Prof. Kitila Mkumbo: Ushauri wa Kishujaa umesababisha Tanzania ishtakiwe katika Mahakama za Kimataifa. Wasomi wetu waliwadanganya Viongozi

Bi nafsi kuhuasu hili la madini JPM alifanya vizuri, maana alitetea mali za wa Tanganyika ilhali yeye ni Rais wa Tanzania.
Tuwe wakweli, madini sio mali ya Tanzania/Muungano, bali ni mali ya Tanganyika. Kiuhalisia kuvunja mkataba wa Tanganyika ni hadi Tanganyika mwenyewe, ila kuusaini kumpa muekezaji tunasaini kwa niaba ya wananchi wa Tanganyika.
Kwani serekali haina pesa ya kununua karasha na kuchimba madini yenyewe? Kama uwezo upo wa kifedha kwanini haifanyi?
Mali isiyo ya muungano, ki mataifa huiuzi wewe raisi wa muungano bila makubaliano ya wewe na mwenye mali, utaishia kuuza kwa mwekezaji akupe kesh mkononi. Vipi utamlaumu raisi wa muungano kwa jambo ambalo sio la muungano? TUWE WAKWELI.
Wa Zenji tunawaona wajinga wakidai kero za muungano ziishe na tunawaita wabishi, ilhali wanatutetea.
Ki mataifa wanajua fika kuwa kuna mali za Tanganyika mbali, mali za Zanzibar mbali na Muungano/Tanzania mbali.
Raisi wa Muungano anahisika na mambo ya Muungano, hayo mengine ni sio yake, ila kwa 7bu ukubwa ni jalala sawa na tumtupie tu.
Alitetea Kwa mdomo
 
..wasomi walimuendekeza Magufuli na kumwambia mambo anayopenda kusikia, badala ya kumwambia ukweli na uhalisia.

..matokeo ya ushauri huo wa " kishujaa" serikali imeburuzwa mahakamani mara kadhaa, imeshindwa kesi, na kulazimika kuingia hasara ya kuwalipa wawekezaji fidia.
Mkuu nina imani kuwa Wewe na Magufuli picha zilikuwa haziendi kabisa na bila shaka una sababu zako binafsi kuliko Uhalisia.

Niseme tu kwamba sisi watu ni wepesi sana kulaumu matokeo wakati hawajui wala.hatutaki kujua chanzo kilicho sababisha matokeo hayo, iwe hata mpira wa miguu. Kazi ya manazi au mashabiki ni kulaumu ama kushangilia matokeo lakini sii maandalizi na utekelezaji wake.

Ni hivi mkuu, tatizo kubwa tulonalo Tanzania ni la KIMFUMO. Na tatizo linaanzia kutokuwa na Azimio la Kitaifa kama wakati wa Mwalimu. Azimio la Zanzibar lipo kimaandishi tu lakini halitumiki kiutawala haswa kwenye UWEKEZAJI. Kila rais anayeingia madarakani anakuja na mfumo wake hakuna restrictions za.kudumu.

Haya Makampuni ya nje yanakuja kuwekeza kutokana na sheria zetu butu. Huenda kusajikiwa (register) kwa address tu na wakapewa liseni. Ambayo huenda kutafuta Ama kufanya utafiti wa biahara hiyo. Hizi liseni zinapatikana kirahisi sana tena hata kwa njia za nyuma lakini halali (registered). Fedha yako tu.

Wapo matapeli na wapo Wawekezaji wa kweli ambao wote nia na dhanira yao ni KUCHUMA kilichopo kutokana na mfumo mbovu. Mfano mdogo chukulia Chalinze Cement ni kampuni ilosajiliwa lakini hawana kiwanda wala ofisi lkn wana liseni halali kabisa hivi sasa ni mjadala Bungeni

Kwa hiyo, mfumo wetu tunasajili Makampuni ya nje kibao tena kwa misifa lakini haya makampuni mengine ni hewa hawakuja kuwekeza hawana hata mitambo ya utafiti wala ni ya biashara ila kuna mchongo fulani.

