Prof. Kitila Mkumbo: Tanzania haitakubali kupangiwa marafiki wala maadui

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amesema ziara za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan nje ya nchi zinalenga kutafuta washirika wa biashara na uwekezaji badala ya wafadhili, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa falsafa ya kuifungua Tanzania kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Akiwasilisha Bungeni Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2025 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2026/27, Prof. Kitila amesema Tanzania itaendelea kutafuta fursa za biashara na uwekezaji bila kuchagua upande wowote wa kisiasa duniani.

Amesema ziara ya Rais Samia nchini Urusi ni sehemu ya mkakati huo wa kutafuta washirika wa maendeleo na si misaada, huku akisisitiza kuwa Tanzania haitakubali kuchaguliwa marafiki au maadui na taifa lolote.

Prof. Kitila amesema msimamo huo si mpya kwani ulianzishwa tangu enzi za Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, aliyesisitiza kuwa Tanzania itadumisha urafiki na mataifa yote kwa misingi ya kuheshimiana, usawa na kutokuingiliana katika masuala ya ndani ya nchi nyingine.

Amesema Serikali itaendelea kushirikiana na mataifa mbalimbali duniani kwa lengo la kufungua fursa za biashara, uwekezaji na maendeleo kwa manufaa ya Watanzania.

Washirika wa biashara sawa swali je sisi tunashindwa nini kufanya biashara hadi tutafute washirika
 
Kitila, endelea kuongeza chumvi hadi mboga ishindwe kuliwa! Badala ya kubalance shobo unaendelea kuwa chawa mwandamizi wa aliyekuteua ili uendelee kubugia keki ya taifa.
Hivi nikiwaita maprofesa mliojazana huko ccm kuwa ninyi ni wasomi wajinga nitakuwa nimeasifia kikamilifu?
Maisha ni haya haya mafupi, huyo Profesa anapata riziki yake huko huko alipo, wewe unaendelea kuzeeka ukitukana na kuwalaani wanaopata riziki zao, inakusaidia nini?.

Unazeeka na machungu moyoni wenzio wameuona ufupi wa maisha wameamua kumtumikia kafiri wanapata mradi wao.
 
Screenshot_20260604_105123_X.jpg
 
Hawa ndio wanafanya maprof waonekane mafala...
Haya mambo ni bora kukaa kimya kwa sababu hao unaowaambia haya wakiamua kukomaa na wewe nchi itapotea....hizo nchi si chadema....
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amesema ziara za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan nje ya nchi zinalenga kutafuta washirika wa biashara na uwekezaji badala ya wafadhili, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa falsafa ya kuifungua Tanzania kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Akiwasilisha Bungeni Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2025 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2026/27, Prof. Kitila amesema Tanzania itaendelea kutafuta fursa za biashara na uwekezaji bila kuchagua upande wowote wa kisiasa duniani.

Amesema ziara ya Rais Samia nchini Urusi ni sehemu ya mkakati huo wa kutafuta washirika wa maendeleo na si misaada, huku akisisitiza kuwa Tanzania haitakubali kuchaguliwa marafiki au maadui na taifa lolote.

Prof. Kitila amesema msimamo huo si mpya kwani ulianzishwa tangu enzi za Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, aliyesisitiza kuwa Tanzania itadumisha urafiki na mataifa yote kwa misingi ya kuheshimiana, usawa na kutokuingiliana katika masuala ya ndani ya nchi nyingine.

Amesema Serikali itaendelea kushirikiana na mataifa mbalimbali duniani kwa lengo la kufungua fursa za biashara, uwekezaji na maendeleo kwa manufaa ya Watanzania.

What surprises me ni kuona kila mtu anaweka mapambio kutetea ziara ya Russia- president, mawaziri, wabunge, machaw
 
Kama hapangiwi marafiki au maadui asiwe tayari pia kupokea misaada yao halafu tuone kama hizo suti anazovaa humo bungeni atazinunua kwa kutumia nini? Mpuuzi mkubwa!
 
Kauli yake itawakela USA na Ulaya, kauli imekaa kimipasho sana bora angekaa kimya

Awamu hii ya 6, wanajiamini sana, anguko lipo karibuni
Upo vizuri Mkuu. Unajua kanuni za Kiroho na dalili zake. Kiburi kikifika kileleni,anguko li mlangoni.

Ee Mungu tuongezee siku za kuishi
 
Back
Top Bottom