Prof. Kabudi: Ndege ya Tanzania, Bombardier Q400 imekamatwa Canada na kesi ipo Mahakamani

Prof. Kabudi: Ndege ya Tanzania, Bombardier Q400 imekamatwa Canada na kesi ipo Mahakamani

Habari
Nimeumizwa sana na taarifa toka kwa waziri kabudi.
Hii imenifanya niwaze mambo machache ambayo nahitaji tuyaongee hapa
Mimi ni mlipa kodi mwaminifu kwasababu nakaywa TAX katika mshahara wangu kwahiyo ndege hii inajasho langu.
Naomba kwanza niiombe serikali ikae ipitie mikata ba ya kununua vitu toka nje.
Nadhani ndege au chochote kianze kuhesabika kuwa mali yetu pale kitakapotua katika Ardhi ya Tanzania.

Kwanini iwe hivyo, hii itafanya wale wanaodai kama wanamambo yeyote yale washike ndege zitakapokuwa zinafanya service sio zikiwa katika manunuzi.

Pili. Serikali ikabidhi au iingie ubia na kampuni ya ATCL na ndege kwa kukodiwa na shirika hilo ili serikali ijinasue na kushikwa shikwa kwa vyombo hivi. Yaani ikiwa huyo mdai anaidai Tanzania kama serikali basi aishike serikali sio kampuni iliyokodishiwa kifaa.

Serikali ijiondoe kununua ndege kwenye nchi ambazo zinaroho ya korosho yaani wanakuuzia kitu bado wanaona wivu . Canada wameonesha upuuzi mkubwa sana .
Ndege imeagizwa bado inatengenezwa alafu mtu anakuja kushika kiwandani unamruhusu kwasababu tu inaalama za Twiga na ATCL?
Hivi nikipeleka gari langu garage mtu aweza lishika garage kama nadaiwa na mwenye garage akampa? Hii inaonekana hicho kiwanda wanamawasiliano na hao mabebelu.
Itoshe serikali kuchukua fedha zetu tukanunue kwingine waachiwe ndege yao.

Mwisho
Hata kama serikali awamu ya kwanza iliingia kwenye madeni hayo ambayo kwangu siyajui terms and conditions zake niwasihi kwa hekima kama watanzania tulivyo na uungwana . Hebu tujinyime tulipe deni hilo.
Hawa wazungu sio watu wa kuwachekea mimi nawachukia sana siwapendi kabisa .

Alafu wale wanaoshabikia hii mimi najikia vibaya sana sio jambo jema. Haya ni maendeleo yetu sisi sio ya mtu mwingine labda kama hutoagi kodi.
Mm naona hizo ndege ni zamtu binafsi kwani bunge halijawahi hata kukaa kikao kimoja ikapitisha bajeti ya kununuliwa ndege
 
Mleta mada upeo wako ni mdogo sana.
Unapaswa kufahamu kuwa, sio serikali au ATCL ambao wako huru kipesa, wote ni watumwa wa madeni kupita maelezo, na tatizo sio kudaiwa, tatizo ni kugoma kulipa kile unachodaiwa. Huu uhuni wa kugoma kulipa madeni unafanywa zaidi sasa, hivyo wanaotudai wameamua kupambana kisheria kuudhibiti huo uhuni.

Dawa ya deni ni kulipa.
 
As far as the matter concerned, I have understood that inept, incompetent person may handle the matter in the wrong way.
 
Haya haraka sana walala hoi bebeni mabango muandamane na kuimba tunataka ndege yetu ingawa hamna chance yeyete maishani mwenu kuona ndani ya ndege hizo wachalia mbali kuzitumia kwa safari. Tanzania oyeeee!!!!!
 
Safari ijayo kamata mtoto wa jiwe anayesoma nje ya nchi.

Mshahara wa dhambi ni mauti, yalishasemwa miaka mingi sana, watumishi wameumia ajili ya hizi ndege,

na bado.

Usipotubu dhambi hii itakusumbua sana, acha kiburi cha uzima hakina mwisho mwema. kutubu ni rahisi tu.

Angalia sasa aibu hiii, unanuka uozo wa fungus mtaa mzima. kumbuka hao ni Mabeberu wenzake.

Lipa tu.
 
Hii ndio aina ya maprofesa wenye degree tano tulionao nchi hii, msikilize huyu Kabudi guy katikati ya maneno utaelewa kuna shida mahali, anaongea na Rais kama vile anamshitaki mtoto (Canada) kwa babaye (Rais wa JMT) kichwani kwake sijui anafikiri Rais wa nchi hii ni nani huko ulimwenguni!

Dawa ya deni kulipa wangemuita mkulima kwenye meza ya makubaliano wamuombe kulipa hata kwa installments. Yanayoendelea ni matokeo ya kujimwambafy, Poor my Country!
 
Canada wachakarike maana watapoteza biashara, hamna tena kununua ndege kutoka huko, habari za makinikia bado huwauma sana.
 
Canada wachakarike maana watapoteza biashara, hamna tena kununua ndege kutoka huko, habari za makinikia bado huwauma sana.
Canada hawawezi kushabikia unafiki dhuluma kisa watakosa soko la Tanzania, Canada wanapenda haki hawataki dhuluma za kishamba shamba toka kolomije
 
Lakini hii serikali yetu inakwama wapi sehemu moja hiyohiyo zinakamatwa ndege zaidi ya mbili na bado unajipeleka. Ni ujinga.
Huwezi kushinda haki kwa ujanja dawa ya salama ya ndege ni kulipa sio kuwkepa safari, je MKULIMA akiweka zuio dunia nzima ndege zitakuwa zinasafiri ndani ya nchi tu?
 
