Prof. Kabudi: Ndege ya Tanzania, Bombardier Q400 imekamatwa Canada na kesi ipo Mahakamani

Haohao ndio mnawaita wahisani wakitoamisaada aumikopo!!!
Mabeberu na michezo yao ya kishetani

Wamemshindwa kwenye karatasi sasa wanavizia mali zetu


Rais Magufuli funga Ubalozi wa Canada Ndani ya saa 72 ili watoe Maelezo
 
Nasisi wakulima wa korosho tunaungananae mkulima mwenzetu katika kesi hiyo ya madai
 
Haya mabeberu yanataka tutudhoofisha lakini tuko imara sana,niendelee kumpongeza Rais Dr Magifuli kwa utulivu huu
 
Ule mkakati uliofanyika pale ubalozi wa South Africa wakati ule labda utasaidia tena.
Yuleyule aliyefanya wakati ule na afanye tena sasa, ahamasishe watu waandamane hadi ubalozi wa Canada na mabango wakiimba "TUNATAAKA. NDEGE YEETU. TUNATAAKA. NDEGE YEETU"

Kitaeleweka tu
 
Tena deni linakaribia thamani ya ndege safari hii mkulima kashika penyewe
Tumuombeeni dua ili afanikiwe
Karma nyingine ya uchafuzi
 
Thubutu yako, nani aache kuingia Canada ajili ya mshamba mmoja tu, limbukeni mawazo. ndege za kunua kwa watu siyo maendeleo, tengeneza za kwako.
LIPA DENI, NA BADO, RAIS HEWA.
 
Duh! Huyu mkulima amezidi sasa, Yani ndege mpya ambayo hata haijakabidhiwa ramsi kwa Tanzania inashikwa!!

Mamlaka nchini Canada zimekamata ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400.

Hii ni mara ya pili kwa ndege ya nchi hiyo kuzuiliwa nchini Canada.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi amethibitisha kukamatwa kwa ndege hiyo iliyokuwa iwasili nchini hivi karibuni.

Sababu ya kukamatwa kwa ndege hiyo, kwa mujibu wa Prof Kabudi ni kesi iliyofunguliwa na mkulima mstaafu raia wa Namibia Hermanus Steyn.

Steyn pia alifungua kesi nchini Afrika Kusini mwezi Agust iliyosababisha ndege aina ya Air Bus 220-300 izuiliwe na hatimaye serikali ya Tanzania kushinda kesi mahakamani

"Mhe. Rais ndege yetu aina ya Bombadier ambayo ilipaswa ifike Tanzania kutokea Canada imekamatwa na mtu yule yule ambaye aliikamata ndege yetu kule Afrika ya Kusini." - Prof. Palamagamba Kabudi, ailisema mjini Dodoma katika hafla ya kuapishwa kwa mabalozi.


...... Soma zaidi hapa Mkulima ‘akamata’ tena ndege ya Tanzania Canada
 
Huo mwaka 80 raisi alikuwa Nyerere?Huyu Mzee naye katuachia majanga!
 
Tanzania yaeleza hasira zake kwa Canada
Amesema Balozi wa Tanzania nchini Canada aliitwa nchini na kuelezwa jinsi nchi isivyofurahishwa na kukamatwa kwa ndege zake kila zinapokaribia kuja kuondoka nchini humo."Nimemwambia sio tu kwamba tunasikitika bali tunakasirishwa, na tunafikiri mheshimiwa rais kukushauri kama Canada inaendelea kuruhusu vitu kama hivyo sio wao peke yao wanaotengeneza ndege, hatukufanya makosa kununua ndege Canada, hata Brazil wanatengeneza ndege," amesema Profesa Kabudi.Amesema wameandaliwa wanasheria kwenda Canada kuipigania ndege hiyo.

Kushikiliwa kwa ndege hiyo kunarejesha kumbukumbu ya ndege nyingine ya Tanzania aina ya Bombardier Q400-8 iliyozuiwa nchini Canada mwaka 2017 kutokana na madai ya Sh87.3 bilioni zilizokuwa zikidaiwa na kampuni ya kikandarasi.
 
Nia yao nzuri Anzori Gwanda apatikane tu, Tundu arudi, tutapaka sana huko majuu mpaka mnuke
Mabeberu yanataka kutufanya nini? Ukizingatia siku zote beberu huwa dume. Au yametufananisha na mitetea ya mbuzi?
 

Lile jopo la wanasheria waliotumwa S.Africa si litumwe tu? ndani ya siku mbili/tatu ngoma itakuwa imeisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…