kuwa Tulimsababishia Hasara kubwa kwa kuzitaifisha mali zake na kuziacha kuharibika.
 
Habari
Nimeumizwa sana na taarifa toka kwa waziri kabudi.
Hii imenifanya niwaze mambo machache ambayo nahitaji tuyaongee hapa
Mimi ni mlipa kodi mwaminifu kwasababu nakaywa TAX katika mshahara wangu kwahiyo ndege hii inajasho langu.
Naomba kwanza niiombe serikali ikae ipitie mikata ba ya kununua vitu toka nje.
Nadhani ndege au chochote kianze kuhesabika kuwa mali yetu pale kitakapotua katika Ardhi ya Tanzania.

Kwanini iwe hivyo, hii itafanya wale wanaodai kama wanamambo yeyote yale washike ndege zitakapokuwa zinafanya service sio zikiwa katika manunuzi.

Pili. Serikali ikabidhi au iingie ubia na kampuni ya ATCL na ndege kwa kukodiwa na shirika hilo ili serikali ijinasue na kushikwa shikwa kwa vyombo hivi. Yaani ikiwa huyo mdai anaidai Tanzania kama serikali basi aishike serikali sio kampuni iliyokodishiwa kifaa.

Serikali ijiondoe kununua ndege kwenye nchi ambazo zinaroho ya korosho yaani wanakuuzia kitu bado wanaona wivu . Canada wameonesha upuuzi mkubwa sana .
Ndege imeagizwa bado inatengenezwa alafu mtu anakuja kushika kiwandani unamruhusu kwasababu tu inaalama za Twiga na ATCL?
Hivi nikipeleka gari langu garage mtu aweza lishika garage kama nadaiwa na mwenye garage akampa? Hii inaonekana hicho kiwanda wanamawasiliano na hao mabebelu.
Itoshe serikali kuchukua fedha zetu tukanunue kwingine waachiwe ndege yao.

Mwisho
Hata kama serikali awamu ya kwanza iliingia kwenye madeni hayo ambayo kwangu siyajui terms and conditions zake niwasihi kwa hekima kama watanzania tulivyo na uungwana . Hebu tujinyime tulipe deni hilo.
Hawa wazungu sio watu wa kuwachekea mimi nawachukia sana siwapendi kabisa .

Alafu wale wanaoshabikia hii mimi najikia vibaya sana sio jambo jema. Haya ni maendeleo yetu sisi sio ya mtu mwingine labda kama hutoagi kodi.
 
Dawa ya deni Ni kulipa tuache kurukaruka kama maharagwe....watangulizi wake wamelipa yeye Ni Nani asimalizie deni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…