Huyu analeta uchuro mchana kweupe. Hizo USD 33 million bora tulipe tu, sasa inakuwa kero. Sisi ni taifa kubwa hebu wamlipe maana pesa zipo. Tuangalie yajayo, vile vile tutaweka heshima maana ni tangu enzi ya Baba wa Taifa, tufanye kila linalowezekana tumalize hii ghasia. We have better things to do kuliko kulumbana na kichaa mabaye ana kakundi ambako kanamsaidia. Lets show maturity.
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi Kabudi amesema ndege ya Tanzania Bombardier Q400 iliyokuwa iwasili nchini hivi karibuni imekamatwa nchini Canada na kesi ipo Mahakamani

NDEGE NYINGINE YA TANZANIA YAKAMATWA CANADA

- Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi amesema ndege aina ya Bombardier Q400 imekamatwa

- Ndege hiyo iliyokuwa iwasili nchini hivi karibuni imekamatwa na kesi ipo Mahakamani

"Mhe. Rais ndege yetu aina ya Bombadier ambayo ilipaswa ifike Tanzania kutokea Canada imekamatwa na mtu yule yule ambaye aliikamata ndege yetu kule Afrika ya Kusini." - Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje.

======

Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amesema ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400 imakamatwa nchini Canada.

Amesema aliyesababisha Bombardier kukamatwa ni Hermanus Steyn, raia wa Afrika Kusini ambaye alifungua kesi ya madai Mahakama Kuu nchini Afrika Kusini akidai fidia ya dola 33 milioni.

Kesi hiyo ilisababisha Mahakama hiyo kuizuia ndege ya Tanzania aina ya Airbus A220-300 kuondoka nchini humo Agosti, 2019.

Steyn, anadai fidia baada ya mali zake kutaifishwa na Serikali ya Tanzania mwaka 1980. Hata hivyo, Septemba 3, 2019 mahakama hiyo iliamuru ndege hiyo iliyokuwa imezuiwa katika uwanja wa ndege wa Oliver Tambo kuachiwa baada ya Serikali kushinda kesi bila kutoa fedha yoyote.

Akizungumza leo Jumamosi Novemba 23, 2019 mjini Dodoma katika hafla ya kuapishwa kwa mabalozi, Profesa Kabudi amesema, “ndege imekamatwa na kesi ipo mahakamani. Aliyesababisha ni yuleyule (Steyn) aliyesababisha ndege yetu kuzuiwa Afrika Kusini.”

Profesa Kabudi amesema kuendelea kwa vitendo hivyo ni hujuma za mabeberu wasiofurahishwa na maendeleo nchini.

Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na Rais wa Tanzania, John Magufuli aliyewaapisha mabalozi hao, Profesa Kabudi amesema, “tulikwenda mahakamani tukamshinda (Afrika Kusini) akakata rufaa na wiki iliyopita tukamshinda tena, huyohuyo sasa amekimbilia Canada amekamata ndege ya Bombardier Q400 ambayo ilikuwa ifike nchini.”

“Jambo linalosikitisha ndege zilizokuwa zinatoka Marekani aina ya Dreamliner mbili hazikukamatwa zimefika lakini kila ndege inapotakiwa kuondoka Canada tunashangaa hao matapeli wanajuaje na ndege zinakamatwa.”
Amesema Balozi wa Tanzania nchini Canada aliitwa nchini na kuelezwa jinsi nchi isivyofurahishwa na kukamatwa kwa ndege zake kila zinapokaribia kuja kuondoka nchini humo.

“Nimemwambia sio tu kwamba tunasikitika bali tunakasirishwa, na tunafikiri mheshimiwa rais kukushauri kama Canada inaendelea kuruhusu vitu kama hivyo sio wao peke yao wanaotengeneza ndege, hatukufanya makosa kununua ndege Canada, hata Brazil wanatengeneza ndege,” amesema Profesa Kabudi.

Amesema wameandaliwa wanasheria kwenda Canada kuipigania ndege hiyo.

Kushikiliwa kwa ndege hiyo kunarejesha kumbukumbu ya ndege nyingine ya Tanzania aina ya Bombardier Q400-8 iliyozuiwa nchini Canada mwaka 2017 kutokana na madai ya Sh87.3 bilioni zilizokuwa zikidaiwa na kampuni ya kikandarasi.

Mabalozi walioapishwa katika hafla hiyo ni Meja Jenerali Anselm Shigongo Bahati (Misri), Mohamed Abdallah Mtonga (Abu Dhabi), Jestas Abouk Nyamanga (Ubelgiji), Ali Jabir Mwadini (Saudi Arabia) na Dk Jilly Elibariki (Burundi).



Chanzo: Mwananchi
Halafu Profesa macho kodo anasema eti walishinda kesi mahakamani?!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Sasa kama kesi mlishinda inakuwaje mnatuma mawakili kugomboa ndege. Si atumwe mtu mmoja tu aende na 'nakala ya hukumu' ndege iachiwe? Mataga kweli!!!!
 
Dawa ya deni ni kulipa ili kufanya Safari za ndege zetu kimataifa ziwe na amani
Tutarukaruka huku na huko, tukijitangaza kuwa wababe, lakini mwisho dawa ya deni ni kulipa.

Hili la kupora mtawapora watanzania wajinga wanaofikiri kuwa serikali ni kama mzazi. Hata wahindi wamekuwa wajanja, kesi zao zinapelekwa nje kusuluhishwa.

Hizi mahakama za kiswahili zimekuwa za kubariki ufisadi na uvunjivu wa sheria unaotendwa na serikali.
 
Back
Top Bottom