Sasa inapokuja gundulika baadae tumeingizwa chooo cha kike kutokana na udanganyifu wa Shirika tunawanyang'anya liseni zao ama tunafuta mikataba yao. Kumbuka mkuu tofauti na Leo na wakati ule tunatawaliwa ni ndogo sana. Tulitawaliwa baada ya sisi kuwakaribisha Wageni hao kwa nia njema kabisa, lakini dhamira yao ni ile ile KUJA KUCHUMA nchi zetu na mafao wapeleke Makwao. Tofauti ni kwamba leo tunasema wanatulipa kodi lkn madini na faida yote ni mali yao. Na zinaenda nje.

Sasa anapotokea Kiongozi ambaye hataki kabisa rasilimali zetu ziwafaidhishe wageni badala ya sisi wenyewe kuwa hapo ndipo ngoma inapoanzia. Kumbuka Azimio la Zanzibar bado lilikuwa na azimio ya kummilikisha Mwananchi uwekezaji wowote japo kwa ubia usiopungua asilinia 51.

Tuliondoa sheeia hizo tukarahisisha sheria ili.kuvutia Wawekezaji na bahati mbaya sana sii wote walokuja kwa nia jema. Tumeona Mahoteli wakibadilisha majina kila baada ya miaka mitano ya nafuu ya kodi. Sii huko tu imefikia mpaka kwenye miradi mikubwa kuzidi kutqka nafuu ya kodi ilihali sisi hatuna share kabisa!

Binafsi nipo na Magu katika hili, naamini kabisa Wachimbaji wadogo wa madini Tanzania au Qlwakulima wetu, wavuvi wetu, Wafugaji wetu wana impact kubwa katika mendeleo ya Taufa hili kuliko haya makampuni ya nje. Sioni sababu kabisa ya kuvutia Wawekezaji wa nje ikiwa sii maswala ya uwekezaji kiwanda cha Tech! Kama cha magari, kumputa, simu au hata kusadiaha na kukata madini hapa hapa nchini.
j
Hivyo, kwa jinsi tunavyosajili makampuni ya nje kuja kuwekeza nchini ndivyo tunavyo jiweka katika hali mbaya zaidi ya kushtakiwa huko mbeleni. MIKATABA MIBOVU ndio xhanzo cha kesi hizi na sii maamuzi yetu kuvunja mikataba hiyo!

Naamini hakuna KILIMO kinachomshinda Mtanzania mpaka tulete mwekezaji kutoka nje - HAKUNA. Wala hakuna Madini tunayoweza kushindwa kuwekeza sisi wenyewe isipokuwa kwa hofu ya kuogopa kivuli chetu wenyewe.

Hii mikataba holela tunayoingia na Mashirika ya nje kwa kuondoa masharti ili kuwavutia ndio chanzo cha kesi za kesho! Unamvutia mwekezaji anayekuja kukuibia ati ajira? Kwani Mkoloni alikuwa hatupi ajira? Kwa nini tulitaka kumuondoa ikiwa wazee wetu waliajiriwa na Mkoloni?..
 
..sikumkubali Magufuli kutokana na tabia zake za KIKATILI dhidi ya wapinzani.

..Mambo aliyoyafanya Magufuli kwa wapinzani, Waingereza hawakuthubutu kuyafanya dhidi ya wana Tanu.

..Kwa mfano, Magufuli alifungulia wapinzani makesi mengi ya uongo na kuwafunga ukilinganisha na idadi ya wana Tanu waliofungwa na Muingereza.

..Lakini ukiacha mtizamo wangu huo dhidi ya Magufuli, ukweli unabaki kwamba sakata lake dhidi ya makampuni ya madini lilikubigwa na ulaghai na propaganda za kisiasa.

..Kila Mtanzania anajua kwamba we are not getting a fair deal ktk mikataba yetu na makampuni ya madini. Sasa kilichotakiwa kufanyika ni kufanya uchunguzi wa kitaalamu na kutoa ripoti na madai ambayo tunaweza kuyatetea popote-- ndani au nje ya nchi.

