Prof. Kabudi: Zambia haijafunga mpaka wake na Tanzania eneo la Nakonde

Prof. Kabudi: Zambia haijafunga mpaka wake na Tanzania eneo la Nakonde

Kuna vitu vinatokea Bongo raia tupo silent tu, wakati vingetokea kwenye nchi za wenye awareness ingekua ni hot topic watu wanaijadili ila sisi as if nothing happened...mf ishu ya speaker na wabunge wa chadema, ndugai ana violate katiba yetu watanzania alafu tunamuacha tu
Jambo ambalo ni baya sana katika kuhakikisha kasi ya maendeleo tunaivuta. Tumelogwa mkuu [emoji24][emoji24]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna vitu vinatokea Bongo raia tupo silent tu, wakati vingetokea kwenye nchi za wenye awareness ingekua ni hot topic watu wanaijadili ila sisi as if nothing happened...mf ishu ya speaker na wabunge wa chadema, ndugai ana violate katiba yetu watanzania alafu tunamuacha tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Inauma sana kwa wale ambao tayari wako aware
 
Ngoja wazushi waje, wote walidesa ndio chababu wanamshadidia another failure Mbowe.
 
1589451526706.png

Serikali imewatoa hofu Watanzania na kusema kwamba Zambia haijafunga mpaka wake na Tanzania. Imesisitiza kuwa uhusiano kati ya nchi hizo ni mzuri.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, ametoa ufafanuzi huo jana Bungeni jijini Dodoma, wakati akihitimisha hoja za Wabunge waliojadili Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2020/2021.

" Nataka niwaambie Zambia haijafunga mpaka na Tanzania, narudia tena Zambia haijafunga mpaka na Tanzania ,haya si maneno yangu,ninayo barua kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje nchini Zambia Joseph Malanji ambaye Mungu amemjaalia kujua lugha nyingi.

"Kwa hapa Tanzania anazungumza kinyakyusa , Kinyiha, Kinyamwanga, na jana na leo tumezungumza kwa Kiswahili. Naomba nisome barua yake japo ni jambo ambalo si la kawaida , ameniandikia barua ambayo imefika leo baada ya kufanyika kwa mazungumzo,"alisema Profesa Kabudi na kisha kuisoma barua hiyo iliyoandikwa kwa lugha ya Kingereza.

Profesa Kabudi alifafanua kwa mujibu wa barua hiyo ambayo imefafanua kwa kina kuwa Zambia haijafunga mpaka, imeeleza kuwa Kamati ya timu ya watalaamu kutoka Tanzania na Zambia watakutana kwa pamoja kuweka mambo sawa na kisha huduma kurejea kama kawaida.

Aidha, Waziri Kabudi, amesema, kamwe Tanzania haitaruhusu maadui kutaka kuivuruga Jumuiya ya Afrika Mashariki.
 
kama kawaida, tunaongelea maadui!

Tunaogopa maadui wasiokuwepo! Kila mara anazungumzia maadui tu, imekuwa ni excuse sasa. Mnaacha kutimiza majukumu yeni mnaota maadui tu. Watajeni basi hao maadui tuwajue.

Very cheap politics!
 
Nini maana ya kufunga? Kama hawajafunga maroli ya mizigo yamezuiliwa kwanini? Wataalamu wanakutana kutatua tatizo lipi? Kabudi ni debe tupu tumpuuze.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom