Tetesi: Prof. Kitila Mkumbo kuchuana vikali na Nyalandu jimboni

Umhh Dr. Nyalandu toka lini ? Bavicha kwa kupamba visivyopambika
Sina uhakika na u DR wa Nyalandu lakini sioni ajabu kwa hilo. Kuna watu wengi sana wanazo PHd lakini hawatangulizi kiungio hicho cha Dr katika kujitambulisha. Lakini wale wapenda ujiko ndio mmmh!
 

Kutokuchaguliwa hilo nimelisema tangu hawali kama ndo hilo unapinga basi pitia mchango wangu utaona msimamo wangu
Usidandia treni kwa mbele
Mm nilichokiongeza hapa ni ile kauli kwamba mnyiramba anadhauriwa na mnyaturu kitu ambacho si kweli
Ndio maana nikaongeza nyama kwamba mnyiramba ndiye aliyesoma kuliko mnyaturu,ata mnyiramba anamdharau mnyaturu kwa kuwa hakusoma,wanyaturu walibaniwa fursa ya kusoma na Muslim,iramba wamisionari walijikita Kule na waliwapa fursa ya kusoma,kupitia makanisa watu walielimika kusoma ndio maana wanyiramba wengi wamesoma

Ata kimaendeleo iramba kuko juu huwezi fananisha na unyaturuni uko unakosema ilongero,mntinko mgori n.k
Naongea kwa kuwa nayajua hayo maeneo na mkoa kwa ujumla
Ingawa si mwenyeji wa huo mkoa

Kuhusu wanyiramba wangapi wametoa mchango kwa taitfa sidhani kama kuna sehemu pamebandikwa orodha ya wanaotoa mchango wa namna yeyote kwa taifa maana ata wewe huwa unatoa mchango kuhusu idadi hilo litakuwa swali gumu k wangu
Kitu kingine kwa taifa hili ili ujulikane labda uwe mwanasiasa vinginevyo siyo rahisi ata profesa mkumbo tunamjua kwa kuwa ni mwanasiasa
Ila iramba kuna wasomi wengi tofauti na unyaturuni maprof na maphd wapo wengi tu ata vyuoni waadhiri

Kama utapingana na mm basi siku moja kaa na mzee wako atakwambia ukweli

Kuhusu seminari,sikusema hayo maeneo uliyoyaorodhesha kuwa yana seminari sema kwa vile umeguswa nadhani umekuja kwa jaziba ila ukweli ndo huo,Muslim waliwabania shule wanyaturu ndo maana hawakusoma waliowengi unyaturuni waliopata fursa ya shulle ni wakristo nadhani hilo unalifahamu ila unabisha tu
Ata huyo nyalandu katoka familia ya kikristo ndo maana alipata fursa ya kwenda shule
 
Na yule mhasibu wa Takukuru ni wa Chadema sio au Leo akitangaza naacha kazi na najiunga Chadema atakuwa mtakatifu! Au vipi?
Mbona unatoa mifano ambayo haiendani? Kwanza una umri gani mkuu? Maana isije ikawa najadiliana na mwanafunzi wa chekechea.
 
Wakuu, mimi bado narudia kusema hivi: Njia ya ushindi kwa Dr Nyalandu ipo wazi kabisa. Anyway, let us wait and see what will happen ila mtakuja kuniuliza. Nyalandu ni mchapakazi hodari na wala hana kashfa yoyote kama CCM wanavyojaribu kuonyesha hasira zao baada ya yeye kuhamia CHADEMA. Aidha, Dr Nyalandu ameiletea Singida Kaskazini maendeleo ya kutosha ndio maana wamekuwa wakimchagua kuwa mbunge wao kwa muda wa miaka 20 mfululizo. Msidhani kwamba Wanyiramba ni mazombie, wanajitambua sana.
 
Huo ni mtazamo wako wewe binafsi uharisia bado unasubiliwa kutoka kwa wapiga kura
 
Mkuu kwa Nyalandu ni Wanyaturu na huyo Kitila anatoka kwa Wanyiramba. Kule atokako Mwigulu
 
Mkuu kwa Nyalandu ni Wanyaturu na huyo Kitila anatoka kwa Wanyiramba. Kule atokako Mwigulu
Eti nimesikia baadhi ya wanaCCM wanajinasibu kwamba hata akishinda Nyalandu watamtangaza Kitila! Hizi naziona kama dua za kuku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…