..Magufuli na wataalamu wake walitoa ripoti ambazo sio za kweli. Matokeo yake hakuna anayeweza kuzitetea ripoti zile.

..Ripoti za Magufuli na wataalamu wake zimetunyima nafasi kujua uhalisia wa tunachopoteza ktk sekta ya madini.

..Kwasababu hatujui tunachopoteza, basi tumeshindwa hata kujua tunawadai nini wawekezaji, na hata hicho walichoahidi kutufidia hatujui kama ni stahiki yetu, au bado tunapunjwa.
 
Hizi sasa ni Siasa kumbe?!! Sasa wewe ulutaka afanye kama William Ruto? Aruhusu Mikutano na maandamano wakati Upunzani hawakumtambua yeye na Shein toka wanaapishwa? Ujue Magufuli alichukiwa na pande zote ndani ya CCM mtandao wa Lowassa na Membe na huku UKAWA ambao waliikosa Katiba Mpya chini ya JK. Hasira zao wote ilikuwa JPM.

Magufuli alichukua nchi katika hali na wakati mbaya sana maana CCM ilikuwa chali! na kosa jingine alipochukua sera za Upinzani ambao kiaina zilikuwa za mwalimu Nyerere ziliwakwaza wengi na Upinzani wenyewe wakamgeuka kutokana na mtandao wa Lowassa.

Kwa hiyo, Mtandao wa Membe, Lowassa ulohamia Chadema wote walikuwa against him. He was left alone akaweka imani yake kwa Wananchi. Imani ambayo leo CCM ina sauti kwa Wananchi. Kama sii yeye sidhani kama CCM wangekuwa na sauti hata ya kusema wamayosema leo hii..

Mambo mengi yalofanyika wakati ule ilikuwa LAZIMA
Aliweka zuio la Mikutano na maandamano kwa sababu hakutambuliwa na Upibzani toka anaingia madarakani. Now, just imagine ingetokea nini kama angeruhusu! Kenya ingekuwa na afadhali maana huku Lowassa (Chadema) Membe (ACT) na halafu wote hawamkubali.

Kina Lissu hawa walifikia mpakankusaka.nyaraka za Seeikali dhidi ya kesi kama hizi za madai. Yaani walikuwa tayari kuisaidia Acacia dhidi ya Tanzania sio Magufuli kwa malipo ya Ndululu.

Mwisho, nakuomba sana usifananishe kabisa utawala wa Mkoloni na Magufuli kwa sababu vyama.vile vyote vilifanya kazi ya Mkoloni kwa matakwa na masharti ya Mkoloni. Uhuru tulopewa haukuhusiana na UCHUMI bali tuoandishe BENDERA jambo ambalo walilazimika kufuata matakwa ya UN, lakini bado tulibakia member of the (CommonWelath). Undani wa Hii Common - Wealth ndio unatubana kwenye mikataba..
 
Na kuhusu report ya Magufuli. Mkuu kamchezo kamechezwa baada ya kifo chake. Kila.kitu tunaambiwa sii kweli ilihali rais alitangaza wazi wazi mbele ya Watanzania walichokubaliana. Leo mnabadilishiwa maneno na kuambiwa haikuwa hivyo. Kila mtu mwoga kusema ukweli. Sioni ajabu UNAFIKI wa.Watanzania maana ni moja ya mila zetu. Hii ni sawa na Familia moja baada ya kufa mzazi wao wanadai ile wosia (WILL) haikuwa halali...
 
Heshima kwako JokaKuu . Huyu jamaa ni wale wale tu. Haya alitakiwa ayaseme wakati yanafanyika na siyo kusubiri baada ya kuona Magufuli and co hawapo kwenye ulaji ndiyo aseme. Nina uhakika hata Magufuli angekuwepo mpaka sasa asingesema haya. Jamaa nimeshamdharau sana huyu na hana tofauti na hao anaowasema.
Kwa utawala ule ungekuwa ww ungesema?
Alafu baada ya kusema unafikilia Nini kingefuata!!
 
