Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo kupitia Ukurasa wakewa X (Twitter) amekanusha taarifa iliyotolewa na Sauti ya America inayoelezea Mkopo wa Tanzania na Masharti ya kuiachia kuchimba madini baharini.
Soma: - Tanzania imepokea mkopo kutoka kwa Korea Kusini na kutoa sehemu ya bahari na madini
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Kitila Mkumbo ameandika:
- Ziara ya Rais Samia Korea Kusini atasaini Mkopo wa Tsh. Trilioni 6.51
Soma: - Tanzania imepokea mkopo kutoka kwa Korea Kusini na kutoa sehemu ya bahari na madini
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Kitila Mkumbo ameandika:
URONGO. Hakuna masharti kama hayo. Mkopo huu ni sehemu ya makubaliano katika awamu ya pili ya ushirikiano wa miaka mitano ijayo. Ni mkopo nafuu utakaolipwa katika miaka 40 kuanzia mwaka wa 26 kwa riba ya 0.01%.
Kuhusu madini ya kimkakati (strategic mineral resources-SMR), mkakati wa Tanzania ni kutafuta wawekezaji watakaowekeza katika utafiti, uchimbaji na kuongeza thamani ndani ya nchi.
Tumeweka wazi duniani kote kuwa tunataka wawekezaji watakaosafirisha betri za magari na sio madini ya kimkakati kwa lengo la kutengeneza betri hizo nje ya nchi. Kuhusu uchumi wa buluu, tumesaini mkataba kwa lengo la kushirikiana katika kuboresha teknolojia ya uvuvi, kujenga bandari za uvuvi na viwanda vya kuchakata Samaki. Eneo lingine ni ushirikiano katika teknolojia ikiwemo kujenga chuo cha TEHAMA nchini.
PIA SOMA- Ziara ya Rais Samia Korea Kusini atasaini Mkopo wa Tsh. Trilioni 6.51