..tunakosea kumchambua Kitila Mkumbo binafsi.

..njia sahihi ni kuchambua hoja aliyoitoa.
Tunamchambua yeye binafsi ,ili watu wajue vizuri kwamba ana historia ya kuforge vitu na si mkweli.Je ,wakati wa JPM ,kwann hakuongea anayoongea?Hii ,Ina maana kwamba historia Ina mhukumu kuwa ni mhongo na mnafiki.Hafai kabisa .Ni mchumia tumbo.
 
Hizi sasa ni Siasa kumbe?!! Sasa wewe ulutaka afanye kama William Ruto? Aruhusu Mikutano na maandamano wakati Upunzani hawakumtambua yeye na Shein toka wanaapishwa? Ujue Magufuli alichukiwa na pande zote ndani ya CCM mtandao wa Lowassa na Membe na huku UKAWA ambao waliikosa Katiba Mpya chini ya JK. Hasira zao wote ilikuwa JPM.

Magufuli alichukua nchi katika hali na wakati mbaya sana maana CCM ilikuwa chali! na kosa jingine alipochukua sera za Upinzani ambao kiaina zilikuwa za mwalimu Nyerere ziliwakwaza wengi na Upinzani wenyewe wakamgeuka kutokana na mtandao wa Lowassa.

Kwa hiyo, Mtandao wa Membe, Lowassa ulohamia Chadema wote walikuwa against him. He was left alone akaweka imani yake kwa Wananchi. Imani ambayo leo CCM ina sauti kwa Wananchi. Kama sii yeye sidhani kama CCM wangekuwa na sauti hata ya kusema wamayosema leo hii..

Mambo mengi yalofanyika wakati ule ilikuwa LAZIMA
Aliweka zuio la Mikutano na maandamano kwa sababu hakutambuliwa na Upibzani toka anaingia madarakani. Now, just imagine ingetokea nini kama angeruhusu! Kenya ingekuwa na afadhali maana huku Lowassa (Chadema) Membe (ACT) na halafu wote hawamkubali.

Kina Lissu hawa walifikia mpakankusaka.nyaraka za Seeikali dhidi ya kesi kama hizi za madai. Yaani walikuwa tayari kuisaidia Acacia dhidi ya Tanzania sio Magufuli kwa malipo ya Ndululu.

Mwisho, nakuomba sana usifananishe kabisa utawala wa Mkoloni na Magufuli kwa sababu vyama.vile vyote vilifanya kazi ya Mkoloni kwa matakwa na masharti ya Mkoloni. Uhuru tulopewa haukuhusiana na UCHUMI bali tuoandishe BENDERA jambo ambalo walilazimika kufuata matakwa ya UN, lakini bado tulibakia member of the (CommonWelath). Undani wa Hii Common - Wealth ndio unatubana kwenye mikataba..

..nazungumzia Magufuli kutumia vyombo vya dola na mahakama dhidi ya Watanzania wasiokuwa na makosa yoyote.

..unasema CCM ilikuwa chali, na Magufuli aliogopa mtandao wa Membe, na Lowassa. sasa hofu hiyo ya Magufuli inahusiana nini au inahalalishaji uteswaji na vifungo bila hatia vya vijana wadogo kama Peter Lijualikali, Joseph Mbilinyi, Mdude Nyagali, na wengine wengi?

..kuhusu suala la Lissu hata tukisema ni kweli alitafuta nyaraka za serikali, je ni halali kumuua kinyama kama walivyojaribu? Hivi ni makosa Mbunge kupewa nyaraka na taarifa sahihi kuhusu mikataba ya serikali? halafu mbona Deo Mwanyika waliyedai alikuwa anashirikiana naye amepewa Ubunge na huyohuyo Magufuli? Mbona yeye Magufuli na timu yake walikuwa wana-negotiate na Accacia / Barrick? Je, walikuwa hawabadilishani nyaraka?

..mwisho, hatukupewa Uhuru ili Watanganyika/Watanzania wadhalilishwe, kuteswa, na kuuwawa, na Waafrika wenzetu. Wazungu wakitutesa na kutuua tunaweza kusema wanafanya wakati sisi sio ndugu zao. Sasa ikitokea Mtanzania mwenzetu anakuwa katili dhidi yetu kuliko Wazungu tunapaswa kujisikia namna gani? Je, tunatakiwa tunyamaze tu?
 
Tunamchambua yeye binafsi ,ili watu wajue vizuri kwamba ana historia ya kuforge vitu na si mkweli.Je ,wakati wa JPM ,kwann hakuongea anayoongea?Hii ,Ina maana kwamba historia Ina mhukumu kuwa ni mhongo na mnafiki.Hafai kabisa .Ni mchumia tumbo.

..inawezekana mambo yote uliyosema dhidi ya Prof.Kitila ni ya kweli, lakini yote hayo hayahalalishi kupuuza hoja aliyoitoa bungeni. Je, nchi inaingia hasara kwa kuvunja mikataba kiholela kwa madai kwamba ni uzalendo? Je, wasomi walitoa ushauri wa kweli, au walitoa ushauri kuendana na haiba na matamanio ya Raisi / Magufuli?
 
Na kuhusu report ya Magufuli. Mkuu kamchezo kamechezwa baada ya kifo chake. Kila.kitu tunaambiwa sii kweli ilihali rais alitangaza wazi wazi mbele ya Watanzania walichokubaliana. Leo mnabadilishiwa maneno na kuambiwa haikuwa hivyo. Kila mtu mwoga kusema ukweli. Sioni ajabu UNAFIKI wa.Watanzania maana ni moja ya mila zetu. Hii ni sawa na Familia moja baada ya kufa mzazi wao wanadai ile wosia (WILL) haikuwa halali...

..Unafiki ni kushangilia na kusifia wakati tunajua kabisa kwamba Magufuli alikuwa anasema uongo.

..Unafiki wa Watanzania ni kukaa kimya, na wengine kusifia, wakati Magufuli akitumia vyombo vya dola na mahakama kutesa wapinzani.

..Baadhi yetu walijitoa ufahamu huku mambo ya hovyo yakifanywa na watawala.
 
Daaah hivi kuna wakati watu wanashangilia na kukaa kimya kama sasa hivi? Neno CHAWA sii limeanza majuzi tu.

Ebu rudia nyuma itazame michango ta watu kati ya mwaka 2015 hadi 2020 halafu fananisha na sasa! Sikiliza hasira za watu utaambiwa ati watu walikuwa hawasemi, wanaogopa! All Lies ushahidi upo hapa hapa JF.

Magufuli alisifiwa kwa kazi inayoonekana! Iwe ujenzi wa Miundombinu, kuondoa kodi kandamizi, kuwaruhusu Machinga na Mama Ntilie, kuwasaidiwa watu wanyonge walodhulumiwa papo kwa papo na vinginevyo. Hakuna alomsifia kwa sababu anafunga watu infact Msigwa aliachiwa huru na fedha za Magufuli na Sugu alitoka jela kwa msamaha wa Magufuli. Sugu huyu alimpa Tulia kudole cha kati akitoka Bungeni. Umesahau?

Aidha kama alikosea kwa kufanya hivyo unaweza nambia. Mimi binafsi nilimsifia kwa SERA zake, walofanya kina Bashite hayo nitamhukumu Bashite mwenyewe! Lakini wakati wake kosa la Bashite ni la Magufuli yaani hata Polisi ni Magufuli. leo hii kosa la Mwigulu, January, Bashe, sijui nani ni kosa la mhusika sio Mama. Mbaya wenu alobakia ni Mbunge Mpina wakati huyu anatetea maslahi ya Wananchi.

Wakati wa Magufuli hata Mwanasiasa akihama nchi wanasema Magufuli, kumbe wengine wameona mchongo wa kwenda nje kujipa wao Mashoga au Wakimbizi wa Serikali kumbe ni Bashite kawafungulia njia.

Hizi Siasa.mkuu wangu watu wanazitumia kwa.manufaa yao. Magufuli alipingwa kwa sababu za kimaslahi. Bashite anatukanwa sana kwa sababu huko Ulaya lazima watumie kigezo chake wapate sheria. Huyo huyo Akirudi huku analaani Ushoga na kudai yeye sii Mkimbizi. Alaaaa so what is what..All this shit, has nothing to benefit Tanzanians, be smart..
 
Mpango upi wakati wanadai cost za damages!! kilichobakia ni utekelezaji wa uhukumu sio kupewa leseni. Yaani miaka 5 Sasa hajachimba kitu Leo alainike kisa amerejeshwa nchini? Zile cost za miaka 5 atazifidia nani?

Haya makampuni kweli ni yakinyonyaji lakini ni CCM wenyewe mmeingia hii mikataba so mnapoivunja msitumie ujuaji maana hela za hongo mmekula alafu mnakiuka makubaliano mnategemea Nini?
Wanaona aliyopo wana mmudu kama yule kafungua kesi amelipwa na mimi ngoja nikafungue kesi lazima nilipwe. Sasa mtu amekaa na lessen miaka nenda rudi hafanyi chochote kwa ni wasinyanganywe. Mbona akina sumaye hapa walinyanganya baad ya kushindwa kuendeleza na ndo sheria inavyotaka hivyo
 
Hizo leseni wengine walipata toka enzi za Mkapa na hakuna cha maana walichofanya.

Achilia mbali sheria na regulations mkataba pia una ‘performance clause’ umepewa eneo uchimbe madini; sio ulihodhi tu.

Uwezi kazi kwanini uachiwe umiliki tu, hizo kesi watashindwa sio kwa sababu serikali ilikosea, wameingia na kuvuruga strategy waliyoikuta na kufanya mambo kwa staili wanayoijua wao wenyewe.
Wanafanya hav Ili wamkomoe Marehamu" poor Tanzania "
 
Kesi za namna hiyo kwa wenzetu wengine wasio na uzalendo huzitumia kama ni Fursa !! Na ndicho tunacho tahadharisha !! Lakini huenda tunajisumbua tu maana Uzalendo uliobakia ni msamiati wa kizamani !!
Yes you commented like intellectual person not like chawa chini ya samia kila mtu anachungulia fursa tu
 
Mkuu ngoja nikueleweshe... Hayo madai ya toka mwaka 1974 yalikuwa yakilipwa kidogo kidogo kila mwaka,
Mwinyi alipunguza, Mkapa alipunguza, Kikwete alipunguza..

Sasa tukapata eti mzalendo no moja.. Akakataa.....
Kuna kesi imeisha juzi juzi, Serikali itatakiwa kulipa Billioni 290 ..kama sikosei.. Na kosa lilifanyika 2016 kwa Serikali kuchukua ardhi kwa nguvu maeneo ya Bagamoyo na kumpatia Bahresa kujenga kiwanda cha sukari..

Ile ardhi ilikuwa ya mwekezaji wa nje.. Jiwe akatuma wasaidizi wake wakafyeka kila kitu kwenye hiyo ardhi..Kisha wakampa hati mpya Bahkresa..

Hapo yote yanafanyika kwa Jiwe mwenyewe na washauri wanampamba bila kujua kwamba watu wakienda mahakamani itakuja kuleta hasara kwa Serikali
Uanjua sheria ya ardhi lakini tena kwa mujibu wa katiba huyo mwekezaji alikuwa anamwekeza nini mpaka ardhi ikachukualiwa .mbona sheria ipo wazi tu kama haujaendeleza ardhi .inachukuliwa .
 
Sheria zipo wazi lakini mikataba mingi imesainiwa kwa sheria za nje. Kama tunaweza kiuka Katiba ya nchi unadhani kuna Ugumu kukiuka Sheria ndogo za nchi? Yapo mashamba kibao yamelala miaka. Na yapo machimbo ya madini bado hayaja vumbuliwa, tuendako ni kiza.

Nakumbuka shamba moja la ngano kule Karatu, ulikuwa mradi wa Canada ulikufa ghafla! Sababu siijui leo tunaagiza ngano nje. Hilo shambawatu wanagawana ardhi na wanapewa liseni ya umiliki na hawalimi ngano. Ipo siku kitawaka halafu tuanze kushikana mashati.

Nchi imeliwa sana na kibaya zaidi watu wanatazama kesi badala ya kutazama MIKATABA yenyewe ambayo tuliipigia kelele sana kabla ya Uchaguzi wa 2015.

Leo hii watu wote wamegeuka! Wanaita Wawekezaji wengine kwa mtindo ule ule ulotuingiza matatizoni.
 
Sijui hilo jina la 'zithromax' uliliokota wapi kwa akili kama unazoonyesha hapa!
Mwenye ufahamu wa mambo yanayohusu hilo jina hawezi kuwa na akili za kipuuzi namna hii.
Jibu huyu jamaaa anamadanikio gani ndugu kwenye hizo kesi mpaka umsifie hivyo
 
Wanaona aliyopo wana mmudu kama yule kafungua kesi amelipwa na mimi ngoja nikafungue kesi lazima nilipwe. Sasa mtu amekaa na lessen miaka nenda rudi hafanyi chochote kwa ni wasinyanganywe. Mbona akina sumaye hapa walinyanganya baad ya kushindwa kuendeleza na ndo sheria inavyotaka hivyo
Wapi hizo kesi zinasema wamenyang'anywa kwa sababu ya kutoendeleza migodi?

Umeambiwa wamefutiwa leseni sababu hawakucomply na regulations mpya za 2018.

Kingine issue sio JPM, mbona na yeye aliweka kifungu cha kwamba mashtaka yote yasikilizwe na mahakama za ndani ila mabeberu walipokataa ikabidi wafute hicho kipengele.
 
Hakupewa ardhi ahodhi akisubiri soko likae vizuri ndio afanye uwekezaji wenye tija. Mkataba wake ulitaka aangalie kama madini yapo, achimbe wote tupate. Mtu kapotea halafu anataka amiliki ardhi afanye udalali.

Ukitaka kuona utapeli wote hao madai yao sio kurudishiwa mikataba yao ili kuendeleza shughuli za uchimbaji wa madini.

Wao wanadai compensation tu ya kunyang’anywa ardhi ni watu ambao walikuwa hawana hela ya hiyo shughuli wamechukua ardhi, wamehodhi, wanasubiri wanyang’anywe washitaki serikali wavune kirahisi; na huu ndio muda wao.
Mkuu umeeleweka vyema sana uzi ulipaswa kuishia hapa kitumbua kama zito junior kama hatakuelwa basi
 
Mkuu 'Rasbamba; hebu tulizana kidogo utueleze utaratibu wenyewe hasa upoje katika kupewa ardhi huko wanakopewa hao watafuta madini.
Hii ardhi huwa wanapewa hati miliki ya eneo husika, kama kwa mfano ugawaji wa viwanja unavyofanyika?

Katika utaratibu huo mwekezaji hupewa masharti gani ya kuyatimiza.

Inaelekea kuwa na ufahamu juu ya swala hili, hebu tufafanulie vizuri ili tujue makubaliano yahusuyo uwekezaji wa namna hiyo.

Jibu lako hapo juu ulilompa 'Mayor', kidogo halijitoshelezi, nadhani ulchukulia tu kwamba wasomaji watakuwa wanajua unachozungumzia. Fafanua kidogo sote tupate uelewa.
Simple tu kama ule mkataba aliosaini kikwete wa bandari ya bagamoyo na mingine ndo ilisainiwa kwa muundo huwa mtu anakuja na bla Bla eti ni mwekezaj hana chochote
 
Back
Top Bottom